Tanzania Yang'ara Utalii wa Tiba Afrika Mashariki

Tanzania Yang'ara Utalii wa Tiba Afrika Mashariki

benzemah

JF-Expert Member
Joined
Nov 19, 2014
Posts
1,533
Reaction score
3,187
Tanzania imetajwa kung'ara katika utalii wa tiba kutokana na watu kutoka nchi mbalim- bali zikiwamo za Jumuiya ya Afrika Mashariki (EAC) kujitokeza kwa wingi kupata matibabu ya kibingwa kwa magonjwa tofauti hususani moyo, mifupa na saratani.

Waziri wa Afya, Ummy Mwalimu alisema tangu Julai 2022 hadi Machi 2023, wagonjwa 812 kutoka nchi hizo za ukanda, wamehudumiwa nchini katika hospitali za taifa, hospitali maalumu na za kanda.

Julai 2021 hadi Machi 2022, idadi ya waliofika nchi ni kutoka Kenya, Uganda, Burundi, Rwanda, Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo (DRC) na Sudan Kusini ilikuwa 368, hali inayoonesha kuwapo ongezeko kubwa.

Licha ya nchi za EAC, wengine wametoka nje ya ukanda hususani nchi za Zambia, Comoro, Zambia, Malawi na Msumbiji kwa ajili ya kupata matibabu nchini. Katika hotuba ya bajeti ya wizara yake aliyoisoma bungeni wiki iliyopita, Ummy alielezea utendaii kazi wa hospitali zinazotoa huduma za kibingwa nchini ikiwamo Hospitali ya Taifa ya Muhimbili (MNH).

Alisema utalii wa tiba umeendelea kuimarika nchini baada ya uamuzi wa serikali kuimarisha huduma za kibingwa na ubingwa bobezi hali inayozidi kuvutia wagonjwa kutoka nchi mbalimbali kuzifuata Tanzania.

"Serikali inayoongozwa na Rais Samia Suluhu Hassan itaendelea kuimarisha upatikanaji wa huduma hizo na kuanzisha nyingine ili Tanzania iwe kitovu cha utalii tiba barani Afrika," alisema Ummy.
 
Imeng'arang'araje wakati kila kona ya nchi hii watu wanataabika na huduma mbovu hospital?Au kwa kuwa wanapenda kusifiwa?
 
Back
Top Bottom