Tanzania wanafiki, kuendesha umelewa ni kama imeruhusiwa, Polisi wanaangalia tu

Tanzania wanafiki, kuendesha umelewa ni kama imeruhusiwa, Polisi wanaangalia tu

ubarinolutu

JF-Expert Member
Joined
Oct 22, 2012
Posts
2,424
Reaction score
4,954
Habari Wanajamvini,

Hivi sisi Watanzania na Jeshi la Polisi ni watu wanafki sana hasa kwahili suala la kuendesha umelewa. Jana nilienda na gari yangu Police Mess nikanywa Konyagi zangu mbili nikaondoka nikawasha gari yangu huyo, huku baadhi ya polisi wakinisalimia, na wengine niliwazungushia raundi.

Tanzania kuendesha umelewa ni kama imehalalishwa yani; watu wanaenda kunywea pombe polisi na wanaenda na magari na wanalewa hawakamatwi.

Ukienda katika mabaa asilimia 90 ya magari yamepakiwa nje watu wanalewa baadaye wanaendesha na wengine kupata ajali, halafu unaambiwa eti huruhusiwi kunywa halafu ukaendesha combo cha moto wakati hata mtoto wa la kwanza ukimtuma akakuoneshe mtu anayeendesha amelewa, anakuonesha.

Ukitembea weekend magari asilimia 70 yanayotembea kwanza saa tano usiku madereva huwa wamelewa na Police wapo tu, tena na hao ndiyo wanaongoza kwa kuendesha wamelewa.

Hii sheria ifutwe au IGP ajiuzulu kwa kushindwa kuzuia walevi kuendesha vyombo moto.
 
Back
Top Bottom