Tanzania tunatia aibu wenzetu wanasonga kwenye democracy

Kamundu

Platinum Member
Joined
Nov 22, 2006
Posts
9,780
Reaction score
15,488
Nchi kama Zambia, Malawi , Kenya, Botswana zimeona mbali sisi tumebaki na wizi wa kura na uchawa. Tupiganie nchi yetu

Huyu ni Wakili wa Rais Duma Boko amewasili katika Hotuba ya Bajeti ya mwaka 2026 iliyofanyika katika Parliament Buildings jijini Gaborone

Your browser is not able to display this video.
 
Nchi kama Zambia, Malawi , Kenya, Botswana zimeona mbali sisi tumebaki na wizi wa kura na uchawa. Tupiganie nchi yetu
Nilikushauri uwe na heshima!, hi Nchi ni ya CCM, watu wake ni mali ya CCM, katiba ni ya CCM na kura pia ni za CCM!, one can not steal from oneself, hakuna wizi wowote kwasababu mtu huwezi kujiibia kitu ambacho ni chako mwenyewe, ni unakuwa ni umechukua!. Uchaguzi wetu ni igizo tuu la uchaguzi, kinachofanyika kwenye uchaguzi ni
unachukua ...
unaweka....
malizia....!
P
 

Tunakujua brother wetu umekuwa chawa mkubwa wa Samia. Samia na genge lake wameuwa na kuiba kura huo ndiyo ukweli. Umekuwa mwepesi wa kusingizia sheria ili kujifurahisha nafsi lakini bro ukweli ni huo. Nakuomba sana kwa sisi tunao kuheshimu na kukupenda usiharibu legacy yako kwa kutetea mambo ambayo yanarudisha nchi nyuma. Achana na uchawa na kujaribu kuwa kati wakati mambo yako wazi kwa kiasi hiki. Hii nchi watu wanatekwa tu, uchaguzi unaibiwa na ruhswa imekuwa utamaduni sasa kwanini bado unatetea hawa jamaa! inasikitisha na tutakuweka kwenye maombi seriously.
 
Sasa uwajibikaji unakuja vipi bila demokrasia?

Yaani kama hauwajibiki kwa wananchi, kwanini mtu ufanye kazi?

Na pia unapataje mandate ya kuongoza?

Na checks and balances zitatoka wapi bila demokrasia?
China hayo mambo yakoje?!..democracy ipo kwenye mataifa kwa miaka mingapi?.. kabla ilikuaje?
 
China ni society tofauti na yetu, hatuna maadili kama yao so tukiacha politburo ya watu wachache iamue kila kitu inazaa majizi tu.
Hapa zitto junior kaongea point sana. China huwezi kuwa na utekaji kama hapa Tanzania , rushwa ukishikwa ni kitanzi au jela mfano mkuu wa majeshi wa sasa yupo kwenye kesi ya rushwa. Hapa Tanzania Raisi kajaza ndugu zake kwenye uongozi fake, rushwa kila mahali, mtoto wake anapiga madili kila siku , kuhonga machawa kama hawa wa mitandao. Hatuwezi kuendelea bila demokrasia. Azimio la Arusha lilishindwa kwasababu waliwaiga China ikashindikana

zitto junior kosa kubwa sana mlifanya ni kuiongia kwenye chaguzi itawachukuwa miaka mingi sana kurudi kuaminika
 
@zitto junior kosa kubwa sana mlifanya ni kuiongia kwenye chaguzi itawachukuwa miaka mingi sana kurudi kuaminika
Mkuu kwenye mazingira kama yale what are the chances Chadema tungepata hata kiti kimoja? Nadhani tungeambulia maybe majimbo 3 tu labda na viti maalum 10+ ila that's it.

Na je tungekua na credibility ya kudai uchaguzi haukua huru ilihali tumeshiriki na "kupewa" viti vichache.

Nadhani kutoshiriki ni kutoa fursa kwa watawala kujitafakari na kuleta reforms kuliko kushiriki na kulalamika tu kama ACT au CUF wanachofanya sasa
 
Unamaanisha na sisi tuchague rais shoGa ili tukidh demoklasia uipendayo
 
Leo umeandika vyema mkuu paschal, nimekupa na like. Ni mpaka watu watakapoamua kujitoa kwenye gereza la CCM ndo kutakuwa na uchaguzi ambao si igizo. Si kwamba naichukia CCM bali matendo yake ndo mabovu tu na ndo ninayochukia.
 
China ni society tofauti na yetu, hatuna maadili kama yao so tukiacha politburo ya watu wachache iamue kila kitu inazaa majizi tu.
Kwani wakati wa nyerere kulikua na democracy hapa,ghuba kuna democracy?
Democracy haiangalii society ni mfumo wa siasa unaweza kufanyika popote pale
 
Demokrasia peke yake haina maana.

China haina Demokrasia kama yetu lakini wako maili elfu moja mbele kimaendelea kuliko sisi.

Akili ya mtu mweusi tukubali kabisa Ina kasoro kubwa sana.

Unawezaje kukabidhi kila kitu, bandari, mbuga, dhahabu, airport, na Rasilimali zote watu wa nje au kuzipiga mnada, halafu unaenda kuomba misaada ????

Angeishi hapa Tanzania mzungu miaka kumi tu ya kimkakati tungeshudia tofauti ya akili ya mweusi na mzungu.
 
Kwenye kila kitu. Kama wataka kujua kwa kiasi gani Tanzania kama nchi, na kama watu, tulivyochelewa nenda nje. Nchi yoyote ile.
Kama haijaendelea Ki nchi (majengo, barabara, viwanda, mpira... ) itakuwa imeendelea Ki wananchi (elimu, employment, amani na usalama) Hata Msumbiji!
 
Mnachezea nchi sana nyie watu wa CCM, watu wanatekwa, kuuliwa na wengi wako jela kama kina Lisu wanateseka, civil wars nyingi na umaskini uliokithiri ni siasa chafu kama za CCM, nini maana ya uhuru tuliopata kama hata kura tulizopiga hazihesabiwi, nchi inaelekea shimoni kwa hizi akili na kila mtu ataumia
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…