Kwa kweli nashindwa kuelewa ni nini kinachoendelea nchi! Ni kweli mazingira ya kufanya biashara yamekuwa magumu sana kwa wawekezaji wa nje, lakini hasa kwa wawekezaji wadogo wa ndani. Kuna watu sijui ni kwamba hawajui implication ya hii kitu au uzembe tu katika taasisi zao.
Hebu fikiria mipango kama Business Environment Strengthening Programme (BEST) na Property and Business Formalisation Programme (PBFP) inavyokula hela za walipa KODI lakini impact na output zake bado ni ndogo sana. Ina maana Eng. Salema na Lyimo hamuoni haya?
Yaan nchi kama RWANDA ukienda kusajil kampuni, inakuchukua takribani masaa nane to get it done (and when I say to get it done, i mean all the paper work), lakini Tanzania kufanya Name Search tu, ni zaidi ya siku tatu na bado tunasema eti tuko kwenye information era.
Sijui hawa watu huko wizara ya viwanda na biashara wanafanya nini? Kwa mfano Bunge lilipitisha sheria moja iitwayo BARA ( Business Activities Registration Act, 2007) lakini mpaka leo (%years later) haijaanza kutumika. Jamani hata kwa pilot project zinawashinda? Sheria hii pamoja na mambo mengine ilikuwa ina-decentralize shughuli za BRELA ili watu waweze kufanya usajili katika wilaya zao bila kulazimika kwenda Dar es Salaam, tena in ONE STOP
SHOP.