SoC04 Tanzania tunayoitaka ni ile yenye macho ya kuona kizazi cha tatu na cha nne kutoka hivi sasa

SoC04 Tanzania tunayoitaka ni ile yenye macho ya kuona kizazi cha tatu na cha nne kutoka hivi sasa

Tanzania Tuitakayo competition threads

promisegeofrey2012

New Member
Joined
May 31, 2024
Posts
2
Reaction score
0
Ili kuendana na kasi ya mabadiliko ya kisiasa, kiuchumi, kielimu, kiteknolojia pamoja na kiutamduni hatuna budi kuhakikisha baadhi ya mabadiliko katika mfumo mzima wa ajira kuanzia ngazi ya chini, mpaka ngazi juu yanafanyika, ili kufanya malengo ya taifa ya maendeleo ya muda mfupi, kati na muda mrefu yanafikiwa.

Licha ya kuwepo sera, sheria na kanuni mbalimbali za ajira kwa watumishi wa umma, na hata wale wa binafsi imeonekana wazi kuwa bado suala la ajira limegubikwa na changamoto mbalimbali, ikiwemo mazingira mabovu ya kazi, upungufu na ubovu wa vitendea kazi, watendaji, migogoro, upendeleo katika michakato ya kuajiri pamoja ufinyu wa bajeti serikalini.

Kulingana na hali hiyo serikali inapaswa kubuni mbinu na namna mbalimbali za kukabiliana na changamoto zinazoikabili sekta ya ajira nchini kwa kufanya mambo yafuatayo.

1. Kuweka mifumo ya wazi na ya kufikika katika suala zima la kuajiri wafanyakazi wa serikali.

2. Kugawa ajira za serikali katika aina kuu tatu
(a )Ajira ya mkataba kulingana na dira ya maendeleo ya miaka mitano,5
(b) Ajira ya mkataba kulingana na dira ya maendeleo ya miaka 10-20
(c) Ajira ya kudumu iendane na dira ya maendeleo ya taifa kuanzia miaka 25_50
Hii yote ni kuendana na dira za maendeleo za muda mfupi, kati na muda mrefu, na kila aina mkataba iwe na malengo yanayopaswa kufikiwa hali, ambayo itachagiza ufikiwaji wa malengo ya kudumu ya kitaifa.

2. Iundwe sera madhubuti ya kitaifa juu ya uendeshaji wa shughuli mbalimbali serikalini ambayo itasimamiwa na watu wote watakaofanikiwa kuwa viongozi, sera ambayo haitakuwa na sura ya chama wala mrengo wowote wa kisiasa, kiitikadi wala kidini.

3. Kupunguza nafasi za ajira za kuteuliwa na kuunda mpango maalum wa kuwachuja watendaji wa serikali wanaokuwa kwenye vyeo mbalimbali mfano, wakuu wa wilaya na mikoa, makatibu,wenyeviti na wakurugenzi ili kutoa fursa ya kupata watendaji wenye uadilifu, na uchapakazi uliotukuka, tofauti na sasa ambapo teuzi hizo hutokana na historia za kujuana, na itikadi za kisiasa.

4. Kubuni sera na mitaala ya kielimu iliyojikita katika kupandikiza bunifu mbalimbali,kuanzia elimu ya awali, msingi, sekondari na elimu ya juu ambazo zitapunguza mrundikano wa upungufu wa ajira pale ambapo wahitimu mbalimbali wanapokuwa wamehitimu masomo yao, kwani wengi watakuwa wamejiajiri.

5. Kuanzishwa kwa sheria na kanuni kali za kuwawajibisha watendaji na watumishi wa umma wanapokuwa wazembe makazini, hali itakayochochea umakini na uwajibikaji kwa watumishi hao.

6. Kuboresha maslahi ya watumishi wa umma hali itayochochea uwajibikiji, kujituma, uzalendo pamoja na kupunguza rushwa inayosababishwa na ukosefu wa kipato pamoja na kuboreresha kima cha chini cha mshahara, kiendane na mabadiliko ya mfumuko wa bei.

7. Katika ajira za sekta maalumu ikiwepo elimu, afya na usalama serikali itilie mkazo ujenzi wa miundombinu imara, pamoja na kuboresha mazingira ya kazi,kuongeza vitendea kazi vya kutosha, kutoa motisha na zawadi kwa watendaji bora na kuwapatia makazi bora na usafiri wa nafuu ili kuwarahishia utendaji kazi wao.

8. Elimu na semina mbalimbali, mafunzo kazini na warsha mbalimbali zifanyike ili kiboresha utendaji kazi uendane na mabadiliko ya kisayansi pamoja kidigitali.

Mwisho Tanzania tunayoitaka ni ile yenye macho ya kuona kizazi cha tatu na cha nne kutoka hivi sasa,inayojali mustakabali wa vizazi na vizazi vya Tanzania ya baadae
0755173096/0655506609
promisegeofre03@gmail.co
 
Upvote 2
Back
Top Bottom