Linguistic
JF-Expert Member
- Mar 16, 2021
- 3,669
- 8,268
Wiki iliyopita siku ya mapumziko nilikwenda kwenye Kiwanja kimoja kutazama Vijana wakicheza Mpira wa miguu kwenye mashindano ya kugombania Kombe la Mbuzi!
Nikagundua kuwa Tanzania tuna vipaji vikubwa sana vya Mpira wa miguu ambavyo vimekosa muongozo wa kucheza mpira wa kitaalam tangu utotoni (Professional football) kutokana na kukosa walimu!
Wakati naondoka akanikimbilia Kijana mmoja akiwa na wenzake
Akaniambia
kaka samahani ninacheza sana mpira lakini nakosa nafasi kwasababu ya hali yetu ni masikini!
Nilishindwa kumuelewa,
Nikamwambia Kipaji hakijifichi, ukifanya vizuri lazima utaonwa, Jifunze zaidi na ongeza juhudi utafanikiwa!
Akaniambia,
Anacheza vizuri mpira wa miguu na aliwahi kujaribiwa katika moja ya klabu kubwa nchini Tanzania na alifuzu majaribio kwa kiwango kikubwa sana lakini alikwamishwa,
Nikamuuliza ilikuwaje,
Akaniambia alipigiwa simu usiku na msimamizi wa yale majaribio ya timu ya Vijana akajulishwa kuwa amefuzu majaribio lakini katika nafasi anayochezea wapo wawili hivyo mmoja atachukuliwa na mmoja ataachwa,
Akaambiwa atoe rushwa ya shilingi laki mbili ili asajiliwe!
Kijana ni mdogo na familia yake ni duni, akajaribu kuongea na wazazi wake lakini nao hawakuweza kuwa na kiasi hicho cha pesa ili watoe rushwa mtoto wao mwenye kipaji asajiliwe!
Ilipofika asubuhi yule mwenzake alifanikiwa kutoa rushwa akasajiliwa na kupewa vifaa na yeye akaachwa!
Hivi ndivyo hali ya rushwa ilivyo kubwa katika Taifa letu!
Hata wenye vipaji wanazuiwa kuonesha karama zao walizojaliwa na Mwenyezi MUNGU!
Kuna wachezaji wanasajiliwa toka nje ambao nikiangalia viwango vyao haviwafikii kabisa wachezaji tulionao hapa Tanzania lakini Watanzania hawa wamezibwa kuonekana na kufanikiwa na ukuta mkubwa sana wa rushwa!
Tuna wachezaji wazuri wengi kuliko akina Sarpong, Mugalu Calinho, Wawa na wengineo lakini rushwa inawakosesha nafasi
Nina hakika ukifuatiliwa usajili wa wachezaji wengi wa nje kuna rushwa kubwa sana,
Wanachukuliwa wachezaji wa nje wasio na viwango kwa madau makubwa ambayo wachezaji hawaambulii fedha hizo, fedha zinaliwa na kamati za usajili!
Tunatoa Pesa nje bila sababu za msingi!
Hata kwenye sanaa nako hali ipo hivyo hivyo!
Nyimbo nzuri nyingi hazipigwi kwasababu walioimba hawajatoa rushwa,
Kwa wasanii wa kike hulazimishwa mpaka kutoa rushwa ya ngono ili nyimbo zao ziweze kupigwa ama waweze kucheza kwenye filamu!
Ni muhimu sasa kwa Serikali kupitia wizara ya Habari, Sanaa na Michezo kushirikiana na Takukuru ili kuchukua hatua za kupambana na rushwa katika sanaa na michezo na kuweka sheria ya Fair competition ili kuzuia watu wabaya wachache wanaotaka kuhodhi sanaa na michezo na kuifanya Tanzania isiendelee!