Tanzania tunakopa lakini uwezo wa kusimamia fedha hizo na miradi hatuna. Tuboreshe sheria kupambana na ufisadi

Tanzania tunakopa lakini uwezo wa kusimamia fedha hizo na miradi hatuna. Tuboreshe sheria kupambana na ufisadi

Sir robby

JF-Expert Member
Joined
Jun 22, 2022
Posts
2,396
Reaction score
4,080
Watanzania sio kama tunapinga nchi yetu kukopa, kinachowafanya wananchi waonekane kuogopa nchi kukopa ni uwezo mdogo wa watendaji wetu wa kusimamia miradi mikubwa na pia ufisadi mkubwa wa fedha unaofanywa na watendaji "Report ya CAG" imebainisha na pia hakuna hatua zozote zinazochukuliwa na mamlaka husika zaidi ya kulindana.

Ndio maana wananchi wanataka Katiba mpya ili Sheria nyingi ziboreshwe ili kudhibiti ubadhilifu wa fedha za umma na miradi.

Nchi nyingi zilizoamua kukopa zimeboresha kwanza sheria zake ili yeyote atakaye fuja mali ya umma achukuliwe hatua kali.

Mfano ni nchi ya China, na ndio maana wamefanikiwa kiuchumi.
 
Back
Top Bottom