Nilishawahi kuwaza hili ,nikajiuliza hv hata wale viongozi wa dini wanaokaa jirani na rais hawalioni hili japo kumshauri rais kupitia mifano ya kitabu Cha Yusuf na pharaoh!!?
Mafuta yameshuka Sana, Ni wakati sahihi wa kutengeneza reserve kubwa ya mafuta km nchi nyingine zenye upeo,
Kwa Hali ilivyo Sasa uchumi wa dunia unatikisika,japo Africa Corona haijaathiri Sana ila nchi wanachama wa misaada zimeathirika kwa kiasi kikubwa hvyo huko mbeleni tutegemee na ss kuathirika,nadhani ingekuwa vema kwa serikali kuwa na reserve ya kutosha ya madini amabayo hapa kwetu yapo kwa wingi...
Tuna dawa yetu ya Corona iliyotengenezwa na nimr,nadhani hii tungeitangaza vizuri tungeuza Sana sio tu Africa Bali hata Europe maana kutokana na historia yetu kuhusu Corona(hakuna lockdown,hakuna hospital iliyojaa wagonjwa wa Corona)
Nilishaangaa msimu wa mavuno sikuona tamko lolote kwenye wizara husika kuhusu kuweka reserve ya kutosha ya chakula,ndo kwanza wakulima walikuwa wanalalamika mazao yamekosa wateja,mahindi yameporomoka bei
Tumeona baadhi za nchi zilivyojikomboa kiuchumi kwa faida za Vita labda kuuza silaha, ujuzi huku wakinufaika kwa Mali asili za nchi husika Kama malipo
Ni wakati na ss kupanga mipango itakayotunufahisha na Corona