Tanzania tunahitaji mabadiliko ya kila kitu lakini siyo amani yetu

Victor Mlaki

JF-Expert Member
Joined
May 1, 2016
Posts
5,628
Reaction score
6,411
Tanzania inasubiri kwa hamu maamuzi sahihi ya watu wake, maamuzi ambayo yataukilia mustakabali mzima wa Taifa katika wakati uliopo na wakati ujao.

Watoto wa Taifa hili kwa kujua au kutojua wanaangukia katika maamuzi ya Watanzania wenye sifa za kupiga kura. Kura yako moja ina thamani kubwa sana kwa sababu imebeba mustakabali wa Taifa.

Tumeanza kushuhudia mabadiliko mengi yenye kiwango tofauti katika Nchi yetu lakini ni jambo la pekee sana ambalo Mungu ametukirimia kuwa Taifa lenye amani.

Tunahitaji mabadiliko zaidi, kasi ya maendeleo zaidi na uongozi bora mara dufu lakini hauhitaji kamwe amani yetu kubadilika au kubadilisha na mtu au kikundi chochote cha watu kwa maslahi yao binafsi au ya wafadhili wao kuvuruga tangamano letu la kitaifa na amani yetu.

Tunatamani watoto wetu waendelee kutabasamu wakifurahia uwepo wa Wazazi wao juu ya ardhi bora na yenye baraka zote iliyopita Tanzania. Ninatamani maisha niliyoishi kwa miongo mitatu na ushee yaliyonifanya kuamini maisha ni popote kwenye Mama Tanzania yawe pia ni maisha ya kizazi changu.

Tanzania 2020 hatuhitaji kufuata utaratibu tu wa kufanya uchaguzi kila baada ya miaka mitano ila tunahitaji kufanya uchaguzi sahihi, wakati sahihi, maamuzi sahihi ili kumpata Kiongozi sahihi.

Hatuhitaji kumchagua mtu kuwa Rais ili kubadilisha vyama vinavyoshika dola, hatuhitaji kumchagua mtu kwa sababu anakosoa sana, hatupaswi kumchagua mtu kwa sababu ni jasiri na haogopi kitu, hatupaswi kumchagua mtu kwa sababu ya kumuona huruma.Watanzania tunapaswa kujua kwa dhati kabisa kuwa tunachokichagua mara zote ni "Amani yetu".

Tunachagua amani kwanza ndipo tunaangalia Kiongozi tunayemuona atafaa kuulinda " Uhuru na Umoja wetu".

Tusimchague yeyote yule kwa sababu tu anatamani sana nafasi ya Urais, tusichague mtu kwa sababu ana marafiki wengi ndani na nje ya Nchi. Ninadhai Watanzania tunafahamu masuala yetu ambayo ndiyo yanayotufanya tumtafute mtu wa kutuongoza kuyatimiza.

Nitatumia ujuzi wangu wote kuhakikisha ninamuelewesha kila mtu kuelewa masuala kwanza kabla ya kumuelewa Mtu kwa sababu masuala ya Tanzania ni muhimu kuliko kuwajadili watu. Huu siyo wakati sahihi hata kidogo kujadili watu badala ya masuala ya msingi ya Taifa hili.

Nitakuwa sehemu ya kuwaambia watu wote wanaonizunguka kuwa hatupaswi kumchagua mtu yeyote mwenye maandalizi yya kuishi nje ya Ardhi ya Tanzania kwa sababu zozote zile.

Tutampinga mapema sana mtu yeyote ambaye hata kwa kuhisi tunaweza kuona dalili za kuja kulipa kisasi kwa sababu kazi ya Kiongozi ni kuunganisha watu na siyo kugawanya watu. Hatuwezi kuruhusu nafasi kubwa kiasi hicho kuchukuliwa na mtu ambaye tunaona kila dalili ya kugeuza dola kulipa kisasi na watakaoumia ni sisi wenyewe.

Tanzania imetufadhili sana hatutakubali fadhila hizi ambazo ni kwa neema za Mungu tu tuzichezee.
 
Hii mbinu ya kutisha watu achaneni nayo . hakuna mwenye mawazo ya kuvuruga amani
Tayari mnaanza kukosa pumzi, pumzi ya mwisho mnaanza vitisho vya sijui Amani imefanyaje
Uzeni sera mkuu
 
hii mbinu ya kutisha watu achaneni nayo . hakuna mwenye mawazo ya kuvuruga amani
Tayari mnaanza kukosa pumzi, pumzi ya mwisho mnaanza vitisho vya sijui Amani imefanyaje
Uzeni sera mkuu
Amani ndiyo suala la msingi mno kwa Taifa letu kuliko watu, kuhubiri amani ni uhai wa Taifa hili.
 
Amani ndiyo suala la msingi mno kwa Taifa letu kuliko watu, kuhubiri amani ni uhai wa Taifa hili.
Wasioitaka amani ni wale wasioitaka haki. Wewe unaomba kura huku unajiamini ni wewe nasi wengine !!. Tunazidiwa sana na wenzetu
 
Bila haki amani ni pambio tu masikioni mwa watu- Unawaambia wanao wawili au watatu kuwa atakayeshinda hiki utampa kitu fulani, Mshindi anapatikana na anaonekana lakini ulichoahidi unampa mwingine na visingizio vingi utafikiri aliyeshinda atakuwaje?
 
Asante, amani siku zote ni tunda la haki. Hakuna amani bila haki.
 
Kwani kibiti amboni na ikwiriri waliotaka kuvuruga amani walikuwa warundi au wasomali si ni watanzania au! !
hii mbinu ya kutisha watu achaneni nayo . hakuna mwenye mawazo ya kuvuruga amani
Tayari mnaanza kukosa pumzi, pumzi ya mwisho mnaanza vitisho vya sijui Amani imefanyaje
Uzeni sera mkuu
 
Bila ya haki hakuna amani, kilichopo sasa ni uvumilivu ambao unakwenda kwisha kama haki haitakuwepo.
 
Mnahubiri "Amani" bila "Haki" mnatuona mataahira.. Kajipange tena ndio uje uandike tena.
 
NDUGU WA CCM NI

Unafiki
Utesi
Dhulma
Uuwaji

Na partner wao mkubwa ni SHETANI
 

Lakini CCM mmetoka mbali sana,kutoka kulaghai wasiolewa mpaka kutumia mabavu,kunyanyasa na kuua
Indeed it's a big step na mengi yajayo yanafurahisha kwa watu wa MUNGU na yachukizayo kwa watu wa SHETANI
 
Lakini CCM mmetoka mbali sana,kutoka kulaghai wasiolewa mpaka kutumia mabavu,kunyanyasa na kuua
Indeed it's a big step na mengi yajayo yanafurahisha kwa watu wa MUNGU na yachukizayo kwa watu wa SHETANI
Unaweza kutoa ushahidi wa moja kwa moja wa aliyeuliwa na chama ulichokitaja hapo? Andiko langu halijataja vyama wala halina uhusiano na kujadili watu au vyama. Tujadili masuala kwanza.
 
Mithali 14:34
Haki huinua taifa; Bali dhambi ni aibu ya watu wo wote.

Vv
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…