SoC02 Tanzania ya dhahabu

SoC02 Tanzania ya dhahabu

Stories of Change - 2022 Competition

Jetway

New Member
Joined
Sep 10, 2022
Posts
2
Reaction score
1
vita vimepigwa kwa mabomu na siraha nzito ili kujenga ngome na kasili lenye kuwafanya watumwa na watwana kuishi katika hali ya usawa, pia mapambano hayo yamechochea umoja na mshikamano katika kujenga jumba lenye kutoa makazi kwa vizazi vijavyo na kuhakikisha afya, kwa hakika walimwaga jasho na damu kujenga mnara ambao utasimama ili kuleta usawa, umoja, maendeleo na hata kuhakikisha maendeleo katika falme.

Kwa umoja huo ulipelekea ushindi mkubwa mno kwa king'oa miti mikubwa eneo la kujenga jumba hilo la kifalme na kufanikiwa kusimamisha minara kama ile ya baberi kwasababu ya umoja, mshikamano katika kufikia malengo kwa kupinga unyonyaji, je kuona minara iliyojengwa na mashujaa ilikua ndio dhumuni la kujenga jumba au kasri la kifalme? je kumwaga jasho na damu wakati wa kung'oa miti mikubwa ndio lilikua lengo kuu?

Maswali haya yanagonga na kuumiza vichwa sana kizazi cha nuru kwani ukombozi ulitukia kwa kukata miti mikubwa na kusahau kung'oa visiki ndani ya falme, kwa hakika vita vya kujenga falme hiyo ilipelekea wahenga wengi kujisisi ni mashujaa na kusahau kwamba walitumia nguvu zao bure na kuhadhiliwa kiakili hadi ikapelekea kuhaaribu kizazi cha badae, kwa kuwajengea hofu na mashaka pia wakawaaminisha kuwa wako huru kutumia nguvu zao ya mkini wametawaliwa kwa mara ya pili kiakili, yote haya yalitokana na nini?

Tazama baadi ya visiki vilikua vikilinda na kutumikia miti mikubwa ndani ya msitu vikasahau kwamba wao ni watu wa nyumbani, hivyo ndivyo vinavyosababisha hadi nyakati za kukimbilia maendeleo nchi kujikwaa na kupata pancha na safari kulega lega, je chanzo cha uchumi wa nchi ya kifalme pamoja na wananchi wake kuwa duni ni visiki?

Tazama nchi kama China ilipata msaada kutoka kwenye hii nchi ya kifalme na hadi sasa vitabu vimeandika tu na kubaki kwenye historia kwa nchi ya kifalme kujisifu kwama walikua sawa kipindi cha historia lakini hawataki kujiuliza vitu vilivuvyowatenganisha kutoka kwenye usawa huo kweli kwenye miti hakuna ujenzi pia nguvu nyingi huzeesha lakini mjukuu wangu penda sana kutumia akili nyingi ili uishi maisha mazuri sana bila kuzeeka kwani visiki vilitumia akili nyingi sana ili kujaza matumbo yao wenyewe wakasahau kujenga ufalme kwa faida ya kizazi kinachokuja, je walishindwa kuitumia china kama kazi radi, au kuchukua mbinu na mwiongozo waliotumia katika kujenga ufalme walakini wanajijali wenyewe tu pamoja na kizazi chao.

Kwa hakika kungoa magugu na visiki sio kwamba haiwezekani ila ni hofu iliyojengwa ndani ya watu na wananchi wa kifalme, Kwasababu wanatumia pesa za wananchi bila kujali chanzo ni jasho na damu na kuachilia wanyama wakali wanaokuja kulalua ufalme tazama mnyama kama escrow, Richmond, na IPTL, kwa hakika wanyama kama hawa mjukuu wangu ndio wanaadhili nguvu za wazee wetu wa zamani na mashujaa wetu, hii yote ni kwa sababu ya uongozi mbovu wenye visiki vingi sana vyenye kuoneana aibu katika kutubu aibu zao na kula pesa za wananchi na kusema ni pesa ya mboga tu kwao na kusahau kwamba kufika kwao juu ni kwa sababu ya wananchi wa ufalme pamoja na watu wa kifalme. kwa hakika kama uongozi ukiendelea kuwa lege wananchi wataendelea kumwaga machozi kama maji, yamkini kunabaadhi ya viongozi wapo wenyenia ya kukuza uchumi wa wananchi ingawa kunabaadhi ya visiki vipo vinawaathiri hao viongozi wazuri wenyenia nzuri na kizazi kipya kwa hakika kunahitajika mapinduzi katika uongozi wa jumba la kifalme ili nasisi tujenge malezi boro katika nyanja za maendeleo, je kiongozi mzuri moja anaweza kujenga nchi mwenywe?

Rahasha kwa hakika mapinduzi ya uongozi yanataweza kujenga ufalme mpya kama mashujaa walivyofanya mapinduzi ya kung'oa msitu mkubwa sisi inatupasa tupambane kung'oa visiki na magugu ili kujenga kizazi kipya.

kwa hakika ungozi wa mapinduzi unahitaji kujenga teknolojia ya ufalme kwani falme inahitajika kujitegemea yenyewe sio kutegemea nchi nyingine, hii ndio tabia za falme lazima ufalme uwe na uchumi wake, technology yake, huduma bora za madawa na mitaara yake bora ya elimu je elimu inayotolewa na viongozi wa falme ya visiki iko vipi?

Kwa hakikika serikaili ya kifalme inamali nyingi mno hata kusomesha wanafunzi wa falme nzima kuanzia shule za msingi hadi elimu ya juu, lakini uongozi huu unadhani kumpa elimu kijana ni bora rahasha hili nilitamkwa na mbunge na kushauri serikali ya kifalme kwa kusema kama serikali inauwezo wa kusomesha wanafunzi hata nchi nzima bila uchumi kuteteleka mheshimiwa mfalme kwanini hawa vijana wanaohitimu elimu ya juu tusiwapatie mtaji pale tu wanapohitimu wakiwa katika kundi hata la watu watano wataano au hata mmoja mmoja Kwasababu tumewapatia mkopo tukijua kabisa maisha yao ni ya chini.

Kwa hakika mbunge alikua mwelevu mno kwani alileta hoja ya msingi ambayo ingekuza uchumi wa kifalme si kwawasomi tu ila hata kwa watu wa hali ya chini tazama kama wahitimu wakitendewa haya itasaidia sana kupunguza ukosefu wa ajira ndani ya jumba la kifalme pia wataanzisha biashara na makampuni ambayo yataajiri wasomi na wasio wasomi hii itapelekea kubadilisha teknolojia ya kifalme kwani vijana hao wamehitimu katika nyanja mbaalimbali na wanaujuzi wa kutosha, kuliko kuwaacha vijana hawa kurudi mtaani bila muelekeo wowote wakiwa wanakumbwa na tatizo la kukosa ajira kwa hakika maendeleo huletwa na vijana kwasababu vijana ni nguvu ya taifa kuliko kuwaacha vijana kutumia ujuzi wao katika wizi tazama vijana wengi wanaosomea masuala ya kimtandao wanatishia jamii yetu kwa kukosa kazi au ajira.

Tazama nchi nyingi zilitumoa mbinu za kuinua na kuwashika mkono watu wao wenyeujuzi na wenye elimu ili kujenga teknolojia yao hususani nchi kama vile china pia viongozi wazuri wanapasa kujenga miradi muhimu yenye kuimalisha ufalme tuitazaame India ni moja ya nchi iliojiendeleza sana katika sekta ya afya na kutambulika duniani kwanini nchi ya bendera ya rangi nne ishindwe.

Tazama kunamiradi muhimu sana ilianzishwa na kiongozi mzuri lakini alipoitwa hayati nayo pia ikapunguza mwendo ila yote haya ni kuendekeza visiki kwani hutoa maoni mabaya na pia ni vingi katika ufalme hivyo ningumu sana mimea kustawi ndani ya magugu na visiki vinavyochipua na dawa ya yote ni kung'oa visiki vyote sio kukata machipukizi kwani lashalasha ikishuka vitamea tena, kwa hakika vijana wakishikwa mkono lazima nchi yetu itakua na miundombinu itabadilika na hata uchumi wa mtu mmoja moja utakua ila yote inakua ngumu kwasababu ya baadhi ya visiki vinavyojali matumbo yao na kusahau jasho na damu za mashujaa.

Sasa niwakati wa kubadilika wananchi wa kifalme wanatakiwa wafumbue macho hata katika jambo la kuteuwa wawakilishi bora kwani tunahitaji viongozi wanaokumbuka jasho na damu za mashujaa sio kufanya sherehe kubwa na kula vyakula vizuri bila maumivu
 
Upvote 2
Back
Top Bottom