Tanzania tunatakiwa tubrand chips mayai

Yu wili iti ende drinki enethingi yu wanti. Delishazi miti izi oso availabo. Iti izi apu tu yu bebi buu ๐Ÿ˜‚
๐Ÿ˜‚๐Ÿ˜‚๐Ÿ˜‚๐Ÿ˜‚๐Ÿ˜‚๐Ÿ˜‚๐Ÿ˜‚๐Ÿ˜‚๐Ÿ˜‚๐Ÿ˜‚๐Ÿ™Œ๐Ÿพ๐Ÿ™Œ๐Ÿพ๐Ÿ™Œ๐Ÿพ
 
Mr. President. Shida ya chips ipo katika mafuta yanayotumiwa katika kuzikaanga. Mafuta hayo huchemshwa sana na mara nyingi hurudiwa rudiwa. Hii ni hatari sana kwa afya ya mfumo wa usambazaji damu mwilini (cardiovascular system).

Tafiti mbalimbali zimeanza kuonyesha kuwa mafuta yanayotokana na mbegu (mf. Karanga, alizeti, zabibu, canola, pamba, mahindi) siyo mazuri maana yana kiasi kikubwa cha Omega 6. Omega 6 ikizidi mwilini inaweza kusababisha matatizo mengi ya kiafya. Na mafuta haya yanapaswa kuandaliwa katika joto la kawaida na kamwe hayatakiwi kutumiwa zaidi ya mara moja. Sasa chips zetu hizi unakuta mafuta yamerudiwa rudiwa mpaka yamekuwa meusi kama oil ya kwenye gari. Hii ni hatari sana!

Mafuta pekee yanayopigiwa upatu ni Virgin Olive oil na yale yanayotokana na mbegu za maparachichi. Hata haya inabidi yaandaliwe katika joto la kawaida (olive oil) na yasirudiwe rudiwe kupikiwa.

Chips yai zikipikwa kwa moto wa kawaida kwa kutumia mafuta salama (virgin olive oil au avocado seed oil) na zikaliwa mara moja moja ni chakula salama.



 
Siku hizi kuna air fryer, viazi unanyunyizia tu mafuta zinatoka chips fresh kabisa. Hoja ya chips zina mafuta si hoja tena.
 
Kweli mimi mtu wa Mara niseme habari za chipsi mayai dah. Tusameane kaka
 
Pale nini inavunja nguvu za kiume? Mayai ni afya na tunayala daily,
Viazi ni wanga ile, sasa ni kipi hasa? mafuta au?
Watu wanaongea vitu wasivyovijua au kuwa na ufahamu navyo.

Kimsingi kabisa chips na mayai ni vyakula vizuri vyenye virutubisho kama vyakula vingine.

Tatizo kubwa ni mafuta yanayotumiwa kukaangia hivyo chakula hasa kwa wanaofanya biashara wanatumia mafuta hayo hayo kukaangia kwa kuongeza mafuta mapya na kuchanganya ya zamani.

Kisayansi katika kemia hayo mafuta yametengenezwa kwa muunganiko wa carbon na hydrogen bond.

Kinachotokea ni kwamba kama mafuta yatatumika mara moja au mbili hayana madhara kwa sababu structure yake au muundo haubadiliki sana.

Kwa hiyo kwa wanaopika nyumbani tuseme unapika chips au unakaanga halafu unatumia mafuta hakuna madhara yoyote hasa kiafya.

Kwa wanaofanya biashara wanatumia mafuta yale yake kukaangia kinachotokea yanabadilika structure navkupelekea kuwa carcinogens( visababishi vya saratani) na magonjwa mengine ya mishipa ya damu na moyo( coronary heart disease)

Kwa maana hiyo chips mayai kama zinapikwa home huwa hazina tatizo ni chakula kizuri tu.

Ukitaka kufahamu ubora wa chips unazokula kabla ya kuagiza nenda jikoni kagua mafuta wanayotumia kukaangia, cheki na karai au vifaa vitunikavyo kukaangia utaweza kupata picha halisi. Ukikuta mafuta machafu utayaona tu hata chips zinabadilika rangi na kuwa rangi ya brown au nyeusi.
 
Mkuu una uhakika uko sawa?
Mbona nyuzi mfululizo
Kwani ni kosa kufungua nyuzi mfululizo mbona jamiiforums hawalalamiki
Kwamba nikitumia haki yangu kama member nakua na matatzo ya akili??? Je kwenye hizo nyuzi kama zina makosa kwanini usimwambie moderator azifute
 
 
Uko sahii
Ndo maana nimesema chips mayai yenyewe haina shida hila kujua imepikwa na mafuta gani kwa sababu swala la kupikwa na mafuta ya aina ipi hio ni ishu nyingine
 
Maduka ya home appliances.
The one we have tuliletewa na wale waarabu wanauza electronics door to door
Ina muda gani ikiwa inafanya kazi? Kama ni durable na haina vipengele vya mara kwa mara, unaweza kuniambia ni brand gani mkuu? ASANTE ๐Ÿ™๐Ÿฟ
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn moreโ€ฆ