TANZANIA YA WATANZANIA
UTANGULIZI
Ili nchi yeyote iweze kuendelea ni lazima kuwe na ushirikiano baina ya serikali, jeshi na wananchi. Katika suala Zima la kuboresha uchumi, siasa na maendeleo ya jamii ni jukumu la kila mmoja katika jamii. Hivyo basi ili Tanzania iweze kufika mbali ki maendeleo ni vyema kuwe na ushirikiano.
KISIASA,
Miongoni mwa nyenzo mhimu zinazosaidia nchi kuendelea ni siasa. Nchi kama marekani, south Korea na china ni nchi zenye maendeleo zaidi kwasababu ya siasa yake imara. . Hivyo serikali ya Tanzania haina budi kuimarisha siasa yake.
Kuna maeneo kadhaa ya kisiasa ambayo yanahitaji mabadiliko nchini Tanzania. Hapa kuna baadhi ya mifano:
. Utaratibu wa Uchaguzi: Kuna haja ya kufanya mabadiliko katika mfumo wa uchaguzi ili kuongeza uwazi, usawa na haki. Mfumo wa sasa unaonekana kuwa na udhibiti mwingi na kutokuwa na uaminifu wa kutosha. Mabadiliko yanapaswa kufanywa ili kuhakikisha kuwa uchaguzi ni huru na wa haki, na kwamba kuna uwazi kamili katika mchakato mzima.
Mamlaka ya Rais: Katiba ya Tanzania inatoa madaraka makubwa kwa Rais. Hii inaweza kusababisha ubaguzi wa madaraka na udikteta. Ni muhimu kufanya mabadiliko ya katiba ili kupunguza madaraka ya Rais na kuongeza uwajibikaji na uwazi katika mfumo wa serikali.
Mfumo wa Vyama vingi: Tanzania ina mfumo wa vyama vingi, lakini mazingira ya kisiasa yanaweza kufanya iwe vigumu kwa vyama vya upinzani kufanya kazi yao kwa uhuru na haki. Mabadiliko yanahitajika ili kuweka mazingira sawa na kuhakikisha kwamba kuna ushindani wa haki katika siasa.
Uwajibikaji: Kuna haja ya kuimarisha uwajibikaji katika serikali na taasisi nyingine za umma. Mambo kama uwazi, uwazi na uadilifu yanapaswa kushughulikiwa kikamilifu na kuzingatiwa kwa kufanya mabadiliko katika mikataba na sheria za kitaifa.
Kupambana na Ufisadi: Ufisadi ni mojawapo ya matatizo yanayoathiri siasa, uchumi na jamii nchini Tanzania. Kuchukua hatua madhubuti kukabiliana na ufisadi, kutekeleza sheria na kuimarisha mifumo ya uwajibikaji kutaimarisha
KIUCHUMI,
Hii ni nyenzo kubwa ambayo ili nchi yeyote iweze kusimama lazima iwe na uchumi mzuri, yaani toshelevu. Tanzania ni miongoni mwa nchi zilizo jaaliwa vyanzo vizuri vya uchumi ikiwa ni pamoja na
- Bahari (zinawezesha usafirishaji)
- Maziwa na mabwaya(ni vyanzo anuai vya umeme)
- Ardhi yenye rutuba ( inawezesha shughuli za kilimo)
- Madini
- Mbuga za wanyama (zunatuletea fedha za kigeni)
- Rasilimali watu ( sensa ya watu na makazi 2022 inataja kuwa ni zaidi ya
NINI KIFANYIKE KUIMARISHA UCHUMI,
1. Kuwekeza katika Kilimo: Kilimo ni sekta muhimu nchini Tanzania ambayo inaajiri zaidi ya asilimia 70 ya nguvu kazi ya taifa. Kuzingatia kilimo cha kisasa, kuboresha teknolojia, kusambaza pembejeo za kilimo, na kuhakikisha upatikanaji wa masoko kwa wakulima itasaidia kuongeza uzalishaji, mapato na usalama wa chakula na bidhaa. Kuwepo kwa mvua za kutosha na maziwa pia kutasaidia katika kukuza kilimo. Hivyo ni jukumu la serikali kuajiri wataalamu wa hali ya hewa na wabobezi wa kilimo watakao toa ufafanuzi kwa wakulima ni lini, wapi na zao gani walime wakati huo
Mfano
Mkoa kagera
Wilaya biharamulo
Biashara. Kahawa na ndizi
Chakula. Ndizi na mkunde
Mwinuko/msl. 1100-1800
Mvua/mm. 600-1400
Joto: 10-30
Udongo: Ph4-7
Mchanganyiko. Tifutifu, kichanga na mfinyanzi.
Mkoa: kagera
Wilaya: Bukoba
Biashara: Kahawa, ndizi, vanilla na chai.
Chakula: Ndizi, mkunde na chai
Mwinuko: 1200-1800
Mvua: 800-1400
Joto: 10-30
Udongo:. Ph4-7
Mchanganyiko. Tifutifu ,kichanga , changarawe na mfinyanzi
Na Mwongozo uzalishaji mazao 2017.
Kupitia hivo itakuwa ni rahisi kwa mkulima kujua alime zao gani kwa mda gani na akiwa sehemu gani.
2. Kuwekeza katika Miundombinu: Kuimarisha miundombinu itasaidia kuongeza uchumi na kuvutia uwekezaji. Tanzania inaweza kujenga na kuboresha barabara, reli, viwanja vya ndege, na bandari hii ikiwa ni pamoja na mjini na vijijini ili kurahisisha usafirishaji wa bidhaa kutoka sehemu za uzalishaji (vijijini ) kwenda masokoni (mjini) na nje ya nchi pia.
3. Kuboresha Mazingira ya Biashara: Serikali inaweza kuchukua hatua za kuondoa urasimu na kuboresha mazingira ya biashara ili kuvutia wawekezaji na kuhamasisha ukuaji wa sekta binafsi. Kuboresha mfumo wa kodi, kupunguza urasimu wa leseni na ruhusa, na kuimarisha mfumo wa sheria na haki za umiliki wa mali itasaidia kuongeza uwekezaji na kuzalisha ajira miongoni mwa wazawa.
5. Kukuza Viwanda:
Hii ni pamoja na kuimarisha viwanda vya ndani vya mikono na kuanzisha viwanda vya kisasa kupitia kuruhusu uwekezaji kwa wadau kutoka nchi jirani na ughaibuni.
6. Kujenga Ushirikiano wa Kimataifa: Tanzania inaweza kujenga ushirikiano na nchi zingine na taasisi za kimataifa ili kupata msaada wa kiufundi, teknolojia, na fedha za maendeleo. Kupitia ushirikiano wa kimataifa, Tanzania inaweza kushiriki katika biashara ya kimataifa, kukuza utalii, na kuinua uchumi wetu.
KIJAMII
Jamii ni watu na watu ndioo jamii.
Hayat Mwalimu J. K Nyerere alianzisha mfumo wa socialism (Ubuntu) kutoka south Africa ambapo dhumuni lake kubwa ilikuwa ni watanzaniaa tuishi kijamaa. "Ubuntu umuntu Akabantu" ikiwa na maana kuwa utu wa mtu ni utu asiye na utu sio mtu ata kama anafanana na mtu. Kwa maana hiyoo alitaka kila mtu amthamin mwenziee
JE NINI KIFANYIKE KUIMARISHA MFUMO WETU WA KIJAMII
1. Kuanzisha madarasa ya ujamaa.
Kupitia madarasa , semina na matamasha mabalimbali tunaweza kuiwezesha jamii na vijana kiujumla kuwa na utu miongoni mwao. Utu ndio nyenzo kubwa katika jamii kwani utasaidia vijana na jamii kushirikiana, utasaidia kuhimiza yaliyomema (uwajibikaji, kujitolea, upendo, ukweli na uwazi, kuwaheshimu wakubwa kwa wadogo) na kukemeaa maovu (rushwa, ubinafsi, dhuluma, ukabila, ulawiti na ubakaji na unyonyaji)
2. Mapinduzi ya mfumo wa elimu.
Mfumo wa elimu yetu adi kufikia hivi sasa n elimu ambayo inamuwezesha mtoto au kijana kujua kusoma na kuandika tu huku akiwa hana weledi na ujuzi kuhusu kitu anachosomea. Hivyo serikali haina budi kuandaa kaadhi ya kada kama ifuatavyo.
-baada ya elimu ya msingi mtoto anatakiwa Moja kwa moja kuanza kusomea kazi anayotaka yeye mwenyewe kuja kuwa. Hii itamsaidia mtoto kuwa na ujuzi na kitu anachosomea tangu utoto wake pia inampunguzia mzigo mkubwa mwanafunzi wakati wa usomaji kuliko kusoma masomo mengi katika elimu yake ya sekondari na baadae anapofika chuo kikiuu anaanza upya kabsa.
- kuwataka wazazi wajue na wahakiki vipaji vya watoto wao wakati wa ukuaji wao.
Kila mtoto anakipaji chake na mara nyingi watoto huonesha vipaji vyao wawapo watoto ingawa jamii nyingi za kitanzania huwa na tabia ya kudharau vipaji hivyo na kupelekea kupotea kwa vipaji. Wakati wa ukuaji wa watoto wengi wao huanza kuchora, kucheza mpira, kuimba, kuruka sarakasi, kutengeneza magari, kushona nguo na Midori, kupika vyakula kwenye makopo,wengine pia hucheza wakiigiza kuwa madaktari, walimu, wanajeshi na mapolisi.
Huo ni mwanga mzuri kwa watoto kwani ni vitu wanavyokuwa wamezaliwa navyo Toka moyoni iwapo mzazi atagundua nini mtoto wake anapenda kuwa na akamshika mkonon mtoto wa namna hiyo labda kwa kumnunulia vitbu vya kategoria hiyo na akampeleka mtoto shule za kipaji chake inaweza kusaidia kupunguza wimbi la wafanyakazi wengi wasio na moyo wa kufanya kazi. Kwani kila kazi ni wito.(passion).
3. Kuhamasisha dini katika jamii zetu
Kupitia dini utasaidia kupunguza baadhi ya mambo machafu yanayoendelea katika jamii . Kwani dini zote uislamu na ukristo zinafundisha maadili mema., Uamunifu, ukweli , uwazi na huruma. Hivo itasaidia viongozi na wanajamii kuishi katika amani na ushirikiano wakiwa na hofu ya mwenyezimungu miyoni mwao.
HITIMISHO
Tanzania ya watanzania ni Tanzania yetu sote kila mmoja anajukumu la kuilinda na kuijenga nchi kama mwananchi wa nchi hiyo. Tuungane na tushirikiane katika kuondoa mizizi ya ukoloni mamboleo katika nchi yetu.

Attachments
Upvote
4