MADELA,
Huo unaouita unyonge ulitupataje?
Au tulizaliwa nao?
Basi tunahitaji uhuru utakaotuondolea unyonge.
Unaongea kinyume chake.
Mwalimu Nyerere aliondoa unyonge wake binafsi kwanza kama mtanganyika, akakubali lolote liwalo na liwe akajiingiza katika siasa na kaamua kutoa mapendekezo ya kubadili maazimio ya TAA ya kudai mambo madogo madogo ya kutaka kujifananisha au kuwa equated sawa na wazungu na kudai uhuru kamili.
Uhuru jambo kubwa kuliko mambo yote.
Futa unyonge kwanza kisha Dai Uhuru.
Aliondoa unyonge kwa kujielimisha.
Aliondoa unyonge wake kwa kuwaambia watu wengine haki zao kama binadamu.
Aliondoa unyonge wake kwa kukubali kuacha kazi ya ualimu pale Pugu ilo mpa maslahi makubwa katika mazingira ya unyonge ili kuunganisha nguvu za wanyonge wengi nakudai Uhuru.
Mtu mnyonge hawezi kusimama mbele ya bwana wake mkoloni na kudai Uhuru, hawezi kufanya hivyo kwa sababu pingu za unyonge wake hazitomwacha.
Mtu mnyonge hana muda wa kupambana na unyonge wake, ila ana muda wa kufikiria machungu yatakayo mpata, au kile atakacho kosa kwa kuingiza jeuri yake na kujikweza juu ya unyonge.
Unyonge tumeuvaa kama nguo, wakituambia unyonge wetu unatupendeza tunakubali na tunazidi kuuwekea matarizi juu yake na hata kujivunia.
Hata hapa JF ukisoma maandiko ya watu wengi tu utaona wazi jinsi wajivuniavyo unyonge wao kwa nguvu zao zote na akili zao zote.
Ukisikia watu wa kawaida kabisa Tanzania wanapiga stori nakusema kwamba Tanzania ni nchi ya Amani huku wana njaa hawajala tangu jana jioni na sasa ni saa 6 au 7 ya mchana wako nje ya baraza wanapiga stori na mekoni hakuna msosi unajua hawa ni watu waliovaa unyonge na wanajivunia hali yao ya unyonge kwa kujidanganya.
Ukisha jua kwamba wewe ni mnyonge kazi kubwa uliyo nayo ni kupambanua mambo yakufanyayo kuwa mnyonge.
kujua tu kwamba wewe ni mnyonge si suluhisho.
Kuorodhesha mambo yakufanyayo kuwa mnyonge ni hatua muhimu.
Kujenga mkakati wa kupambana na kila kikupacho unyonge ni muihimu zaidi.
Muhimu kuliko vyote ni kujitolea muhanga kuingia katika mapambano ya kujitoa katika unyonge kwa kuvunjilia mbali yale yakufanyayo kuwa mnyonge biala kuogopa wala kujali matokeo.
"Wale jamaa wa vizazi na vifo hawakupi cheti cha kuzaliwa mtoto wako mpaka uwape kitu kidogo"
Chukua hatua, andika barua kwa kingunge mwenyewe wa vizazi na vifo, toa malalamiko yako rasmi peleka kopi kwa mbunge wako na kwenye gazeti unalo liamini na kama unamwanasheria mtumie.
Ukikubali kutoa kitu kidogo unadumisha unyonge.
Mara nyingi tunazidiwa na mchecheto wa hofu ya kuchukuliwa hatua kwa ujeuri wetu wa kudai haki na kukubali hali halisi hata kama kwa namna zote hali ile haturidhiki nayo.
Haki ni haki yako, lakini mara ngapi katika maisha ya kila siku yasiyohusisha viongozi wa serikali umepata kunyimwa haki??
Unaweza kunyimwa haki yako kwakupambikwa sifa isiyo yako.
Mwoga yule.
Atatufanya nini yule?
Hebu tumfanyizie tuone atafanya nini!
Atathubuti ana roho ya kuku yule.
Wakati mwingine ni lazima sauti yako isisike ili uweze kupata kilicho haki yako.
Mtu anaweza kumwita mkeo chemba na kuanza kumtongoza huku wewe unasikia wazi wazi, kwa sababu shati la unyonge lime kukaa vyema unajifanya hujui kinachoendelea.
Fedha yake, Msuli na ukubwa wa kifua chake wala cheo chake kamwe visitumike kuendeleza unyonge wako.
Kule Busanda wananchi wanazomea viongozi wa CCM.
jiulize kwa nini?
Watu wale wametambua kwamba kila siku wanadanganywa kwa ahadi za uongo kwa sababu wao ni wanyonge. Ili kukomesha aina yote ya uongo, mara kiongozi akianza kusema uongo watu wanazomea.
Zamani tuliamini kabisa kwamba tukimzomea kiongozi wa kitaifa nguvu zote za serikali zitatuangukia kma wimbi la Sunami.
Kwa kutambua kwamba unyonge wetu ni vazi la manyasi tuwezalo kulivua tukitaka, tumeanza kujenga utamaduni wa kuwapa majibu yao viongozi wote wanaothubutu kuendelea kututia katika unyonge.
Tuna wabunge wengi sana pale Bungeni ni wanyonge kuliko Bibi yangu kule Malinyi.
Wametumwa kwenda kuwasemea wananchi ili kuharakisha maendeleo yao, lakini wamefika kule, wamegawiwa au kuvishwa majoho yaunyonge na kushindwa kujenga hoja nzito dhidi ya ujuha mwingi ufanywao na watendaji wa serikali na mashirika yake.
Mbunge mara zote anafanywa mjinga kwa kupewa nafasi za hapa na ple katika vyombo fulani iliaendelee kupata per DM na sitting allowance.
Wabunge jeuri hunyimwa nafasi za kuwapa kipato cha ziada, ukiwa jeuri sana wanakupa nafasi ili wapate kukumaliza kama wanavyo jaribu kummaliza bwana mdogo Zitto.
( Zitto bado nakuamini endeleza moto)
Unaweza kuvaa suti pande tatu lakini bado u mnyonge.
Unaweza endesha VX na GX za nguvu lakini bado u mnyonge.
Kile kikuzuiacho kutumia nafasi yako uwezo wako kama mtu kama mwakirishi kama sheikh kama padri kusema ukweli hadharani ndicho kikupacho unyonge.
Kile kitupacho unyonge mara nyingi tumedhani ndicho kitupacho shibe na raha kidogo tuliyo nayo. Kwa kudhani hivyo mara zote nafsi na hisia zetu zimeshindwa kuturuhusu kupambana na unyonge wetu kwa sababu kupambana na unyonge wetu ni kama kupambana na kile kitupacho na kilindacho uhai na utu wetu.
Amen