SoC04 Tanzania ya Uhakika

SoC04 Tanzania ya Uhakika

Tanzania Tuitakayo competition threads

Chilimba

Member
Joined
May 1, 2022
Posts
8
Reaction score
7
Nipende kushiriki katika stories of Change kama mdau wa JF. Kama vijana na wananchi wa Tanzania kunamambo ambayo tungependa kuona Nchi yetu ikiyazingatia hasa katika kuendana na dhima kubwa ya Sayansi na Teknolojia. Ninamambo machache tu kushiriki nanyi.

1. Kuwepo na kitambulisho kimoja ambacho kitakua ni kiunganishi cha vitambulisho vingine, mfano kiwe na taarifa za kuzaliwa, lessen aina zote, pasi ya kusafiria ili kumsaidia mwananchi kupata huduma kwa wakati na kuondoa baadhi ya usumbufu.

2. Kuwepo mfumo wa kuhifadhi taarifa au majina ya mtoto kidigitari nasemea hili upande wa majina yale ambayo unakuta Cheti cha kuzaliwa, vyeti vya taaluma, Na kitambulisho cha Taifa taarifa zinakua tofauti lakini ni vyeti vya mtu mmoja. Kungekua na mfumo wa uingizwaji wa taarifa za mtoto Kungekua hakuna taarifa ambazo zingekua zinatofautiana.

3. Ulipaji wa bidhaa kwa mfumo wa kieletronic, Serikali ingeona umuhimu wa kuhamasisha wananchi wake kupunguza matumizi ya malipo kwa njia ya cash badala yake kuongeza wigo wa matumizi ya Fedha ya kielectoni, hii ingepunguza uchakavu wa fedha, kuimbiwa, usumbufu wa chenji kubwa kuliko ni kodi haitokwepwa hivyo serikali itaongeza pato ipatikanayo na kodi.

4. Ajira za mda za serikari zisimamiwe na idara husika, Mfano sensa na makazi, usimamizi wa wapiga kura; vijana wengi wamesha kua na imani ya kwamba hawana mtu juu yao (connection) hivyo ajira nyingi zinazotolewa wanaonufaika ni wale wale ambao wanawatu juu yao, kungekua na usimamizi usio na upendeleo vijana wangenufaika kwa haki.

5. Kutambua vipaji, vijana wengi wamejikuta wakisomea fani ambazo sio vipaji vyao; serikali ingeona umuhimu kuwa na VETA katika shule za msingi na kunasa vipaji vya watoto wangali bado wako shuleni ingewajengea uzoefu watoto kuwa na ujuzi na kuutumia uwezo kujipatia kipato badala ya kutegemea ajira.

Nipende kuwashukuru wana JF na stories of change 2024 pamoja katika kuifanya Tanzania Bora
 
Upvote 2
Kuwepo na kitambulisho kimoja ambacho kitakua ni kiunganishi cha vitambulisho vingine, mfano kiwe na taarifa za kuzaliwa, lessen aina zote, pasi ya kusafiria ili kumsaidia mwananchi kupata huduma kwa wakati na kuondoa baadhi ya usumbufu.
Kweli kabisa, makompyuta yapo ni kusakinisha tu tayari.
 
Back
Top Bottom