Tanzania ya viwanda inakuja

Tanzania ya viwanda inakuja

Congo

JF-Expert Member
Joined
Mar 13, 2008
Posts
2,081
Reaction score
2,325
Miaka ya hivi karibuni inashuhudia matajiri wakiongezeka. Wanatunza fedha benki. Ndio maana BONDS zikitangazwa fedha zinatolewa zaidi ya bond. Ina maana watamzania wana fedha kwenye mabenki.

Nawashauri watanzania weusi. Wasioogope kuwekeza kwenye viwanda. Matajiri wakubwa ni wenye viwanda. Mitaji inakuwa mikubwa hivyo mafanikio yanaongezeka.

Uwekezaji wa viwanda ndio mtaji mkubwa zidi kwenye nchi.

Serikali inachotakiwa kufanya ni kuweka mzaingira bora. Mfano. Kama viberiti vinaweza kuzalishwa na kutosheleza soko kwa nini viagizwe. Serikali iweke kodi kubwa ili kulinda viwanda vya ndani. Na TRA ihakikishe onatoza kodi halali kwa bidhaa zinazoingia.

Mazingira yaweza kuwa bora lakini kama TRA itashindwa kutoza kodi za mizigo inayoingia nchini kulingana na sheria inavyotala. Viwanda vyetu havitakua.

Wapiga dili wakipatta mamilioni wasipeleke fedha nje ya nchi. Nchi yetu ya amani. Wawekeze nchini. Kila siku kujenga nyumba na magorofa nani atakaa kama hakutakuwa na waajiriwa watakaolipwa mishahara mizuri wakake humo?
 
Back
Top Bottom