Tanzania yaimarisha mawasiliano yake ya kibiashara na Malawi

rose mzalendo

Member
Joined
Mar 5, 2019
Posts
71
Reaction score
114
Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Mhandisi Isack Kamwelwe (MB) ameiagiza Mamlaka ya Usimamizi wa Bandari Tanzania (TPA) kujipanga kuhudumia shehena ya mzigo wa Malawi kutoka asilimia 20 hadi 100 kuanzia sasa.
Waziri Kamwelwe ametoa agizo hilo wakati wa kikao cha pamoja baina yake na Waziri wa Uchukuzi na Ujenzi wa Malawi, Mhe. Jappie Mhango (MB) kilichofanyika jijini Dar es Salaam.
“Hivi karibuni kumetokea mvua kubwa ambazo zimesababisha uharibifu mkubwa kwenye Bandari ya Beira nchini Msumbiji pamoja na nchi ya Malawi ambayo awali ilikuwa ikiitumia Bandari hiyo kupitishia mzigo wa Malawi, kutokana na uharibifu huo sasa Malawi wataitumia Bandari ya Dar es Salaam kwa asilimia 100 badala ya asilimia 20 ya awali,” amefafanua Waziri Kamwelwe.
Waziri amesema kwamba Bandari ya Beira kwa sasa imeoshwa kabisa na mafuriko yaliyotokea na jambo hilo sasa linaifanya Malawi kuanza kutumia Bandari za Tanzania hususani Bandari ya Dar es Salaam kwa asilimia mia moja.
Pamoja na hilo Waziri Kamwelwe amesema maamuzi ya kutumia Bandari za Tanzania pia yametokana na mazungumzo ambayo ameyafanya na Waziri mwenzake wa Malawi yaliyolenga kuimarisha mahusiano ya kibiashara baina ya nchi za Tanzania na Malawi.
Ameongeza kuwa mkutano wake na Waziri mwenzake pia umelenga kuona mahusiano baina ya nchi hizi mbili yalianza wapi na wapi wanaweza kuboresha na wamegundua kuwa tayari kulikuwa na mkataba wa mahusiano kati ya Tanzania na Malawi ambao ulisainiwa na Mawaziri wa Uchukuzi mwaka 1987.
“Bahati nzuri tumeupata na tumeupitia mkataba huo wa mahusiano ambao kimsingi ndio uliifanya Serikali ya Malawi ikajenga Bandari kavu ambazo leo zinazojulikana kama Malawi Cargo hapa Dar es Salaam na Mbeya,” amefafanua Waziri.
Amesema kuwa ili kuendelea na utekelezaji wa mkataba huo wamekubaliana kuunda timu ambayo itapitia mkataba huo ambao kimsingi haujawahi kufanyiwa marekebisho ili uweze kukidhi matakwa ya sasa ya kisheria, taratibu na kanuni kwa lengo la kuingiza mabadiliko yatakayokidhi mahitaji ya sasa ya kijamii na kibiashara.
Mhandisi Kamwelwe ameongeza kuwa katika kutekeleza mkataba huu Mawaziri watakuwa wakikutana kila baada ya miezi sita ili kujadili mambo ya kibiashara na kwa kuanzia tayari amemuagiza Mkurugenzi Mkuu wa TPA, Mhandisi Deusdedit Kakoko kujipanga kuhudumia nyongeza ya shehena ya mzigo kutoka Malawi kwa asilimia 100.
“Ni lazima mjipange ili kuhakikisha mzigo unapitia kwa haraka katika muda wanaotaka wateja wa Malawi na kwa bahati nzuri kwenye Bandari Kavu za Malawi kuna miundombinu mingi mpaka matanki ya mafuta hivyo ni matumaini yetu kwamba mzigo utaongezeka,” ameongeza Waziri.
Sambamba na hilo Waziri amebainisha kwamba Serikali itahakikisha kwamba mahusiano ya kibiashara na kijamii baina ya Tanzania na Malawi yanakuwa makubwa na ili kutekeleza hilo wamejipanga kufanya kikao kingine tarehe 14 Juni 2019 jijini Dar es Salaam.
Inatarajiwa kwamba timu ya wataalamu mbalimbali kama vile Wanasheria, Wataalamu wa Biashara na Maafisa Mipango watapitia makubaliano ya mwaka 1987 na kuweza kuona endapo kuna haja ya kubadili kidogo baadhi ya vifungu vya makubaliano ili kuviboresha na kuendana na hali ya sasa hivi.
Kwa upande wake Waziri wa Uchukuzi wa Malawi Mhe. Mhango amesema wanaishukuru sana Serikali ya Tanzania kwa undugu mkubwa waliouonesha kwa Wananchi wa Malawi na hasa katika kuwapatia msaada mkubwa wa madawa na chakula kwa waathirika wa mafuriko.
 
Ama kweli kufa kufaana

Waichangamkie sasa hii fursa ata kama bandari ya beira ikipona wamalawi waendelee kuitumia bandari ya dsm

Sent using my iPhone using jamiiforum app
 
Dah. Kumbe huko kunabalaa isee bandati imeenda yote.. Duh kwahiyo sasa wale wakongo waliokuwa wamehamia beira huko watarudi dsm na malawi pia watatumia hii bandari yetu..

I wish ningekuwa mkurugenzi hapo bandarini jawa wasingerudi kutumia tena bandari ya beira huko.
 
Umewaza kama mm hii nafasi wangeipata wakenya dah.......
Sent using my iPhone using jamiiforum app
 
Hongera mlio pewa dhamana ya kuwasilisha nchi zenu na mnapambana kuhakikisha nchi zenu zinanufaika na uwakilishi wenu
 
Yaan ata ile SGR yetu tungejenga kuelekea kusini kule ndio kuna soko la kweli ila kule kaskazini hamna biashara ya kweliii
 
Yaan ata ile SGR yetu tungejenga kuelekea kusini kule ndio kuna soko la kweli ila kule kaskazini hamna biashara ya kweliii
Target ni congo kwanza maana drc wapo eneo la kimbinu zaidi lkn kuna siri pia ya SGR kuelekea huko ambayo ni kutaka kuwin ule mpango wa China one road network

Sent using my iPhone using jamiiforum app
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…