Tanzania yaanza msako wa kilimo cha bangi

Tanzania yaanza msako wa kilimo cha bangi

ldleo

JF-Expert Member
Joined
Jan 9, 2010
Posts
1,116
Reaction score
1,121
Mamlaka za kupambana na dawa za kulevya Tanzania zimeanza msako wa nchi nzima kwa watu wanaolima bangi.

Kamishna Jenerali wa Mamlaka ya Kudhibiti Dawa za Kulevya (DCEA) Gerald Kusaya amesema Jumatano kuwa heka 21 za bangi zilizogunduliwa katika wilaya za Arumeru na Monduli mkoani Arusha zimeharibiwa tangu msako uanze Mei 20, na kuongeza kuwa msako umeanza mkoani humo kwa sababu mkoa huo unasifika vibaya kwa ulimaji wa bangi.

Aidha amebainisha kuwa washukiwa wawili wamekamatwa wakihusishwa na umiliki wa mashamba ya bangi, na wengine wawili wamepatikana wakibeba kilo 220 za bangi kwenye pikipiki.

Amefafanua kuwa msako huo uliofanywa na DCEA ikishirikiana na vyombo vya usalama wakiwemo polisi, utaendelea na utafanyika katika mikoa yote nchini.
 
Rass inno nganyangwa uwapi...??? Njoo mtoe maoni,ushauri na elimu kuhusu huu mmea kwa taasisi hii:
 
Wakati sisi tukipambana kuteketeza bangi, Bunge la Zambia limeshapitisha muswada wa kilimo cha bangi kwa tafiti za kisanyansi.
___________ ____________ _______________

Zambia's cabinet has approved the publication and introduction of a bill in parliament for the legalization of the cultivation of cannabis.

Soma zaidi:
 
Kwanini wasiende kuiuza Jamaika tupate pesa za kigeni?
 
Wenzetu wanalima na kuuza na kujipatia fedha za kigeni,sisi tunaanzisha mshikemshike kuwasumbua wazalishaji
Nalog off Z
 
Back
Top Bottom