Tanzania: Watu 76 kati ya 100,000 hugundulika kuwa na saratani. 68% wamefariki 2021

Tanzania: Watu 76 kati ya 100,000 hugundulika kuwa na saratani. 68% wamefariki 2021

John Haramba

JF-Expert Member
Joined
Feb 4, 2022
Posts
365
Reaction score
1,374
Kwa takwimu za Shirika la Umoja wa Mataifa la Tafiti za Saratani (IARC) za 2018, zinaonyesha kuwa tatizo la saratani nchini Tanzania limekuwa likiongezeka siku hadi siku ambapo inakadiriwa kuwa katika kila watu100,000, watu 76 hugundulika kuwa na ugonjwa wa Saratani.

Kwa hiyo nchi yetu inakadiriwa kuwa na wagonjwa wapya wa Saratani 42,060 kwa mwaka na takribani wagonjwa 28,610 sawa na asilimia 68 hufariki kutokana na ugonjwa huo.

Takwimu kutoka kwenye kanzi data (Population based Cancer Registry) zilizo anzishwa kwa Kanda, zinaonesha kwamba wagonjwa wapya 14,136 walifikiwa na huduma ambayo ni sawa na asilimia 33 ya makadirio ya wagonjwa wapya wote kwa mwaka 2021 ikiwa niongezeko la asilimia tano ukilinganisha na takwimu za Mwaka 2020 ambapo jumla ya wagonjwa wapya 12,096 (28%) walionwa.
 
Back
Top Bottom