SoC04 Tanzania tunayoitaka ndani ya miaka 5, 10, 25

SoC04 Tanzania tunayoitaka ndani ya miaka 5, 10, 25

Tanzania Tuitakayo competition threads

Chacha sanawa

New Member
Joined
Jun 16, 2024
Posts
1
Reaction score
2
TANZANIA TUNAYOITAKA NDANI YA MIAKA 5,10,25

Tanzania ni nchi iliyopo Afrika Mashariki ambayo inaongoza kuwa nchi ya amani na upendo kwa makabila mbalimbali pamoja na Nchi mbalimbali ambayo ina maziwa, mito, bahari, mbuga za wanyama, misitu, Ndege wazuri, uoto wa asili na sifa nyinginezo nyingi N.k

Sifa za Tanzania tunayoitaka ni kuwa na viongozi bora wanaopiga rushwa vita, wanaotoa huduma safi isiyo na ubaguzi kwa watanzania, wanaotatua kero za watanzania

Kuwa na madaktari wenye huruma na upendo kwa wagonjwa

Kuwa na watalaam mahiri kwenye kutatua migogoro ya Ardhi

Kuwa na Askari polisi wanaofanya upelelezi bila manyanyaso na mateso kwa mtuhumia ile hali bado Mahakama haijamtia hatiani

Kuona mabwana shamba wanatoa elimu ya kilimo kule vijijini na kuwasimamia wakulima toka kuandaa shamba hadi kuvuna ili kupata mazao bora na sio bora mazao

Kuona mabwana Afya wanazunguka vijijini kutoa elimu ya Afya kwa jamii ikiwa ni pamoja na madhara yatokanayo na uchafu au kutokuwa na vyoo kwasababu kule vijijini wengi hawana vyoo wanajisaidia kwenye vichaka

Kuona huduma bora za Afya na za kisasa zinatolewa katika vituo vya Afya vilivyopo vijijini

Kuona wenyeviti wa vijiji hawauzi Ardhi kwa wageni kutoka katika nchi nyingine Mfano kutoka Kenya hii inaweza pia kuleta madhara kwa taifa

Kuona elimu ya mlipa kodi inatolewa katika shule za msingi, kuona wafungwa wanapungua magerezani

Kuona watanzania wanawezeshwa vyema katika matumizi ya Gesi asili ili kutunza mazingira,

Kuona mikataba ya kibiashara na nchi nyingine inawekwa wazi na faida ya mikataba hiyo ianishwe vyema

Kuona wafungwa wanakula milo mitatu kwa siku kwasababu nao ni binadamu kuna wengine wamepelekwa kule kwa kusingiziwana wengine kww bahati mbaya

Kuona watoto wetu kwenye mashule wanakuwa na usimamizi mzuri hasa kwa mabinti ili kuepuka mimba za utotoni

Kuona Mahakama zinatenda haki kwa uharaka zaidi ili kupunguza mlundikano wa mashauri Mahakamani

Kuona vyombo vya habari vinapewa uhuru wa habari

Kuona haki za watoto zinalindwa, haki za wakina mama zinalindwa,haki za wakina Baba zinalindwa,kuona mabaraza ya kata yanafanya kazi kwa mujibu wa sheria za Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

Kuona Mabaraza ya Ardhi na Nyumba ya Wilaya yanatenda haki kwa uharaka ili kumaliza migogoro ya Ardhi kwa Watanzania

Kuona chanel za ndani ya nchi zinaonyeshwa bure tofauti na sasa ambapo zinalipiwa kwa Mfano Stertimes,

Kuona huduma ya mawasiliano inapelekwa vijijini hasa sehemu ambazo minara haijawahi kujengwa

Kuona walimu wanafundisha somo la kilimo kuanzia shule za msingi

Kuona huduma za makanisa zinakuwa na sehemu maalumu siyo katika makazi ya watu ambapo kunakuwa na kelele hata usiku

Kuona elimu ya madini inatolewa kwa wachimbaji kabla hawajaanza kuchimba, kuona mikataba ya madini inapungua hapa Tanzania

kuona wanafunzi katika shule za msingi wanafundishwa Masomo angalau manne kwa siku siyo somo moja au mawili ninayoyaona kwa sasa.

Ninachoamini mawazo hayo yote yakifanyiwa kazi Tanzania tunayoitaka itakuwa hivyo

Ahsante sana naomba kuwasilisha
Ni Mimi
Chacha Manga sanawa.
 
Upvote 8
Back
Top Bottom