Tanzania tunajenga uchumi wa kisanii?

Tanzania tunajenga uchumi wa kisanii?

kamili

JF-Expert Member
Joined
Feb 10, 2011
Posts
1,217
Reaction score
853
Jana rais Kikwete amesihi suala la kuwekeza kwenye science, lakini maneno yake hayaendeni na kinachoendelea. Hebu fikiria ni mara ngapi kwa siku umeona vipindi kwenye vyombo vya habari kama tv, video, redio au magazeti wakionesha au kuongelea vipindi vya kisanii kama muziki au moves?

Je ukisafiri kwenye mabasi huwa wanaonesha nini hasa kwenye video? je ulishawahi kuona vipindi vinavyoonesha mafanikio katika elimu, mifugo, kilimo, au biashara? Je kwa mifano hiyo vyombo vyetu vya habari vinafinyanga bongo za watanzania ili tuwe nani?

Je vipindi kama TMT, bongo star such, na vinavyofanana na hivyo ni kwa nini hupata wasailiwa wengi kupindukia lakini sijawahi kuona mfano kama huo kwenye elimu, kilimo, au biashara.Nimeona washindi wa vipindi hivyo wakipata zawadi hadi sh. milioni 50, lakini je washindi wa form four au form six hupata zawadi ya sh. ngapi? Na je hutangazwa kwa kurudiwa rudiwa kama inavyofanyika kwenye vipindi vya kisanii?

Mfano mwingine miaka ya hivi karibuni kumezuka wanasiasa vijana mahiri na wenye ujasiri kwa kusema wanavyofiki bila ya uwoga, je kuna chombo gani cha habari ambacho kinatoa speech zao kwa kurudia rudia ili kuwahamasisha vijana wasome kwa bidii waje wawe viongozi shupa-vu baade?

Je kuna taifa duniani ambalo limeendelea kwa usanii tu? Waalimu na wazazi wanalalamika kila siku kuwa watoto hawataki kusoma, je si kwa sababu bongo za watoto wetu zinafinyangwa kisanii?

Nawasilisha
 
Usanii waanzia ngazi za juu
Bandar yajengwa bagamoyo sio Tanga au Ntwara.
Kiwanda cha juice chajengwa Bagamoyo sio Lushoto au Muheza.
Usanii wa ajabu
 
Back
Top Bottom