L/G
Hii inatokana na Nini? Na sitaki kuamini ni Africa nzima tupo hivi ila ningependa niwasilishe hii Kwa nchi hii pendwa ya Tanzania
Kwanini? Ni police force na sio police service, unakuta police anaogopwa na raia hata akihitaji ushirikiano na wananchi wanaweza wakamuhepuka Kwa kuogopa kuishiwa gerezani au mahabusu, asikari wa Tanzania sio rafiki wa wananchi wake mda mwingi yupo teari Kwa kutumia mabavu tu, mpaka unakuta raia wanawachukia asikari wao wakati wapo Kwa kuwalinda
Na mbaya zaidi hii ipo Kwa vitengo karibia vyote vya asikari Tanzania wao wababe na wanajiona wao ndio wao yaani hakuna mtu anamwambia kitu, hii ni mbaya sana kitaifa/kinnchi
Kitafutwe kitengo hata kimoja kiwe police service Kwa raia wake, itapendeza na itasaidia sana, wawepo asikari ambao hawashiki bunduki adhalani Wala kumpiga raia kibao Ili na sisi tuwapende na tushirikiane nao
Nilipita nchi kadhaa hapa Africa, nimepata experience Kwa asikari wa mataifa kadhaa, aisee kwenye sector ya asikari tupo nyuma sana na tunadhani tumeweza lakini sio kweli
Baadhi ya nchi hapa Africa Asikari ni rafiki wa raia na hazina machafuko Wala waalifu wengi ila ikifika zamu ya police force wapo asikari watakuja kutuliza fujo
Tanzania ipo chini ya police force na sio police service.