SoC02 Tanzania yangu

Stories of Change - 2022 Competition

Ibojr

New Member
Joined
Jul 24, 2022
Posts
3
Reaction score
3
TANZANIA YANGU

1. ~Mkumbushe mwanao kuwa WIVU utamfanya amchukie Mtu ambaye alipaswa ajifunze kutoka kwake..✍🏻

2. ~Mkumbushe Mwanao kuwa Msaada sio Haki yake asipopewa Asinung'unike atafute Chake...✍🏻

3. ~Mkumbushe Mwanao kuwa Tumeona mazuri kwa watu waliokuwa wakiitwa wabaya na Tumeona mabaya kwa watu waliokuwa wakiitwa wazuri kwahiyo Aishi na kila mtu kwa akili...✍🏻

4. ~Mkumbushe Mwanao kuwa bila Mungu hatofika popote...✍🏻

5. ~Mkumbushe Mwanao kuwa Tunakosa Usingizi ili wanaotutegemea wapate kulala Vizuri...✍🏻

6. ~Mkumbushe Mwanao kuwa Akiwa baba hata akiumwa hatotamani watoto wajue maana tumaini lao pekee ni yeye...✍🏻

7. ~Mkumbushe Mwanao kuwa Kilicho bora kwake hakiwezi kuwa bora kwa watu wengine...✍🏻

8. ~Mkumbushe Mwanao kuwa Alipoamka leo kuna Mwenzake amevuta Pumzi ya Mwisho, inabidi amshukuru Mungu kwa hii zawadi ya Siku Nyingine...✍🏻

9. ~Mkumbushe Mwanao kuwa Njia yake ikishanyooka Asithubutu kuwanyooshea vidole ambao Njia zao bado zina KONA...✍🏻

10. ~Mkumbushe Mwanao kuwa Mtu atakae mpatia Bega wakati analia basi Asimsahau wakati amenyamaza...✍🏻

11. ~Mkumbushe Mwanao kuwa Wengine hatuna Mtu wa kumtegemea au Ndugu wa kumlilia Shida, Ukimtoa MUNGU Tunaamini sana kwenye Nguvu, Juhudi na Maarifa Yetu. ZAIDI Aishi Vizuri na Watu ila asijipe umuhimu kwenye maisha ya WATU...✍🏻

12. ~Mkumbushe Mwanao kuwa anayemuona anacho kuna siku alikua hana kama yeye Msihi aendelee kutafuta...✍🏻

13. ~Mkumbushe Mwanao kuwa akitanguliza kutafuta Umaarufu kabla ya Pesa basi ku-FAKE kutamtesa...✍🏻

14. ~Mkumbushe Mwanao kuwa tunaanzaga na tulicho Nacho ili kutafuta ambacho Hatuna...✍🏻

15. ~Mkumbushe mwanao kuwa Furaha ya kweli katika maisha ni pale tu anapokuwa na Amani ya Moyo bila kujali hali ya maisha aliyonayo...✍🏻

16. ~Mkumbushe mwanao kuwa kuna maamuzi ili yamletee Faida lazima yamuumize kwanza...✍🏻

17. ~Mkumbushe mwanao kuwa asivuke Bahari Kusalimia Watu Ambao Hawawezi Kuvuka Hata Mfereji ili kumjulia Hali Yake...✍🏻

18. ~Mkumbushe mwanao kuwa bila Mungu sisi si chochote si lolote...✍🏻

19. ~Mkumbushe mwanao kuwa uvivu ni chanzo cha fikra potofu dhidi ya waliofanikiwa...πŸ™„

20. ~Mkumbushe mwanao kuwa heshima yake ya uzeeni hutengenezwa ujanani...✍🏻

Nondo za maana hizo...naiona Tanzania yenye kustawi kwa kasi endapo tukinywa vyema maarifa katika kisima cha nasaha za wazee wetuπŸ™πŸ»
 
Upvote 1
Be innovative my brother this is competition but all in all appreciate but remember one thing your youth and world demands as to be creative
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…