Tanzania tuongeze wigo wa Biashara na Congo DRC

Tanzania tuongeze wigo wa Biashara na Congo DRC

N'yadikwa

JF-Expert Member
Joined
Aug 10, 2014
Posts
7,427
Reaction score
10,905
Katika gazeti la The Citizen la leo Agosti 24,2020 habari iliyopo ukurasa wa mbele inasema "Nchi za Afrika Mashariki zinapoteza fursa ya biashara na Congo DRC inayofikia Dola za Marekani Bilioni 10.

Hii ni hasara kubwa kwa Tanzania (Sitaki nizisemee nchi nyingine za E.A).
Congo-Prof.jpg

Awali ifahamike kwamba Idadi ya watu wote wa Congo ni nusu ya idadi ya watu wote wa nchi za Afrika Mashariki.

Ni muhimu Tanzania kuongeza mauzo ya bidhaa na huduma huko Congo kwa kuzingatia kwamba hadi hizi sasa nchi hiyo kubwa sana Kusini mwa jangwa la Sahara hivi sasa bidhaa zake nyingi ambazo ni consumer goods inazipata kutoka China na Afrika Kusini huku katika nchi za Afrika Mashariki Rwanda ikiongoza kupeleka bidhaa huko ikifuatiwa na Uganda.

DRC hivi sasa bidhaa zake nyingi inaagiza China (31.2%), Afrika Kusini (15.8), Zambia (13%), Ubelgiji (5.4) na India (5.3%).

Congo DRC ina customer base ya watumiaji milioni 81 na SISI Tanzania tunafaa kuwa kinara wa biashara kwenye Taifa hili badala ya kufocus soko la nje zaidi. Tayari tuna viwanda vikubwa kabisa katika ukanda huu vikiwemo vya Saruji,Marumaru,Juisi,na hiki cha Sukari kinachojengwa plus vilivyopo, tunazalisha bidhaa za chakula za kutosha na nadhani ni wakati sasa tuliangalie soko hili kama eneo muhimu kistratejia kwa ajili ya mustakabali mwema wa nchi yetu.

Serikali mpya mtakaoingia hiyo keshokutwa October tafadhali washawishini wawekezaji wetu watanue mbawa huko na muweke mazingira ya biashara huko ili tuweze ku-tap hii market opportunity. INAUMA kuona nchi za mbali zinaongoza kuuza tena bidhaa za kawaida ambazo tunazo in excess kwa hawa jirani zetu. Tuachane na hawa wakenya wanatuchelewesha na kutuletea figisu figisu kwenye biashara. Hata misosi tuuze DRC.

Viva Tanzania Vivaaa!!!

Soon tutakuwa wababe wa uchumi kwenye Ukanda huu tukitia bidii.
Boulevard_du_30_juin_Kinshasa_Democratic_Republic_of_the_Congo.jpg
 
Ni kweli mkuu. Ni muda wa kuhoji serikali yetu kutuwezesha kimitaji.
 
Back
Top Bottom