SoC02 Tanzania ya sayansi na teknolojia inawezekana, na ina mchango mkubwa katika kuendea kaulimbiu ya Tanzania ya viwanda

SoC02 Tanzania ya sayansi na teknolojia inawezekana, na ina mchango mkubwa katika kuendea kaulimbiu ya Tanzania ya viwanda

Stories of Change - 2022 Competition

Esak

Member
Joined
Aug 1, 2022
Posts
9
Reaction score
10
Je, unahitaji kujua kwa undani nini kifanyike Ili kukuza sayansi na teknolojia nchini usipitwe ndugu mwana JF naomba pia unisaidie kunipigia kura mwishon mwa andiko hili, Mungu akubariki 🙏🏼

Sayansi ni maarifa yapatikanayo kwa kufanya vitendo Ili kudhibitisha habari au jambo fulani. Tanzania imekua ikijihusisha kwenye maendeleo ya sayansi na teknolojia na baadhi ya sera kuhusu sayansi na teknolojia zimeanzishwa, hii imepelekea kuanzishwa kwa chombo kiitwacho Tanzania Commission For Science and Technology (COSTECH).

Pamoja na kuanzishwa kwa sera na chombo hicho bado kuna changamoto mbalimbali zinazoikumba sekta hii muhimu katika maendeleo ya viwanda nchini, Changamoto hizo ni pamoja na ukosefi wa sera wazi au madhubuti juu ya sayansi na teknolojia, utegemezi wa teknolojia ya nje (dependence technology, ukosefu wa motisha na mazingira rafiki kwa wanasayansi na teknolojia wa ndani, msisisitizo mdogo kwenye masomo ya sayansi mashuleni.

Kwa hiyo kutokana na kaulimbiu ya Tanzania ya viwanda Serikali Haina budi kufanya jitihadi kukuza teknolojia nchini itakayoendana na kasi ya Tanzania ya viwanda kwa sababu Tanzania ni mojawapo ya Nchi yenye malighafi na raslimali nyingi Ila tunashindwa kuzitumia kutengeneza bidhaa (products) kwa sababu ya kiwango kidogo cha sayansi na teknolojia.

Hivyo Ili kuepusha utegemezi wa teknolojia ya nje serikali kupitia wizara ya Elimu, Sayansi na teknolojia inatakiwa kufanya yafuatayo:

# Kutokomeza Rushwa katika uingizaji wa teknolojia mpya nchini hii kwa sababu Rushwa italepelekea kuleta teknolojia feki au iliyopitwa na wakati kutokana na ukweli kwamba teknolojia mpya (modern technology) inahtaji mtaji au ruzuku ya kutosha, kwa hiyo matumizi ya fedha za umma kwa manufaa binafsi yanadidimiza ukuaji wa sayansi na teknolojia nchini.

# kusimamia au kuboresha uendeshwaji mzuri wa COSTECH,
Hii itasaidia COSTECH kufanya kazi zake vizuri na kwa weledi kama uanzishwaji wa sera mpya juu ya sayansi na teknolojia, usimamizi wa Tafiti mbalimbali za kisayansi, kurahisha ufanyaji kazi na wadau mbalimbali Ili kukuza sayansi na teknolojia, kushauri serikali kuhusu mambo mbalimbali yahusuyo sayansi na teknolojia, kufanya kazi za utafiti wa viwanda pamoja na mashirika mbalimbali hayo yote yatasaidia kukuza sayansi na teknolojia nchini.

# Uboreshaji wa mazingira na motisha kwa wanasayansi wa ndani ya Nchi ( local craftmen, technocraft and scientist),

Wanasayansi wa ndani hawana budi kithaminiwa na serikali hasa wanapofanya ugunduzi mbalimbali hii itawafariji na kuongeza bidii naaarifa zaidi nakuondoa utegemezi wa teknolojia ya nje.

# kuwepo kwa sera madhubuti na wazi kuhusu sayansi na teknolojia nchini
Sera ni hatua au mawazo flani yanayowekwa na serikali au shirika flani Ili kutekeleza na kufikia malengo flani kwa hiyo serikali iweke sera hizo Ili kutekelezwa na mwisho tuweze kufikia Tanzania ya viwanda iliyohaja na malengo yetu.

Hitimisho Ukuaji wa sayansi na teknolojia hauna budi kutiliwa maanani kwa sababu ni sekta muhimu itakayosaidia maendeleo na mapinduzi ya uchumi na pia ni sekta muhimu kwenye sekta mfano Afya, Kilimo, na Madini,

Ahsantee 🙏🏼🙏🏼 naomba kura yako mwanajamii forums
 
Upvote 23
Kaka naomba nielezee kivip tutajitoa kwenye dependence technology Ili Hali tuna mazingira ambayo siyo conducive??
 
Uzii mzito huu hakika hii ikifuatwa na serikali kupitia COSTECH na wadau mbalimbali italeta mabadiliko
 
Kuwasapoti wanasayansi wa ndani na kuwapa motisha, kuendeleza kile walichogundua na kuwapa mishahara mizuri hii itasaidia kukuza sayansi na teknolojia nchini, Mazingira mazuri inahusisha mitaji kwa ajili ya uwekezaji kwenye sekta hii, suala ambalo serikali inatakiwa kukusanya fedha mbalimbali kutoka katika shughuli nyingine za kiuchumi na kuwekeza pia kualika wadau mbalimbali au wafadhili watakawekeza kwenye sayansi na teknolojia nchini
 
Back
Top Bottom