SoC04 Tanzania yangu: Mazingira yangu ndiyo kesho yangu

SoC04 Tanzania yangu: Mazingira yangu ndiyo kesho yangu

Tanzania Tuitakayo competition threads

isaac shonga

New Member
Joined
Nov 1, 2015
Posts
1
Reaction score
0
Idadi ya watu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania inakua kwa kasi na hasa katika maeneo ya vijijini kutoka watu milioni 12 (sensa 1967), milioni 33.5 (2002), milioni 44 ( 2012) na milioni 62 (2022), idadi ya watu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania inatarajiwa kuongezeka hadi milioni 80 ifikapo mwaka 2035 na hadi zaidi ya milioni 129 ifikapo mwaka 2050. (UN DESA Population Division, 2019b).

Ongezeko hili kubwa la watu linapelekea uharibifu wa mazingira wa moja kwa moja kwa sababu zifuatazo:

  • Ukosefu/upungufu wa ardhi kwa ajili ya kufanya kilimo cha mazao ya biashara na chakula
  • Uhitaji wa maeneo kwa ajili ya makazi hivyo kupelekea watu kuharibu mazingira kwa kukata miti ili kupata maeneo ya ujenzi
  • Kuongezeka kwa uhitaji wa nishati ya kupikia (kuni na mkaa)
  • Kukosa maeneo ya ufugaji hivyo kupelekea mifugo wengi kufugwa katika eneo dogo na,
  • Kuongezeka kwa shughuli za ujangili, uwindaji haramu na uvuvi haramu.
Aidha, athari za mabadiliko ya tabianchi zinaendelea kuwatumbukiza watu wengi katika dimbwi la Ujinga, umaskini na magonjwa ya mlipuko. Kuwepo kwa vipindi virefu vya ukame, mvua zisizo na msimu maalumu, vimbunga, mafuriko na matetemeko ya ardhi ni baadhi ya ishara za mabadiliko ya tabianchi ambavyo kwa namna moja au nyingine hupelekea watu kushindwa kulima au mazao kuharibiwa vibaya na kusababisha hali ngumu kwa wananchi hawa na kupelekea umasikini.

Serikali kwa kushirkiana na wadau wengine, sekta binafsi, taasisi za dini na mashirika mengine ya ndani na nje yanafanya jitihada mbalimbali katika kuhamasisha juu ya uhifadhi na utunzaji wa mazingira. Jitihada hizo na pamoja na Serikali kuanzisha kampeni mbalimbali za upandaji wa miti kama vile kampeni ya MAZINGIRA YANGU,TANZANIA YANGU NAIPENDA DAIMA na kampeni ya SOMA NA MTI ambazo zote zinalenga kuhamasisha watu kuwa na kawaida ya kupanda miti kwenye maeneo yao.

Madhara yanayotokana na shughuli za binadamu–mabadiliko katika matumizi ya ardhi, matumizi mabaya ya ardhi, uzalishaji wa gesi ya ukaa inayosababisha mabadiliko ya tabianchi, uchafuzi na ueneaji wa aina ya miti isiyokuwa ya kiasili–ni masuala yaliyo wazi.

Kwa mujibu ya ripoti ya wakala wa misitu Tanzania (TFS) zaidi ya hekta laki nne za misitu hupotea kila mwaka kutokana na shughuli za kibinadamu ikiwemo uanzishwaji wa mashamba mapya ya kilimo, ukataji miti kiholela kwa ajili ya matumizi ya kuni na mkaa na upasuaji mbao.

Aidha kwa sasa, uchafuzi umeharibu maji katika maeneo ya mbalimbali na aina nyingi ya samaki wanaangamia. Shughuli za binadamu pia zimechangia hali ambayo hupelekea virusi kusambaa kwa haraka kati ya wanyama na binadamu, na kupelekea kuzuka kwa magonjwa ambukizi kama vile COVID-19.

Kwa mjibu wa ripoti iliyochapishwa mwaka jana, hali isiyoweza kubadilishwa ya uharibifu wa mazingira ya kiasili imekuwa tishio kubwa kwa miongo miwili iliyopita linaloathiri hatua za kufikia Malengo ya Maendeleo Endelevu.

Licha ya hayo, bado kuna uwezekano wa kuwa na hatima nzuri, ila tunahitaji kufanyia sera ya maendeleo mabadiliko makubwa na kuchukua hatua mwafaka.

Hata hivyo kwa lengo la kufikia malengo endelevu ifikapo 2030 (SDGs) serikali kwa kushirikiana na wadau wengine inapaswa kufanya yafuatayo kukabiliana na mabadiliko ya tabianchi:

  • Kushirikiana na wadau mbalimbali ikiwa ni pamoja na wawekezaji katika nyanja ya uhifadhi wa mazingira wa ndani na nje ya nchi wanaoonyesha nia ya kuwekeza katika sekta ya mazingira kama vile NGOs, mashirika ya dini,taasisi mbalimbali na mtu moja moja.
  • Kutoa elimu kwa wananchi juu ya kilimo bora kinachotumia eneo kidogo na kisichoharibu mazingira kama vile kilimo mseto (kuchanganya miti na mazao, agroforestry)
  • Kuhamasisha matumizi ya nishati mbadala ya kupikia kama vile majiko banifu, majiko ya mayoni (yanatumia pumba), mkaa mbadala unaotokana na mabaki ya mimea na takataka (briquettes), majiko ya gesi (kwa kushusha bei ya gesi) na majiko ya umeme. Ripoti za hivi karibuni zinaonyesha ukataji mkubwa wa miti unatokana na sababu za uhitaji wa nishai za kupikia kama vile kuni na mkaa.
  • Kuwawezesha wananchi kiuchumi. Hapa serikali kupitia wadau mbalimbali wanaweza kuwahamasisha wanachi kujiunga kwenye vikundi na kuwapatia mafunzo ya ujasiriamali kasha kuwapatia mitaji ya kuanzisha kile walichojifunza,mfano vikundi vya ufugaji wa kuku, ufugaji wa nyuki, VICOBA n.k. Hii itawasaidia wananchi wanaofanya shughuli haramu za uharibifu wa mazingira waache na wajiunge kwenye vikundi na kufanya sughuli halali.
  • Serikali pia iingize somo la mazingira mashuleni kwenye mtaala wake. Hii itasaidia watoto kupata elimu ya uhifadhi na utunzaji wa mazingira tangu wakiwa wadogo na kuwafanya wakuwe wakiwa na shauku ya uhifadhi.
  • Serikali pia iongeze idadi ya ajira za wataalam na washauri wa maswala ya mazingira kuanzia ngazi ya kata. Hii itasaidia kufika kwa elimu ya mazingira kwa jamii kwa wakati na kwa ufasaha. Kwa sasa serikali haina maafisa wa mazingira katika ngazi ya kata.
  • Serikali iongeze kasi katika kupanga matumizi bora ya ardhi kupunguza madhara yanayotokana na ukosefu wa matumizi bora ya ardhi. Hapa namaanisha mfugaji ajuwe maeneo yake ya malisho, mvuvi ajue wapi na wakati gani anatakiwa avue samaki, wapi viwanda vijengwe n.k.
Siku hizi uhusiano wa umaskini na uharibifu wa mazingira unaeleweka vizuri. Mathalani, uharibifu wa mazingira husababisha umaskini kwa kupunguza upatikanaji wa maji safi, rutuba katika udongo, mazao na huduma nyingine muhimu kwa afya na maisha ya binadamu.

Aidha umaskini nao husababisha uharibifu wa mazingira kwa kudhoofisha juhudi na uwezo wa binadamu kusimamia na kutumia rasilimali kwa njia endelevu.

Kwa kuhitimisha , jitihada zaidi na ushirikiano madhubuti kati ya serikali na wadau wengine zinahitajika ili kufanikisha suala la utunzaji wa mazingira nchini Tanzania.
 
Upvote 0
Jitihada hizo na pamoja na Serikali kuanzisha kampeni mbalimbali za upandaji wa miti kama vile kampeni ya MAZINGIRA YANGU,TANZANIA YANGU NAIPENDA DAIMA na kampeni ya SOMA NA MTI ambazo zote zinalenga kuhamasisha watu kuwa na kawaida ya kupanda miti kwenye maeneo yao.
Nzuri, kupendezesha miji pia sawa.
Kutoa elimu kwa wananchi juu ya kilimo bora kinachotumia eneo kidogo na kisichoharibu mazingira kama vile kilimo mseto (kuchanganya miti na mazao, agroforestry)
Nzuri
 
Kuhamasisha matumizi ya nishati mbadala ya kupikia kama vile majiko banifu, majiko ya mayoni (yanatumia pumba), mkaa mbadala unaotokana na mabaki ya mimea na takataka (briquettes), majiko ya gesi (kwa kushusha bei ya gesi) na majiko ya umeme. Ripoti za hivi karibuni zinaonyesha ukataji mkubwa wa miti unatokana na sababu za uhitaji wa nishai za kupikia kama vile kuni na mkaa.
Lakini rai iwe ni kupata nishati. Maana noshati ni muhimu sana. Wananchi wasibaniwe mno wakati wanamiliki(kwa pamoja) misitu mikubwa tu na uchafuzi wetu sio mkubwa sana bado. Kwa hivyo sera zibalansi
Screenshot_20240506-095702_Chrome.jpg
 
Back
Top Bottom