JanguKamaJangu
JF-Expert Member
- Feb 7, 2022
- 2,780
- 6,607
Timu ya taifa ya Tanzania ‘Taifa Stars’ imeibuka na ushindi wa goli 1-0 dhidi ya Somalia katika mchezo wa kuwania Kufuzu Kombe la Afrika kwa Wachezaji wa Ligi za Ndani (CHAN 2023) kwenye Uwanja wa Mkapa, Dar es Salaam, leo Julai 23, 2022.
Goli limefungwa na Abdul Hamis Sopu dakika ya 47, ukiwa ni mchezo wa kwanza wa mtoano Tanzania wakitambulika kuwa wapo ugenini kwa kuwa Somalia waliomba mchezo wao uchezwe uwanjani hapo
Timu hizo zinatarajiwa kurudiana wikiendi ijayo ambapo mshindi wa hapo ataenda kucheza dhidi ya Uganda, mchezo ambao utaamua nani anafuzu kwenda CHAN 2023.