Tanzania ya "viwanda" imeishia wapi?

Nakumbuka miaka ya mwazo ya mwendazake wimbo wa viwanda uliimbwa sana na tukaambiwa mtu ukiwa vyerehani vinne basi unakiwanda.

Wakaenda mbele zaidi na kusema kila mkoa unaviwanda zaidi ya 100 (hapa figure siikumbuki vizuri ila ilikua kubwa). Na tukaambiwa mpaka mwaka jana Tz kuna viwanda zaidi ya 8400!

Sasa najiuliza je viwanda siku hizi vimeishia wapi? Mbona wanasiasa hawaimbi tena wimbo wa viwanda?
 
Sasa ni Tanzania yakupambana na Chadema.
 
Hiki ktu nlikua najiuliza jana hv mbna wimbo wa Tanzania ya viwanda siusikii? Au kwa sababu sisikilizi taarifa ya habari sku hz?
 
Tuwakaribishe tena WAHINDI warudi kutujengea viwanda kadha wa kadha....
(Rejea miaka ya 60s)
Wahindi wapo vizuri ktk viwanda...
 
Ndiyo zimefanya tuingie uchumi wa kati.
 
Tangu Rais achukue madaraka hajazindua hata kimoja. Vile vilivyokuwa vinajengwa viko wapi?
 
Njoo mkoa wa Pwani ujionee Tanzania ya viwanda inavyomeremeta.

Ukifungia na gaidi ufipa hutaelewa chochote.
Magufuli aliagiza kila mkoa vijengwe viwanda. Mkoa wa Pwani waliitikia, wakaanzisha vingi tu. Ila ni ile aina ya viwanda vya Mwijage. Ukiwa na wake 4 una kiwanda cha kuzalisha watoto
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…