SoC02 Tanzania tunahitaji mapinduzi ya kisekta

SoC02 Tanzania tunahitaji mapinduzi ya kisekta

Stories of Change - 2022 Competition

Luqman mohamedy

JF-Expert Member
Joined
Jul 24, 2016
Posts
899
Reaction score
1,231
Tanzania tunahitaji kufanya mapinduzi makubwa katika sekta kadhaa ili kuiifikia nchi ya ahadi tunayoitamani.

Kuna mambo kama matano kwa mtazamo wangu ikiwa tutachukua hatua kubadilisha nadhani kila kitu kitabadilika

(1)Mapinduzi katika Sekta ya Elimu

(a)Kubadilisha Mfumo wa Elimu.
[emoji117]Kutoka 7-4-2-3 kwenda 6-3-2(Miaka 6 primary 3 Sekondsri 2½ chuo cha ufundi stadi/taaluma) Tutatoa wasomi wanaoweza kujitegemea kwa muda mfupi.
[emoji117]Jenga vyuo vya ngazi ya diploma na cheti vya kutosha nchi nzima.
[emoji117]Tubadilishe Mtaala(Curriculum)
•Iweke wazi aina ya wahitimu tunaowahitaji mwisho wa masomo
• Ipo outdated ni muda sahihi wa kuambatanisha kila somo na mabadiliko ya technolojia
•Elimu iwe ya udadisi zaidi(reserch oriented) kuliko kukariri,lengo la elimu iwe kuleta mabadiliko ya msomaji na mazingira yake sio kupata cheti na GPA kubwa.

-Wanafunzi wanakuwa wanasaidiwa na kupewa project kuwnzia ngazi ya chini.
•Mtaala uwe 50-50% Theory😛ractical,kwa wenzetu walioendelea wanafunzi wa chemistry husoma lab na kila kitu huonyeshwa,Geography na History hupelekwa location nk.

(b)Uwekezaji mkubwa katika elimu
[emoji117]Ujenzi wa Vyuo Vya ufundi stadi vyenye hadhi ya kutoa elimu ya Diploma.
•Kama ilivyofanyika mapinduzi ya elimu kwa ujenzi wa shule za kata 2010 umebadilisha mfumo wa elimu na mfumo wa maisha kwa ujumla kwa muongo huu ujenzi wa hivi vyuo utabadilisha mfumo kwa maisha yetu yote.

-Mapato ya TRA ni zaidi ya 2trTsh+Faida kwenye huduma za serikali 3trTs Est =5trTsh..Chuo kimoja cha ufundi au cha kitaaluma 8bnTsh .Few percent ya hii hela inaweza jenga vyuo kumi kila mwezi.Tukikopa tukajenga pia ni uwekezaji mzuri.

[emoji117]Kuongezwe ajira kwa walimu kwa siku zako 100 za kwanza kuna shule zina walimu 2 wanafunzi 1000,hata kama elimu ni bure ila sio bora.

[emoji117]Serikali itoe elimu bore ya chuo kikuu au kila mwanafunzi apatiwe mkopo 100% bila kujali katokea wapi.

2.Uwepo wa mpango wa Taifa sio ilani ya chama.
[emoji117]Kama nchi tumefeli kwenye kupanga,tunafeli kwenye kutekeleza na tutafeli kwenye maisha kiujumla.

[emoji117]Kama nchi hatuna mpango ila kama chama wana mpango uliopangwa na wachache(kamati kuu ya CCM) bila kushirikisha wengi lakini utekelezaji wake unalazimisha hadi wajumbe washiriki.

Nini ufanye?
Andaa mdahalo wa kitaifa kuanzia ngazi ya mitaa mpaka taifa kisha chuja mawazo nini wananchi tunataka kianze sio kutuamulia.

[emoji117]Litengenezwe jopo la wataalamu na wadau husika wa mipango iliyoteuliwa watengeneze mpango kazi ambao serikali itatafuta vyanzo vya mapato na kusimamia utekelezaji.

(3)Kuunganisha sekta zinazotegemeana
[emoji117]Serikali yetu kila sekta inajiendesha kivyake haina mwanzo wala mwisho,kuanutengano mkubwa sana.
[emoji117]Kuna baadhi ya sekta lazima ziungane mfano sekta ya kilimo X Sekta ya viwanda-Lazima ijulikane wakulima wakilima vinaenda wapi
[emoji117]Sekta ya Teknolojia X Elimu X Viwanda

(4)Mapinduzi kwenye mfumo wa uongozi
[emoji117]90% ya watumishi ni bendera fata upepo atakaloanzisha mh week hoi wataenda nalo wiki nzima na wao.
[emoji117]Bunge limepoteza uwezo wa kupanga lipo kwenye malalamishi tu.
[emoji117]Baraza la mawaziri linafanya kazi kwa mihemko hawna mipango kazi.
[emoji117]Uwazi katika budget na mipango ya kiserikali.

(5)Uwekezaji kwenye vijana
[emoji117]Tunashauri kuwe na budget maalumu kwaajili ya kuwekeza kwenye vijana.
[emoji117]Yaundwe makundi ya vijana wenye taaluma zinazofanana wapewe mikopo yenye riba nafuu,watafutiwe masoko na majukwaa ya kutangaza bidhaa zao.

[emoji117]Hii itaamsha mfumo na mzunguko wa uchumi,60% ya nchi ni vijana 40% hawana ajira au shughuli zinazoeleweka.
 
Upvote 0
Back
Top Bottom