TANZANIA TUNAYOITAKA KWA MIAKA 5 MPAKA 25 IJAYO.
Tanzania , nchi iliyopata uhuru wake mwaka 1961 chini ya utawala wa waingereza, ikiwa chini ya Rais wa kwanza wa jamhuri ya Tanganyika Mwl Julius kambarage Nyerere.
Kama mwananchi wa kawaida, nimeona mambo mengi ambayo yamkini ningekua kiongozi nadhani ningeyafanyia kazi kwa manufaa ya watanzania.
Kwa Rasilimali zilizopo nchini, Tanzania ijayo hata kwa miaka mitano au kumi ijayo inawezekana dhahiri kufanya mambo makubwa yenye manufaa kwa wananchi na nchi kwa ujumla.
Mfano, Rais na watendaji wake wakiweka mikakati kusimamia mbuga zote za wanyama na mapato ya watalii yakawekewa mfuko maalumu kwamba hizo pesa zinazopatikana zijenge barabara tu...ni jambo linalowezekana vizuri tu.
Mkakati mwingine unaoweza kutumika ni matumizi ya mapato ya bandari zote nchini. Pesa za bandari ziwe na mfuko maalumu na hizo pesa zitumike kujenga madarasa, kuajiri waalimu na wafanya kazi wa kada zingine, kujenga vituo vya watoto yatima na kuwawezesha walio na mazingira magumu.
Mkakati mwingine wa kuiwezesha Tanzania ijayo ni matumizi sahihi ya Tozo zinazotozwa na TRA. Mamlaka ya mapato Tanzania[ TRA] ina safari kubwa kuiendeleza Tanzania endapo tu itawekwa mikakati kwa ajili ya maendeleo ya wananchi . Mfano ushuru wa magari yanayoingizwa Tanzania ni mara mbili ya bei yake au hata na zaidi. Pesa ambayo inaweza kutumika kuendeleza miradi mbalimbali ambayo baadae ni msaada kwa nchi.
Pia mamlaka ya mapato inaweza kupanga njia rafiki ili wananchi wasiumizwe na hizi tozo.
Mfano waweke tozo rafiki kwenye vifaa vya ujenzi kwa miaka kadhaa ambapo kila mwanachi atakua na uwezo wa kujenga makazi yake ya kudumu.
Tanzania ijayo iwe na katiba mpya ambayo itawezesha uchaguzi uwe Huru na Haki..ili kupata viongozi wanaochaguliwa na wananchi, sio kama ilivyo kwa kipindi hiki ambacho wanapatikana viongozi wasio na weredi. Viongozi watakaopatikana watakua wanawajibika kwa wananchi ikiwa ni pamoja na kumuondolea mamlaka makubwa aliopewa Rais.
Vilevile katika kuijenga Tanzania mpya kwa miaka mitano au kumi ijayo Wateule wa Rais wapungue ikiwemo wakuu wa mikoa na wilaya awe mmoja tu kupunguza matumizi ya serikali.
Tanzania ijayo inaweza ikaendelea kutokana na uwepo wa Shirika la meme Tanzania [ Tanesco]
Hapa najaribu kutafakari pesa zinazotozwa kwa watanzania wanaponunua huduma ya luku kila mwezi shilingi 1500. Pesa ambayo ikikusanywa kwa kila mwezi kwa miaka angalau mitano au kumi Tunajenga hospitali mpya na kuweza kuwalipa wataalamu wa afya katika vituo hivyo.
Tanzania ijayo ibadilishe mtaala wa elimu,. Elimu ya sasa imejikita kwenye nadharia , mwanafunzi hawezi kufanya chochote hata kujiajiri baada ya kuhitimu masomo ya sekondari au hata chuo kikuu.
Vijana wajifunze kwa vitendo, mfano kilimo, ufundi stadi katika fani mbalimbali kama umeme au ujenzi, shule iwe kama VETA.
Tanzania ijayo iwe na mtaala unaoelezea uhalisia , mfano baadhi ya nchi kama Afrika ya Kusini wanajifunza ufugaji wa kondoo, kwanini Tanzania pasiwe na somo la ufugaji mathalani kwa Jamii za wafugaji kama wamasai ili wafuge kisasa ?
Tanzania ijayo ipunguze baadhi ya masomo kwenye mtaala wa elimu ili wanafunzi wajifunze vichache vyenye tija. Mfao kuna somo linaitwa historia, mada inaitwa historia ya binadamu.
Wanaelezea kwamba binadamu alikuwa nyani, swali linakuja kwanini binadamu wa saivi habadiriki kuwa nyani? Kwa maendeleo ya baadae hii mada haina mantiki.
Tanzania kwa miaka mitano au kumi ijayo inaweza kuendelea endapo Taasisi ya kuzuia na kupambana na rushwa [ Takukuru] na maafisa wake wakaacha kupokea na kubambikizia watu rushwa. Hii itasaidia pesa zinazopotea kwa njia ya rushwa ziweze kutumika kwenye miradi mbalimbali mfano maji masafi.
Pesa nyingi zinapotea kwa mtindo wa rushwa lakini Taasisi husika inapambana na vitu vidogo
Kumbe pesa hizi zingetumika kuwapelekea wanachi maji hivyo Tanzania ingekua na maji kila kona pasipo wananchi kufuata maji zaidi ya kilomita 30 kufuata maji safi na salama au kuchota maji mtoni.
Tanzania ijayo kama itawezekana, misafara ya viongozi isiwe na Gharama kubwa kama kipindi hiki pesa ambazo zinatumika katika ziara mfano ziara ya Rais au makamu wake au waziri mkuu , pesa inajenga zaidi ya madarasa 20 au 30.
Hivyo bajeti ya misafara ikipunguzwa itasaidia kuibadirisha nchini yangu Tanzania.
Tanzania ijayo ifute mbio za mwenge, maana ni ufujaji wa pesa, Mimi kama mwananchi sioni haja ya mwenge wa uhuru kuzunguka kukagua miradi ambayo hata mkuu wa mkoa au kiongozi yeyote wa serikali anaweza kuzindua katika eneo husika.
Pia katika uzinduzi awepo mtaalam hasa wa suala husika, Mfano kama ni uzinduzi wa majengo basi awepo mtaalamu akague kuliko mwanasiasa akague huku hana utaalamu wowote wa jambo husika.
Sambamba na hili ,Tanzania ijayo kwa miaka mitano au kumi, serikali isitishe mikataba ya uchimbaji wa madini kwa nchi kubwa kama uingereza na marekani.
Madini yakichimbwa na nchini husika kutakua na faida kubwa sana na kwa nchi kama Tanzania Tajiri ya madini mbalimbali kama dhahabu na Tanzanite. Pato la Taifa litaongezeka na pesa zitatumika katika miradi mingi ya kimkakati.
Tanzania ijayo ningependa kuwe na sera moja ambayo kiongozi anapopata wasaha wa kuwaongoza wanachi aendane na sera aliyoikuta. Mfano Marekani wanaendelea sababu wana sera ambayo Rais anavyoingia madarakani anaitumikia lengo ikiwa ni kuwaletea wananchi maendeleo na si vinginevyo.
Mwisho kwa umuhimu,
Tanzania itaendelea endapo kutakuwa na mabadiliko ya utawala wa sheria hasa kama viongozi wataweza kuwajibishwa pale wanapoenda kinyume na matakwa ya wananchi waliowachagua.
Mungu ibariki Tanzania.

Upvote
6