Tanzania vs Algeria (Septemba 14, 2015): Mechi ya kufuzu Kombe la Dunia Urusi - 2018

Status
Not open for further replies.

Watu8

Platinum Member
Joined
Feb 19, 2010
Posts
73,773
Reaction score
102,126


Hii ni mechi ya kwanza ya mzunguko wa pili kufuzu kuelekea Kombe la Dunia 2018.

Ni mechi muhimu kwa timu ya taifa ya Tanzania maana itakuwa nyumbani uwanja mkuu wa Taifa.

Katika michezo mitano ya mwisho timu ya Tanzania imeshinda mchezo mmoja pekee, huku ikitoka sare michezo miwili na kufungwa miwili. Algeria wao katika michezo mitano ya mwisho wamepoteza mchezo mmoja tu na kushinda mingine minne iliyobakia.

Hadi sasa Tanzania na Algeria zimeshakutana mara 7, huku mara 3 Algeria ikishinda, mara 1 Tanzania ikishinda na mara 3 ikiwa ni sare.

Kupitia uzi huu tuungane pamoja kushuhudia kile kitakachojiri siku ya mchezo.

Kikosi TZ: Ally Mustapha, Shomari Kapombe, Mwinyi Mngwali, Kevin Yondani, Nadir Haroub, Himidi Mao, Mudathir Yahya, Elias Maguli, Farid Musa, Mbwana Samatta, Thomas Ulimwengu

Waamuzi: Keita Mahamadou, Diarra Bala, Niare Drissa Kamory

TV Listing: ZBC 2, TBC1, Bein Sports 1HD(Bein US)

Live Stream: Watch Live Tanzania vs Algeria


Mungu Ibariki Tanzania
===============
Timu zimeshaingia uwanjani na kuimba wimbo wa Taifa, zinapasha kila mtu kwenye goli lake kusubiri muda rasmi wa shirikisho la Afrika kuanza mpira.

00' Refa kapuliza kipenga kuashiria mwanzo wa mchezo
02' Taifa star wanakosa goli la kwanza baada ya kushindwa kulenga japo walifanikiwa kuipita ngome ya Algeria
02' Taifa stars wanajitahidi kuingia kwenye eneo la hatari kwa pasi nzuri lakini wanashindwa kumiliki mpira
05' Mchezaji wa Algeria yuko chini na inapigwa faulo ndogo kuelekea Taifa Stars
07' Algeria wanafanikiwa kupata mpira wa kwanza wa kona ambao haukuzaa matunda
08' Baada ya mpira wa kona, Ulimwengu anafanikiwa kuunasa mpira na kukimbia nao hadi langoni mwa Algeria, lakini anapiga juuu
21' Samataaaa, amepiga shuti kali na mpira unagonga mwamba, stars wanakosa goli la kuongoza, matokeo 0-0
32' Stars wanakosa goli jingine baada ya kufanikiwa kumpita mlinda mlango lakini beki anafanikiwa kuuwahi
34' Stars wanapata kona yao ya kwanza, Algeria wanatoa na kuwa kona pacha, hata hivyo zote hazijazaa matunda
35' Tanzania wanakosa goli jingine baada ya kucheza vizuri, sentimita chache pembeni ya goli.
38' Samata tena, alibaki yeye na kipa lakini mlinda mlango afanikiwa kuuzuia
42' :A S soccer:Goaaaaaaaaaaaaal, Taifa stars wanaongoza goli lililofungwa baada ya krosi nzuri kutoka winga na Maguli kupiga kichwa kilichoandikia Stars goli la kwanza, Taifa stars 1-0 Algeria
45+1' Kipenga kinapulizwa kuashiria mapumziko
45' Algeria wanafanya mabadiliko, refa anapuliza kipenga kuashiria mwanzo wa ngwe ya mwisho
48' Mpira wa adhabu kuelekea Stars baada ya mchezaji wa Algeria kupata goli hata hivyo Riad anapiga sentimita chache juu ya goli
54 :A S soccer:Goaaaaal, Samataa anaipatia Stars goli pili, Tanzania 2-0 Algeria
65 Mabadiliko Stars, Maguli anatoka na kuingia Ngassa, Ndemla pia anaingia kuchukua nafasi ya Mudathir Yahya.
68' Stars wanapata kona nyingine kuelekea Algeria, hata hivyo haijazaa matunda
70' :A S soccer:Algeria wanapata goli baada ya beki wa stars kudhani mchezaji wa Algeria alikuwa offside
74' :A S soccer:Algeria wanarudisha goli la pili, Stars 2-2 Algeria
90+3' Mpira umeisha, Matokeo Tanzania 2-2 Algeria

Mechi ya marudiano itakuwa nchini Algeria, Stars watahitaji ushindi au suluhu kuanzia magoli matatu ili waweze kufanikiwa, ushindi wowote wa Algeria au suluhu isiyo na magoli au ya goli moja itahitimisha safari ya Stars kuelekea Urusi 2018.



 
Last edited by a moderator:
...mechi kubwa na muhimu hii, Mungu jalia tushinde naamini furaha itaanza kurudi moyoni baada ya kuchakachuliwa oct 25,hata mimi nilikua na hamu yakuanzisha uzi, honger watu 8 umeniwahi!!
 
Tupandishe kwanza uelewa wa mashabiki wetu .Tujumuike kuishangilia stars kila la kheri.
 
Hivi kwanini kila leo sisi huanza nyumbani?

Loya kwa nijuavyo katika mechi za mtoano timu iliyo katika nafasi ya chini katika alama za viwango huanzia mechi yake nyumbani...

Mfano sisi tupo chini ya Algeria ktk mtiririko wa viwango hivyo mechi imeanzia kwetu...
 
Loya kwa nijuavyo katika mechi za mtoano timu iliyo katika nafasi ya chini katika alama za viwango huanzia mechi yake nyumbani...

Mfano sisi tupo chini ya Algeria ktk mtiririko wa viwango hivyo mechi imeanzia kwetu...
Hebu ni kumbushe kenya kama si Uganda wameanzia ugenini hivi walicheza na nani vile? Ni majuzi tuu ili nijaribu kupima unacho sema..
 
Hebu ni kumbushe kenya kama si Uganda wameanzia ugenini hivi walicheza na nani vile? Ni majuzi tuu ili nijaribu kupima unacho sema..

Loya tazama mechi za qualifications zilizochezwa leo na mataifa mengine...

Timu zote zilizoanza nyumbani zipo chini ya wapinzani wao kiviwango...

Kenya kacheza na Cape Verde akiwa Nairobi (Kenya ipo chini ya Cape Verde) na Uganda wamesafiri hadi Lome kucheza na Togo iliyo chini ya Uganda...
 

Attachments

  • 1447438584677.jpg
    9 KB · Views: 842
Sasa hapa nimekupata zaidi asante....! ...
 
Wewe ndio mchawi kuamini hayo unayo yanena! Mwenzio anasaidia kuweka hamasa na kuwakumbusha watu...!

Off topic
Hivi kwanini kila leo sisi huanza nyumbani?

Lakini mkuu mbona hiyo ni nzuri kwetu!?

Me naona kama tukianzia ugenini alafu tukappteza mchezo basi hata nyumbani tutapoteza morale.

Niheli tunaanza nyumbani hapa tukishinda (hata goli moja) basi kunauwezekano wakulazimisha sare ugenini.
 
Lakini mkuu mbona hiyo ni nzuri kwetu!?

Me naona kama tukianzia ugenini alafu tukappteza mchezo basi hata nyumbani tutapoteza morale.

Niheli tunaanza nyumbani hapa tukishinda (hata goli moja) basi kunauwezekano wakulazimisha sare ugenini.
Mkuu pia inategemea sana na aina za mechi...kwa mfano tungekuwa tunaanza kwa Algeria ingekuwa raha sana kwetu kuliko kwao maana pengine wangepaniki sana.....
 
Tuombe mungu kwa kuwa bunduki za algeria zote zimekuja, yacine brahimi na sofiane feghouli hawa jamaa ni nouma
 
Loya kwa nijuavyo katika mechi za mtoano timu iliyo katika nafasi ya chini katika alama za viwango huanzia mechi yake nyumbani...

Mfano sisi tupo chini ya Algeria ktk mtiririko wa viwango hivyo mechi imeanzia kwetu...

Kenya IPO chini kwa Cape Verde
 
Status
Not open for further replies.
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…