#COVID19 Tanzania yafatilia uwapo wa aina mpya ya kirusi cha UVIKO-19

#COVID19 Tanzania yafatilia uwapo wa aina mpya ya kirusi cha UVIKO-19

Cannabis

JF-Expert Member
Joined
Jan 20, 2014
Posts
11,557
Reaction score
33,535
UMMY-2.jpg
Waziri wa Afya nchini Tanzania , Ummy Mwalimu, amesema serikali ya nchi hiyo inafuatilia uwapo wa aina mpya ya kirusi cha UVIKO-19 kilichothibitishwa na Shirika la Afya Duniani (WHO).

Alisema kirusi hicho, kinajumuisha kirusi cha Delta na Omicron, ambacho kimejiunda na kuwa kirusi kipya cha Omicron BA.1.

Waziri Ummy aliyasema hayo jana jijini Dar es Salaam, wakati akizungumza na waandishi wa habari muda mfupi baada ya kufungua mafunzo ya wataalamu wa upasuaji wa ubongo, uti wa mgongo na ugonjwa mahututi yanayofanyika katika Taasisi ya Tiba ya Mifupa na Magonjwa ya Fahamu Muhimbili (MOI).

Alisema WHO inafanya utafiti wa kufahamu ukali wa kirusi hicho kipya na kwa upande wa wizara yake inaendelea kufanya utafiti kuwapo kwa kirusi hicho na kwamba ameshawaelekeza wataalam kufatilia suala hilo.

“Nimeshawaelekeza wataalamu wetu waangalie tuone kama kimeshaingia nchini kwetu kwa sababu nchi nyingine wameshathibitisha,” alisema Ummy.

Waziri Ummy aliwasihi Watanzania kujitokeza kupata chanjo ya UVIKO-19 ili kujikinga na kirusi hicho, kwani chanjo inasaidia pia kupunguza madhara ya ugonjwa huo.

Hata hivyo hali ya uchanjaji bado ipo chini nchini humo kwa sababu asilimia 66 ya wanaougua UVIKO-19 waliolazwa hospitalini hawajapata chanjo, hali ambayo intajwa kuwa ni hatari kwa nchi.

Aidha Ummy alisema kama nchi nyingine ambazo kimeshatangazwa kuwapo, kuna uwezekano wa kuingia nchini kutokana na mwingiliano wa kibiashara katika mataifa mbalimbali duniani.
 
Pana mijamaa ya chama fulani bado itakwambia hiyo ni vita ya mabeberu
 
Hii chanjo iliyoletwa toka mwaka jana, ni kwa ajili ya kirusi kipi sasa, Omicron, Delta au hili tolea jipya, au ni yake matoleo ya mwanzo? Kwa sasa mkubali tu, hili dili la Corona limeshafunikwa na Ukraine conflict, tafuteni namna nyingine ya kupiga pesa, sio lazima kuuza chanjo na vipimio tu, kuweni na utu.
 
Back
Top Bottom