SoC04 Tanzania ya miaka 5 mpaka 25 ijikite katika matazamio haya

SoC04 Tanzania ya miaka 5 mpaka 25 ijikite katika matazamio haya

Tanzania Tuitakayo competition threads

winyrida

New Member
Joined
Jun 25, 2024
Posts
1
Reaction score
1
Tanzania ni Moja ya nchi zilizo na maendeleo endelevu katika sekta mbalimbali,kulingana na takwimu mbalimbali zikionesha hali halisi ya Tanzania tangu mwaka 2021 mpaka matazamio ya mwaka 2024/25,licha ya kukumbana na matatizo mbalimbali kama vita ya Urusi na Ukraine, janga la UVIKO-19 na mabadiliko ya tabia ya nchi.Kwa uongozi uliokuwepo ulipambana na kukabiliana na changamoto hizo Kwa kuunda mikakati ya kutatua tatizo la Vita,utoaji ruzuku ya mbolea na mafuta ya petroli. Ambapo ilipelekea uchumi kukua na kuongezeka Kwa asilimia 4.7 Kwa mwaka 2022,na matarajio ya asilimia 5.2 Kwa mwaka 2023 na asilimia 5.8 Kwa mwaka 2024. Yote haya ni matokeo ya ukuaji katika baadhi ya sekta nchini.

Bali kulingana na kupanda Kwa Bei, kupungua kwa mapato (Kodi) na deni la serikali na vita vya Ukraine,hivi ndivyo vitakwamisha malengo ya maendeleo ya uchumi na Tanzania ya miaka 5 -25 mbele kuendelea kuwa chini au kushika zaidi. Hivyo basi serikali inatakiwa weka misingi mikakati ifikapo 2030 Tanzania isiwe tegemezi katika nyanja zote. Zifuatazo ni baadhi ya sekta kwamishi katika kufikia maendeleo ya Tanzania Kwa miaka 5-25 mbele.

Sekta ya uwekezaji. Kulingana na kuwepo Kwa Kasi kubwa ya uwekezaji nchi , Tanzania inategemea kupata maendeleo rukuki bali tatizo la kuwepo Kwa deni la Nchi nje na ndani itakua kikwazo katika kufikia malengo, kulingana na kuwa nchi itahitaji wekeza pia katika sekta hizo kama kilimo ,madini ,utalii na biashara. Na kuwa kikwazo Cha maendeleo.

Sekta ya miradi mbalimbali. Pia nchi ina miradi tofautitofauti ambayo mpaka Sasa imesimama kulingana na kuwepo Kwa Mapato madogo ya kuimarisha, mchakato endelevu hivyo basi tatizo la ukopaji na mabadiliko ya tabia ya nchi yamepelekea Tanzania kubaki katika maendeleo yasio na mabadiliko. Hivyo basi Ili kuwezesha maendeleo ifuatayo ni baadhi ya sekta zinazotakiwa imarishwa Ili kupelekea maendeleo endelevu ya ndani na nje.

Sekta ya usafirishaji na uchukuzi. Pia Moja ya changamoto katika maendeleo ni kukosekana Kwa michakato ya uwezeshaji katika kuimarisha na kufanikisha usafirishaji na uchukuzi. Hivyo kuwepo Kwa Mapato wezeshi na miundombinu rafiki na rasilimali watu itasaidia kufanikisha sekta hii. Hivyo serikali inapaswa kupunguza matumizi ya Pato katika sekta zisizo na maendeleo ya lazima na mikopo isiyo na tija Ili kuweza kuwekeza katika sekta hii Kwa Tanzania ya badae.

Sekta ya viwanda. Serikali inatakiwa kuwapa vipaumbele wavumbuzi ndani ya nchi Ili kupunguza utegemezi wa wataalamu kutoka nje pia, matumizi ya Pato kubwa katika kuwekeza vifaa ambavyo vinaweza tengenezwa ndani ya nchi,pia ujenzi wa viwanda tofauti Ili kuongeza uwekezaji na Pato la serikali na tatizo la Bei kupanda kama viwanda vya sukari na bidhaa za viwandani,Ili kuwapo na uwiano wa Mapato ya serikali na uzalishaji,Kwa ajili ya maendeleo endelevu.

Sekta ya Utalii. Serikali inapaswa kuimarisha miundombinu wezeshi katika sekta ya utalii Ili kutia hamasa Kwa wageni wanaokuja nchi kutaliina kuona thamani ya Tanzania,kwani kupitia utalii wa ndani utaimarisha ongezeko la fedha za kigeni na uwekezaji katika sekta hii,pia kupitia kauli mbili tofauti tofauti Kwa baadhi ya jamii zinazopatikana karibu na vivutio vya utalii vyapaswa kupewa elimu ya utunzaji mazingira na kulinda rasilimali watu na wanyama wetu,Ili kuongeza tija ya utalii. Na kufikia maendeleo ya Tanzania ya badae.

Sekta ya Madini. Kulingana na ongezeko la uwekezaji nchini, serikali inapaswa kuimarisha miundombinu na mikataba na maeneo wezeshi Kwa wawekezaji Ili kukuza Pato la serikali na kupunguza idadi ya wasio kuwa na ajila.Pia kuwapo Kwa maeneo wezeshi katika sekta hii itakuza wigo katika Pato la fedha za kigeni na ujaribu baina ya Kanda tofauti tofauti na soko la madini licha ya kuwapo Kwa vita ya Urusi na Ukraine.

Sekta ya Mabadiliko ya tabia ya nchi yamepelekea janga la njaa na kupanda Kwa Bei katika baadhi ya maeneo na Kwa nchi Kwa ujumla katika mazao kama mahindi, ngano na kushuka Kwa baadhi ya masoko duniani kama ya tumbaku na pamba,hivyo kupitia mikakati na sera mbalimbali serikali itakazo weka kudhibiti utumiaji mbaya wa mazao na uimatishaji wa kuhifadhi maghala ya chakula, itasaidia katika kuongeza Pato la serikali na kupunguza mikopo isiyo ya lazima,pia kuepukana na madhara ya majanga na mabadiliko ya tabia ya nchi. Hivyo kuipa thamani Tanzania ya miaka 5-25 badae.

Sekta ya Nishati. Tatizo la Bei ya mafuta kupanda Kwa nchi,ni moja ya kwamisho la maendeleo hivyo serikali kupitia sekta hii inapaswa kuwekeza katika matumizi ya nishati mbadala na endelevu Ili kuepukana na kupanda Kwa Bei na kupunguza matumizi ya Pato na fedha za kigeni katika ununuzi wa mafuta na kuendelea kutunza mazingira Kwa kukubaliana na miradi mbalimbali kama Matumizi ya Nishati safi ya kupikia Kwa Tanzania ya badae.

Sekta ya Mapato, Kulingana na kuwepo Kwa takwimu mbovu katika ukusanyaji Kodi ,hivyo serikali inatakiwa imarisha sekta hii katika masuala ya TEHAMA matumizi ya vifaa vya elektroniki katika ukusanyaji Kodi ,ambayo itasaidia wananchi na serikali Kwa ujumla katika kuimarisha maendeleo ya tarafa, mikoa na vijiji mbalimbali.

Sekta ya Habari na michezo.Katika sekta hii serikali inapaswa kupunguza utoaji wa pesa zisizo za lazima( kama pesa Kwa magori yanayofungwa na wachezaji) na badala yake kuwekeza ili kupata faida kupitia soka la michezo, na katika habari kulingana na takwimu mbalimbali zinazoonesha kuwepo Kwa uchache wa waajiriwa Kwa waandishi wa habari na walio ndani ya mkataba, vitisho na uhuru hafifu,pia ubaguzi katika fursa na kipaumbele katika jinsia ya kike. Hivyo Kwa maendeleo ya miaka 5-25 serikali inapaswa kuweka misingi sahihi katika nyanja ya Habari kwani ndio mhimili wa nne katika serikali.

Sekta ya Benki. Kuwapo kwa tatizo la upungufu wa fedha za kigeni na deni la Nchi ndani na nje , serikali inapaswa kuimarisha mikakati katika sekta za kibenki na utumiaji holela wa fedha za kigeni,ambapo kupitia mikakati na sera mbalimbali itasaidia kutoa taarifa za wakopaji na mikopo wezeshi, hivyo itasaidia serikali kuweka uwekezaji katika sekta zenye tija na kuepukana na mikopo isiyo ya lazima. Kwa Tanzania ya miaka 5-25 mbeleni.

Hivyo, kupitia matazamio haya tunategemea kuwa na Tanzania yenye maendeleo endelevu katika sekta zote na changamoto, zote.

TANZANIA YA MIAKA 5-25, HATURUDI NYUMA.

Imeandaliwa na,
Winifrida P John
0624546463
0614203026
 
Upvote 1
Back
Top Bottom