Tanzania yageuka kuwa kitovu cha kusambaza maambukizi ya COVID-19 ukanda wa maziwa makuu?

Tanzania yageuka kuwa kitovu cha kusambaza maambukizi ya COVID-19 ukanda wa maziwa makuu?

Zanzibar-ASP

JF-Expert Member
Joined
Nov 28, 2013
Posts
11,550
Reaction score
40,697
Sio siri tena kwa sasa Tanzania inatajwa vibaya sana duniani kuhusu mapambano dhidi ya COVID-19. Bahati mbaya hali hiyo imepelekea kuitaja Tanzania kama kitovu kipya cha kusambaza maambukizi ya COVID-19 (Covid-19 Epicentre) kwa ukanda wa maziwa makuu.

Hali hii inatokana na hatua ya nchi kadhaa zinazoizunguka Tanzania kueleza kupokea visa vipya vingi kutokea Tanzania na na wakati huo huo zikionyesha kutokukubaliana na namna taifa la Tanzania linavyokabiliana na hatari za kusambaa kwa Corona.

Mpaka sasa nchi za Kenya, Uganda, Rwanda na Zambia zimeweka takwimu rasmi zinazoonyesha visa vipya vilivyotokea huku vikiihusisha Tanzania moja kwa moja na zimeanza kuweka sheria ngumu zaidi kuzuia watu wanaotokea Tanzania kuingia nchini mwao.

Hatua hiyo pia imepelekea kwa Ubalozi wa Marekani nchini Tanzania siku ya jana kutoa tahadhari kuu kwa raia wa marekani waliopo Tanzania kubakia majumbani tu, kwa sababu hali ya maambukizi nchini Tanzania ni ya juu sana huku hospitali za jiji la Dar-es-salaam zikizidiwa na wagonjwa.

Wakati karibu kila nchi ikijaribu kutoa taarifa za mwenendo wa maambukizi ya COVID-19 wa kila siku hali ni tofauti kwa Tanzania ambapo kwa karibu wiki mbili sasa mamlaka za Tanzania zimekuwa kimya kabisa huku Rais wa Tanzania akitilia mashaka mwenendo mzima wa matokeo ya vipimo vya Corona nchini mwake na akihusisha jambo hilo huenda likawa ni njama za makusudi za mataifa ya makubwa kutaka kuichafua Tanzania kwa njia ya kukuza takwimu za maambukizi ya COVID-19. Mara baada ya kuzuka kwa shutuma hizo WHO ilikanusha vikali madai hayo na kusema vipimo vinavyotumiwa Tanzania kupima maambukizi ya COVID-19 ni vipimo sahihi, vinatumika dunia nzima na havina utata wowote katika kutoa majibu stahiki.
 
😭😭😭😭😭😭😭😭😭😭😭
 

Attachments

  • Screenshot_20200513-074757_1589345328887.jpg
    Screenshot_20200513-074757_1589345328887.jpg
    40.5 KB · Views: 1
Upo mtaa wa chato
Huu ni uwongo wa mtandaoni

Tanzania ingekuwa imeathirika na corona tungeona misiba kili kona

Ila mtaani kwetu hakuna taarfa ya msiba wa corona toka hili gonjwa liingie Tanzania
 
Back
Top Bottom