Tanzania yaichapa Libya 9-3, Yatwaa Medali za Shaba (Bronze) kwenye Michuano ya Soka la Ufukweni

Tanzania yaichapa Libya 9-3, Yatwaa Medali za Shaba (Bronze) kwenye Michuano ya Soka la Ufukweni

BARD AI

JF-Expert Member
Joined
Jul 24, 2018
Posts
3,591
Reaction score
8,826
1688157189769.jpeg

Timu ya Tanzania ya Beach Soccer imepata Medali ya Bronze baada ya kufanikiwa kuwachapa Libya Magoli 9-3.

Morocco imetwaa Ubingwa baada ya kutoka Sare ya 3-3 dhidi ya Senegal, mchezo ulioishia kwenye Matuta ambapo Morocco imeibuka na ushindi wa Magoli 4-3.

Mgawanyo wa Zawadi umekuwa kama ifuatavyo, Morocco amechukua Medali za Dhahabu, Senegal wameondoka na Medali za Fedha na Tanzania imebeba Medali za Shaba (Bronze).
1688157199186.jpeg
 
Wangeutumia vyema Uwanja wao wa Mazoezi wa Coco Beach na kuachana na tabia yao ya kupenda Kufakamia Mihogo ya Buku Buku ya akina Sele pale Vibandani wangekuwa wanakuwa wa Kwanza katika kila Mashindano.

Mimi hata siwapongezi nataka Ubingwa.
 
Back
Top Bottom