Tanzania ya pili duniani kwa vivutio asilia vya utalii, tulikwama wapi?

Mama ameonyesha njia na wengine waendelee mfano Waziri wa itali lazima awe na mbinu mpya za kuongeza Watali karibu katika kila msimu

Vizuri wahusika hata waende kwenye facts finding mission kujifunza wenzetu wanafanyaje. Au kama hatina uwezo, ubunifu, tuwaajiri wenye huo uwezo.

Ukipita Dubai unashangaa Airport yao tu yao inaingiza pato kubwa kuliko Pato la Tanzania kwa mwaka, huduma zao ni first class halafu chapchap, miundombinu iliyosimama.

Sababu wanajua watu wao hawapendi hizo kazi na hawana nguvu kazi ya kutosha wameajiri watu wengi sana kutoka nje kuwafanyia kazi. Wakurugenzi na wakufunzi wengi ni wazungu.

Senior managers and top expert wengi ni wazungu, Pilots, wahudumu wa ndani wa ndege na uwanjani, wauza maduka, engineers, madereva, walinzi, cleaners wanatoka kote duniani hadi Tanzania.

Wao kama una uwezo wanakuajiri, haijalishi unatokea wapi. Wanaangalia matokeo.

Wenyewe wameweka systems matokeo yake wamepiga hatua kubwa sana, haraka sana na wanapata pesa nyingi sana.

Kuna vitu vya kujifunza.
 
Tanzania tuna ugonjwa wa kutanguliza wanasiasa na siasa kuliko wanataaluma na taaluma. Wanasiasa ni wala rushwa na 1 kuanzia wa kwanza na raia na 1 mpaka wa milioni55. Hayo yamezaa mifumo mibovu isiyotabirika. Ubovu wa katiba ukiwa ndio engine. Hatuna vipao mbele na kila rais anayeingia madarakani anaweka priorities zake na kupiga teke za mtangulizi wake. Kama mnataka utalii ukue wasikilizeni wadau husika, waacheni wakue muache kuwaua kwa kodi nyingi zisizo na tija mtafika malengo makubwa. Rai yangu.
 
wazo zuri sana, Nadhani wahusika watachukua hizi comments ili kulisaidia Taifa letu,

Mama ameonyesha njia na wengine waendelee mfano Waziri wa itali lazima awe na mbinu mpya za kuongeza Watali karibu katika kila msimu

Ukiangalia dubai mbinu zao za kujitangaza ni za hali ya juu sana. Wana majina yao kwenye viwanja na jersey za Arsenal, AcMilan, wanajitangaza kwenye TV stations nyingi za Ulaya, US, on google, billboards, kwenye magazeti, competitions ukishinda unaenda holiday bure.

Umuhimu wake unawafanya watake kujua, kujifunza na kutembelea zaidi kuhusu nchi husika na vivutio vyake.

Hata Kenya wametupita kwenye kujitangaza.

 

Uko sahihi, Katiba mpya ni kitu muhimu, lakini tatizo letu ni zaidi ya katiba.

Yapo mengi kubwa ni kukosa uzalendo wa kweli, kutaka kujifunza mambo mapya na kwenda na wakati, ubunifu, kuwa deadly serious na umakini wa hali ya juu kwa mambo muhimu.

Dubai, Qatar, ni nchi kifalme, kidikteta.

Lakini ukiangalia kwa umakini wanajali watu wao na kutumia resources zao vizuri. Utaalamu wasiokuwa nao, wanachukua nje.

Muhimu kwao nchi ipate kipato, kuwapatia watu wao huduma bora kama elimu, afya, usafiri, makazi, kazi, kipato cha uhakika.

Huo ndio uzalendo wa kweli, kuhakikisha kila rasilimali inawanufaisha wananchi wote, wananchi wanapata huduma zote muhimu na kutengeneza mazingira mazuri, rafiki ya utalii, biashara, uwekezaji, ajira kwa vitendo, sera wezeshi.

Sisi tungehamia Dubai na mentality yetu wenyewe wote wakahamia Tanzania na mentality yao, Tanzania imeendelea na uchumi mkubwa nakuajiri wote wanaotaka kazi na wengi tu kutoka nchi mbalimbali.

Mentality, ideas, vision, exposure, openmind, correct actions nia dhabiti, ni muhimu.
 
Andiko lako umesema Brazil asilimia 80 ya pato lao la utalii linatoka ndani , idadi ya watu Brazil ni 212,559,417. Sisi kama sisi tuko 60milion so trilion tano ni saizi yetu kabisa kabisa katika case study yako.
Katika utalii wa mali asili kuna hii dhana ya sustainable tourism hatuhitaji ku over use our resources to cope with a globe hype, ukiisha kuharibu vivutio asili ndio imetoka hio tutakua kama Kenya sasa ukienda kwa mbuga zao unaweza kukaa mwezi usione simba zaid ya nyumbu na ngiri tu maana wao wanapambana kweli kweli wakae kwa rank za dunia matokeo yake saivi hawako valid tena .
Tunatakiwa tu promote sana utalii wa utamaduni, michezo na bata tusihamasishe uharibifu wa mazingira kisa vipande vya fedha tutaishia kua na zoo tu kama jirani yetu
 
Wenzetu wana Utalii wa
Night Life.
Yaani usiku Beach zao zinamatukio kama.
Michezo mingi kama Beach Volleyball
Mziki
Michezo ya Casino
Nk

Huku kwetu saa mbili usiku watu wamelala hakuna pa kwenda.
Kufurahia maisha.
 
Umeandika kwa msisitizo sana. Asante

Sent from my VF-795 using JamiiForums mobile app
 
Wenzetu wana Utalii wa
Night Life.
Yaani usiku Beach zao zinamatukio kama.
Michezo mingi kama Beach Volleyball
Mziki
Michezo ya Casino
Nk

Huku kwetu saa mbili usiku watu wamelala hakuna pa kwenda.
Kufurahia maisha.



Hahaha hii kali Sana, Nimependa sana mawazo ya wachangiaji wa hii mada,

Kila mmoja atumie fursa aliyonayo kuutangaza Utali whether ni kwa mtu wa ndani au wanje
 
Tunaweza kupeleka huko watu kujifunza au kuajiri watu tayari wenye ujuzi.


That is it.

Hicho ndicho ninachosema, badala ya kuanza na Royal tour ingeanza hiyo hatua na baadaye ndipo ije Royal tour.
 
Hahaha hii kali Sana, Nimependa sana mawazo ya wachangiaji wa hii mada,

Kila mmoja atumie fursa aliyonayo kuutangaza Utali whether ni kwa mtu wa ndani au wanje
Watalii wakija toka kwao wanataka kupumzika hasa mida ya usiku.
Huku kwetu Tanzania pamoja na kuwa na vivutio vingi vya utalii tuna ukanda mzuri wa bahari kutokea Tanga hadi kusini Mtwara.
Wenzetu huko wanaweka kumbi za Ngumi au Mieleka.
Na michezo mingine ya kumwaga muda wa Usiku kwenye fukwe zao za bahari.
Jambo linalo wafanya Watalii waburudike Usiku mzima pamoja na kufamiana na Wakaka na Wadada wa Kiafrika.
Hiyo ndio inayoitwa.
"Night Life Tourism" inapendwa sana na Watalii.
Nchi za Far East kama Singapole, Malasia, Philippines, Indonesia, Mongolia. Zile zenye Bahari zinapokea watalii wengi sana kwa ajiri ya Night Life Activities peke yake.
Sasa huku kwetu Tanzania ikifika saa 6 ya usiku mji wote kimya, hakuna pa kuspend time. Kizazi cha sasa cha Watalii hakivutiwi sana na hii hali ya kulazimika kulala mapema.
 
Mtu kula kwenyewe ni shida atawaza vipi kwenda kuona nyumbu
Wacheni hii maneno kabisa
 
Mtu kula kwenyewe ni shida atawaza vipi kwenda kuona nyumbu
Wacheni hii maneno kabisa

..tunaweza kujiwekea malengo kwamba ifikapo 2030 nusu ya watalii wawe ni wazawa.

..maana yake ni kwamba itabidi tujenge mazingira ya kiuchumi yanayowezesha wananchi wetu wengi zaidi kuingia daraja la uchumi wa kati au wa juu.
 
That is it.

Hicho ndicho ninachosema, badala ya kuanza na Royal tour ingeanza hiyo hatua na baadaye ndipo ije Royal tour.


Hapana, Tunasema "Wache inyeshe tuone panapovuja,
 
That is it.

Hicho ndicho ninachosema, badala ya kuanza na Royal tour ingeanza hiyo hatua na baadaye ndipo ije Royal tour.


Hapana, Tunasema "Wache inyeshe tuone panapovuja,
 
Royal Tour Film huenda ikafanya maajbu, Kwanza imewafanya Watanzani ndani wamekuwa na awareness kuhusu Utali,

Mpaka hapo tayari 2-0
 
Wanasiasa wa Tanzania siwaamini kabisa.

Baada ya gas kugundulika huko kusini, Kikwete alituambia mitambo ya kufua umeme kwa kutumia gas ikikamilika umeme ungeshuka bei..mpaka leo tunasubiri.

Huyu mama naye ni wale wale tu.
Kwa kifupi usimwamini mwanasiasa hata akiwa mama ako.
 
Unajua mtanzania analipa shs ngapi kuingia national park na mtu asiye mtanzania analipa shs ngapi?

Ukijua Hilo huwezi beza jitihada za kujitangaza nje
 
Hapana, Tunasema "Wache inyeshe tuone panapovuja,


Watalii sio kama mvua ikishanyesha basi, wao ndio wateja wa huduma "customers) na sisi ni "customer careers" na tabia ya mteja ni kupeleka habari za huduma alizopata kwa wenzake, kimsingi mteja ndiye anayetangaza soko lako kuliko wewe mwenyewe unavyojitangaza, soko likiwa bovu andika maumivu na likiwa zuri utalamba dume, au unadhani waliosema mteja ni Mfalme ni wajinga?!--- jinsi Mfalme anapaswa anyenyekewe ndivyo hivyo hivyo mteja anapaswa ahudumiwe (hospitality).

Kuna hoteli moja ilikuwepo mjini Moro, hiyo hoteli ilikuwa inapendwa sana na Wamasai kwa ajili ya Pilau yenye nyama, ni mmasai mmoja tu siku moja alikula pilau-nyama katika hoteli hiyo na (huyo mmasai Moleli) aliporudi kwao Melela akawapasha habari wenzake juu ya hiyo pilau nyama, Ikawa kila wakija mjini basi huenda kwenye hiyo hoteli na kumuuliza muuzaji; "Yero ile chakula uliyompa Molel ile wa Melela ipo?? 😁 -- haikuwa shida kwa Muuzaji kutambua kwamba hao Wamasai walikuwa wanaulizia Pilau- nyama ambao wao waliita chakula ya Moleli, Watalii ni hivyo hivyo kama hao Wamasai.
 
Nakubaliana na hoja zako mkuu. Binafsi mimi ni kuhanga kwa namna moja au nyingine kama mtalii mzawa. Nimewahi kukosa Tour guide pahala kisa inaonekana mzawa hana “tip”

kuna hifadhi fulani napo nilienda, tour guide wamejiwekea utaratibu wa forcing pay kwa mtalii mara ya kwanza nilidhani ni bahati mbaya niliporudi mar ya 3 ndio nikajua ni organized issue.

nadhani ili kufikia nambari ya maajabu lazima tukubali kujifunza kwa walioshinda ila kwa uzingativu “hospitality” na “innovations “ ndizo engines.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…