Je tunayo orodha ya makampuni makubwa 100 hapa Tanzania? Hii itatupa kigezo cha kutengeneza orodha ya matajiri wa Kitanzania.Ila nijuavyo ni kwamba utajiri mkubwa wetu bado umelala (latent). Na yule anayeonekana tajiri sana, bado yuko mbali sana na matajiri wa Dunia. Tujipe moyo kwani Africa ya Kusini, Misri, Sudan na Nigeria sasa wako kwenye orodha ya matajiri wa dunia.