Kaka Pekee
JF-Expert Member
- Apr 3, 2018
- 336
- 564
Kuelekea Tanzania ya Viwonder (Viwanda) ni lini tutafikia kutoa support kwa Wataalamu wetu wabuni na kutengeneza Vimashine vidogo au kubwa za kurahisisha kazi na kutengeneza ajira.
Tukiwa na nia ya dhati ya kupata 'Viwanda' inabidi sapoti hizi ziwepo, fungu liwepo na hamasa iwepo.
Yuko wapi yule jamaa aliyeunda Helcopter yake?
Vipi yule aliyebuni Bajaji yake na akaweka hadi milango?
ameishia wapi yule aliyetengeneza Gari yake Mwenyewe kule Mbeya kutoka kwenye Screpa?....
Haya hao wote labda ilikuwa zamani walikata tamaa, vipi huyu wa Juzi tulimuona kupitia Millard Ayo akiwa anatumia Umeme wake mwenyewe?!....amepewa sapoti gani?, pongezi, hamasa je?!
Tukitaka cha Uvunguni Sharti.......enhee!, basi Hii sirikali yetu badala ya kufikiria Mindege tu tulizonazo hadi sasa zimetosha wekeni fungu lingine huku kwa Wabunifu na Watundu wa mambo walete mengi ya manufaa kupitia teknolojia, Vipawa na Ubunifu ili tupate Tanzania ya Viwanda....tuondokane na hivi VIWONDER vya TBC kutembelea Fundi Cherehani kutuonyesha Mafanikio.