SoC01 Tanzania ya Karne ya 21: Mawanda mapana ya Kifikra

SoC01 Tanzania ya Karne ya 21: Mawanda mapana ya Kifikra

Stories of Change - 2021 Competition

FREDRICK VENANCE

New Member
Joined
Sep 22, 2014
Posts
3
Reaction score
3
Yapata miongo mingi tanguTanzania ilipojipatia uhuru wake kutoka kwa Mwingereza. Imepita mihula mingi ya uongozi, tangu Hayati Baba wa Taifa, Mwalimu Julius K. Nyerere hadi kufikia utawala wa sasa wa Mh. Rais Samia Suluhu Hassan. Awamu ambayo sote tunajivunia kuwa na Tanzania yenye "Uchumi wa Kati" uliofikiwa katika awamu ya tano ya uongozi wa Hayati, Dkt. John Pombe Magufuli.

Ili kuweza kudumisha uchumi huo wa kati, nyanja mbalimbali za kiuchumi, kisiasa, kijamii, kiutamaduni na kadhalika, zinapaswa kutiliwa mkazo.
Hii itasaidia kuendeleza, kuimarisha na kukuza na kwa upana pale ambapo tumefikia. Ili kufikia na kutimiza malengo hayo, fikra yakinifu zinapaswa kuwekwa katika utendaji zaidi na si maneno kwa kuzingatia nyanja zifuatazo:

Nyanja ya Kiuchumi. Ili taifa lolote lipate kiendelea linapaswa kuwa na uchumi wenye mwendelezo uliobora na unaokua. Hii inamaana kuwa, kuwapo kwa njia nzuri za kiuchumi, zikiwemo ulipaji wa kodi zinazotokana na biashara, upatikanaji kwa wakati wa vibali vya kuendesha biashara, uboreshwaji wa miundombinu inayorahisisha shughuli za kibiashara, kutaweza kufufua matumaini ya kuweza kuwa na uchumi imara na utakaozidi kukua kwa kasi zaidi.

Aidha, ili uchumi uweze kukua na kuimarika, hakuna shaka kuwa ni vyema serikali, wadau pamoja na wananchi kwa ujumla kutilia mkazo suala zima la afya ya jamii na afya ya taifa kwa ujumla. Kila mmoja anapaswa kupambana na kushiriki kikamilifu katika mikakati, malengo na mipango ya kuboresha huduma za afya; kujitolea katika shughuli mbalimbali za ujenzi na usafi wa mazingira na kadhalika. Isitishe, serikali inapaswa kuwekeza nguvu zaidi katika sekta ya afya ili kuufanya uchumi wake kuwa wenye afya.

Sambamba na hayo, suala la Utawala bora na uwajibikaji ni wa kutiliwa shime na kupigiwa kelele kwa kina. Utawala huanzia katika ngazi ya familia na kisha kuifikia ngazi ya nchi. Hivyo, basi ikiwa suala la utawala ulio bora utakuwa ni ule usiokidhi matakwa na matarajio ya wale wanaotawaliwa katika jamii; ikiwa ni sambamba na kutokuwajibika kwa dhati kwa viongozi pamoja na wananchi kwa ujumla; basi ni dhahiri kuwa kamba ya umoja wenye tija katika kuuvuta uchumi imara itakatika tu ngali hatujafikia ngambo.

Kilimo ambacho wengi tumekuwa tukijikaririshwa kuwa ni, "Uti wa mgongo wa taifa", nacho hakiwezi kupuuzwa. Ingawa kwa kizazi cha sasa cha sayansi na teknolojia, kilimo ni vyema kikaendeshwa kwa kuzingatia njia bora za kisasa ili kupata mazao na faida bora zitokanazo na kilimo cha kisasa cha kisayans kinachotumia teknolojia ya hali ya juu. Twapaswa kuwekeza nguvu katika kuondokana na dhana ya kulima kwa kutumia jembe la mkono na kufikria mbali zaidi juu ya matrekta na pembejeo nyingine bora za kisasa.

Ili hayo yote yaweze kufanyika kwa ufanisi, uwazi, weledi na kwa harakua, ni dhahiri shairi kuwa, nchi inapaswa kuwa na demokrasia ya kweli. Demokrasi ambayo itampatia mwanachi wa kawaida uwanja mpana wa kushiriki katika kutoa, kuchangia, kufuatalia na kutilia mkazo maoni, mapendekezo na maamuzi ambayo yanafikiwa kwa pamoja ili kutekelezwa pasi na shaka na mamlaka zinazohusika. Uchaguzi wa huru na haki, kuwa na katiba inayomjali na kumlenga kila mmoja, bila kujali matabaka ni mambo ya kupigiwa upatu.

Haki za binadamu ni sehemu muhimu sana katika kuyafanya maendeleo ya nchi kupiga hatua. Kila mtu ana haki yakushikiriki katika shughuli za maendeleo. Ukiachilia mbali suala zima la kuunga mkono baadhi ya haki za kibinadamu zinazokinzana na utamadumi na maadili ya jamii. Kuwepo kwa uhuru unaojali haki za kila mtu, ikiwa ni pamoja na kupata elimu kwa kila rika, kuishi kwa amani bila kusumbuliwa na kadhia za aina yoyote ile, kutawafanya wananchi kushiriki katika maendeleo ya taifa bila kujali jinsi (sex) au jinsia (gender) walizonazo.

Mwisho lakini si kwa umuhimu, ni kuwa, kila jambo linalopangwa ili kufanyika katika mtazamo chanya, ni vema likafanyiwa utafiti wa kina kabla ya kuwekwa katika utekelezaji. Hii itasaidia zaidi katika kufanikisha malengo yaliyowekwa kwa urahisi na haraka sana na si ubabaishaji tu.

Tanzania ya uchumi wa kati inapaswa kuwa na watu wenye mawazo, fikra, mitazamo na mawanda mapana ya kiweledi katika kuhakikisha nchi nzima inapiga hatua kimaendeleo na si kujikita katika "siasa" ama pojoro nyingi. Twapaswa kukumbuka ule msemo wa Kimombo usemao " Practise Make Pafect"( yaani, Uthubutu wa kutenda, huleta usahihi wa wa matokeo). Hivyo, kila mmoja wetu atimize wajibu wake kama mwananchi. Hii ni pamoja na kuweka uzalendo mbele, heshima, kujituma, utii na mipango madhubuti katika kuleta mabadiliko chanya.
 
Upvote 6
Tatizo kubwa katika sekta ya kilimo ni uhakika wa masoko ya bidhaa za shambani. Barabara pia ni changamoto kubwa, mazao kama nyanya ambayo hayakawii kuharibika huleta hasara sana yanapochelewa kumfikia mlaji.
 
Back
Top Bottom