Tanzania yajipanga kujenga setelaiti yake

Tanzania yajipanga kujenga setelaiti yake

Herbalist Dr MziziMkavu

JF-Expert Member
Joined
Feb 3, 2009
Posts
42,872
Reaction score
34,363
Tanzania yatangaza mpango wa kujenga na  kurusha setelaiti yake angani. Picha: Ikulu Tanzania.jpeg

Tanzania yatangaza mpango wa kujenga na kurusha setelaiti yake angani. Picha: Ikulu Tanzania

Katika kukuza na kuendeleza tekinolojia, Tanzania kupitia rais wa nchi hiyo Samia Suluhu Hassan imetangaza kuwa inajenga setelaiti yake na tayari harakati zimeanza.

Na Lulu Sanga
Kwa mara ya kwanza Rais wa jamuhuri ya muungano wa Tanzania ameweka wazi mpango wa nchi hiyo kujenga na kurusha setelaiti yake angani ambayo itafanyikia nchini humo.
Rais huyo amezungumza hii leo wakati akiwa katika hafla ya uzinduzi wa mradi wa minara ya kurusha matangazo ya Televisheni ardhini (DTT), ambapo amesema kuwa tayari mazungumzo yamekwisha anza.
"tunajipanga kuja na setelaiti ambayo niwahakikishie kuwa itakuwepo Tanzania, tunajipanga vizuri tumeanza mazungumzo tutajenga setelaiti Tanzania.” Rais Samia alibainisha
Mpango wa serikali ya Tanzania unawekwa wazi mwezi mmoja tu tangu kurushwa kwa setelaiti ya nchi jirani ya Kenya.
Ikiwa Tanzania itafanikisha hatua hiyo kubwa katika ulimwengu wa tekinolojia, itakuwa ni miongoni mwa nchi chache za Afrika zilizofanikisha kupeleka kifaa hicho angani yaani Algeria, Ethiopia, Kenya, Zimbabwe, Afrika Kusini, Morocco, Misri, Ghana na Nigeria
chanzo.https://www.trtafrika.com/sw/africa/tanzania-yajipanga-kujenga-setelaiti-yake-13284982
 
Mmh! Hiyo Satellite itakuwa inaangaza maandamano ya chadema tu.
 
me nachojua kuwa Tanzania tunaweza kutengeneza kilimanjaro lite au Castle lite.. Sio satellite
 
Back
Top Bottom