Tanzania ya pili duniani kwa vivutio asilia vya utalii, tulikwama wapi?

Unajua mtanzania analipa shs ngapi kuingia national park na mtu asiye mtanzania analipa shs ngapi?

Ukijua Hilo huwezi beza jitihada za kujitangaza nje

..sijabeza jitihada za kujitangaza nje.

..ninachoshauri mimi ni kwamba jitihada za kujitangaza nje, ziende sambamba na jitihada za kuwezesha ongezeko la watalii wazawa.

..tujiwekee malengo kwamba ktk miaka 10 ijayo wazawa wawe 50% ya watalii wanaotembelea vivutio vyetu.
 


Unaongea vitu genuine Sana wewe jamaa
 


Mzawa akaangalie nini?? Tembo au swala, ujue utalii ni hobby bro, -- mtu mlo wake wa siku shida, tozo na kodi kibao, ada za hospitali na za shule nk, atapata wapi pesa ya kutalii.

Nature ya mzungu ni Curiosity katika mambo mengi na utalii ni moja ya Curiosity., Mwafrika naturally is not curious, one of the factors which enhances our underdevelopements is lackal of curiosity.
 
Rais Samia ni mnyenyekevu | Mpole| anastaha | mpenda watu, | Mpenda maendeleo | mchamungu | Mzalendo wa kweli
 
Hao hao chini ya milioni moja wanatosha ,ulizia hao kiduchu hela yao inayokusanywa ni kiasi gani ndio utaona kama hii nchi ina mashimo mengi ya panya buku.
 


Unaeleweka lakini karibu kila mkoa kuna sehemu ya Utali, kweli tunashindwa hata hivyo?
 
Unaeleweka lakini karibu kila mkoa kuna sehemu ya Utali, kweli tunashindwa hata hivyo?


Utalii ni hamasa iliyomo moyoni mwa mtu pamoja na umaskini wetu lakini pia sisi hatuna hamasa ya utalii, kumbuka kwamba kabla ya Wakoloni hawajafika huku Africa wazungu waliwatuma wapelelezi wao kwanza, kumbuka katika zama hizo za giza 1800s mtu anatumwa kuja Africa, Bara jipya kabisa kwao na mtu anajitoma kuja bila kujali hatari itakayomkuta; hii ndiyo nature ya hamasa ya moyoni ya kutalii na kutembea sehemu mbalimbali, hamasa hiyo Wazungu wanayo, baada ya hao wapelelezi kuja na kupeleka taarifa huko kwao kilichofuata unajua; kugawanywa kwa Africa na hatimaye ukoloni. Sisi Waafrica hatukutoka kwenda nje au hata ndani kutafuta makoloni kwasababu hatukuwa na bado hatuna hamasa ya kutalii, kutembea na hata kupeleleza mambo si tu ya kiuchumi bali hata kupeleleza/kutafiti mambo ya kisayansi.

Nimeandika hiyo historia kukazia kwamba Utalii ni jambo la moyoni au hobby ambayo sisi Waafrika wengi wetu hatuna.
 
Wanasema gharama za kutalii tza ni kubwa sana gharama ya siku 1 moja TANZANIA ukienda Morroco unatalii wikii.
KILA kitu bei juu kwa mentality za kizamani za wazungu wanapesa.
 
Mama anatoa Tsh 23.8BL kwaajili ya elimu bure | Mimi Mama Samia hata akiongoza hadi 2035 ni poa to,
 
Ndani ya Uongozi wa Rais Samia,
Mahakama huru,
Bunge huru,
NGOs huru
Media huru

TanzaniakwaniSisi tunatakaje?
 
Mungu Ibariki Africa,
Mungu ibariki Tanzania
Mungu Mbariki Rais Samia,

πŸ™πŸΏπŸ™πŸΏπŸ™πŸΏπŸ™πŸΏ
 
Watalii hawaji mpaka demokrasia itakapotamalaki Tanzania. Chungu kumeza but ndiyo ukweli.

Watalii hawataongezeka hadi pale katiba mpya itakapoandikwa. Unadhani JK (ambaye alikuwa ana interact sana na watalii wakati ule akiwa rais) alikuwa mjinga kuanzisha mchakato wa katiba mpya?
 
Hivi unadhani Watalii wanapenda kila baada ya km 10 polisi wanawasimamisha na kuomba rushwa?

Hivi nani asiyeijua Serengeti dunia hii?

Au unadhani huko duniani hakuna mawakala wanaotafuta watalii kuja huku tz?

Sent using Jamii Forums mobile app

watu wengi sana hawajui serengeti, hata uku uku tanzania kuna watu hawaijui! hata huo mlima the same story, kutanganza ndo kunahitajika mengine yapo kawaida tu

- and on the same time preference znatafautiana kuna wengine wanapenda utalii kupanda milima tu haswa mirefu, wengine mambo ya kale tu huezi mpangia mtu
 


Kwani katiba hii hairuhusu watalii kuingia nchini?!
 
Kwani katiba hii hairuhusu watalii kuingia nchini?!
Ya sasa ni ya mapolisi....inaruhusu mapolisi kuwanyang'anya watalii mali zao pale IGP atakapojisikia kufanya hivyo.
Ni watalii wenye roho ya paka tu (ambao si wengi kama takwimu zinavyothibitisha) ndiyo wanaoweza kuja katikati ya mazingira kama haya!!
 
Mwanamke wa kwanza kuhutubia baraza kuu la Umoja wa Mataifa la 76 tangu tupate uhuru ni Mama Samia Suluhu Hassan,

We Proud on you Mama
_________________________

 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…