Tanzania yaongoza kwa umaskini Afrika Mashariki

Makupa

JF-Expert Member
Joined
Apr 11, 2011
Posts
6,822
Reaction score
4,034
Ripoti ya benki ya dunia imeonyesha kuwa Tanzania pamoja na uwepo wa amani na kuwa ya pili kwa uchumi mkubwa ina idadi kubwa ya watu wanaoishi kwa umaskiini. Kwa mujibu wa ripoti hiyo, idadi ya wanaoishi kwa umaskini nchini uganda ni asilimia 38, Kenya ni asilimi a 43, Rwanda ni asilimia 63 na Tanzani a ni asilimia 68. Kwa mujibu wa ripiti hiyo eneo la kusini mwa jangwa la sahara liko nyuma katika kufikia malengo ya mileniia.
 
Mbaya zaidi, ni nchi inaongoza kwa rasilimali kuliko zote EA, ila rais akiulizwa kwa nini nchi yetu ni masikini anakuwa hana jibu....
 
Hata wakati wa Miaka 23 ya utawala uliotukuka na kuifanya Tanzania nchi ya Ujamaa na kujitegemea bado Tanzania ilishindwa kuzishinda kiuchumi Uganda na Kenya chini ya Iddi Amin Dadaa na Jomo Kenyata.
 
Mbaya zaidi, ni nchi inaongoza kwa rasilimali kuliko zote EA, ila rais akiulizwa kwa nini nchi yetu ni masikini anakuwa hana jibu....

sawa Kikwete hajui kwanini sisi ni maskini lakini Nyerere,Mwinyi na Mkapa walijua sababu za Umaskini wetu kipi kiliwashinda kuondoa umaskini?
 
Mbaya zaidi, ni nchi inaongoza kwa rasilimali kuliko zote EA, ila rais akiulizwa kwa nini nchi yetu ni masikini anakuwa hana jibu....

Ni lazima tuendelee kuwa maskini kwa maana hata hao wanaojiita wapambanaji hawana jipya kila kukicha ni maandamano tu kuanzia jumatatu hadi ijumaa.Jamani hamasisheni vijana kufanya kazi na si kuandamana ili kumfurahisha mwenyekiti wao na katibu wa cdm
 
Ni lazima tuendelee kuwa maskini kwa maana hata hao wanaojiita wapambanaji hawana jipya kila kukicha ni maandamano tu kuanzia jumatatu hadi ijumaa.Jamani hamasisheni vijana kufanya kazi na si kuandamana ilinkumfarhisha mwenyekiti wao na katibu

Usiwe na shaka umasikini utakuwa historia by 2015-16, only ndani ya mwaka moja, ndio utajua kwa nini tulikuwa tunaandamana... kwa sasa una ukungu machoni mwako...
 
sawa Kikwete hajui kwanini sisi ni maskini lakini Nyerere,Mwinyi na Mkapa walijua sababu za Umaskini wetu kipi kiliwashinda kuondoa umaskini?

Hilo siyo level yangu ni swali la kito toto sana find the form two atakujibu kwa nini nchi hii ni maskini, or why Mkapa, Mwinyi and nyerere hawakuweza kuondoa umaskini....2015 tutawaonyesha kwa vitendo, magamba na mafisadi hamtoamini macho yenu
 
mijitu mingine bwana inatia hasira sana, wewe unataka kuufananisha uchumi wa watu milioni zaidi ya 40 na 30?? kijiografia pamoja na idad iya watu Tanzania imezizidi hizo unazozitaja, lakini ukiangalia chumi za nchi za afrika mashariki, Tanzania bado ina nguvu sana, ukilinganisha pia hali ya mtu mmoja mmoja kiuchumi kwa nchi hizo bado utakuta wananchi wa Tanzania wanajiweza kuliko wa nchi tajwa. Tanzania, unakuta mtu ana kipato kidogo lakini ana ardhi, kenya matajiri wachache wasio nacho kabisa ni wengi, Uganda pia hali mbaya zaidi kuliko mahesabu ya vitabuni
 
Increased inflation rate as opposed to per capital income, low agricultural produce support, corruption and embezlement of public funds, weak national policy, roaming democracy and advocacy, bad governance, low escape root from poverty, bad trade and commerce mechanism, mis- management of resources and lack of patriotism.....what do you expect? it is our curse.
 
Mleta mada anza kutembea ukiwa umechomwa ganzi maana habari hii hawaipendi usalama wa wa huni aka wangoa ngucha bila ganzi sasa ili kuwa komoa tembea naganzi kabisa ukiona niaje niaje unajiwahi na ganzi....
 
Ni nchi gani ambako hawaandamani ukiona maandamano yamezidi ujue dhuruma imezidi sana nchi hivyo hata maanandamao lazima yazidi.....hata hivyo tulikaa miaka migai bila maandamono ulifika wapi kimaendeleo..
 
Hata wakati wa Miaka 23 ya utawala uliotukuka na kuifanya Tanzania nchi ya Ujamaa na kujitegemea bado Tanzania ilishindwa kuzishinda kiuchumi Uganda na Kenya chini ya Iddi Amin Dadaa na Jomo Kenyata.

Acha utoto. Nyerere alibinafsisha mgodi gani au aliuza mbuga ipi kwa Waarabu?
 
Hata Rwanda imetushinda!!Wakati wa uhuru TZ na Malaysia tulikuwa sawa kiuchumi lakini leo wenzetu wako juu.Tunalana gani?
 
chitambikwa maendeleo hayo anayajua KINANA Katibu Mkuu wa CCM bigwa wa ufisadi kila sehemu yeye ana kampuni ya wizi wa mali za Watanzania.Tuanze na hii Falcon laundry aliibia jeshi mashine za msaada za kufua kwenye hosptali za jeshi, hivi sasa kampuni yake ya WIA ya mtandao wa Internet ameibia na kufisadi Bandari mabilion ya fedha, Kampuni yake ya TALL inahusika kusafirisha na kutunza container za meno ya tembo ya mabilion ya shilingi na Emirates Sshipping Company ambayo yeye ni wakala wake Tanzania ndiyo inasafirisha macontainer ya meno ya tembo kwenda China na HongKong.Sheria ya Wakala na Tra inakataza mmiliki wa Wakala wa MELI kuwa na ICD , lakini kINANA ANA MILIKI ICD na bado ni wakala wa EML. Tanzania ccm wameiozesha yote kwa tamaa za utJIRI NA UIFSADI.kINANA KELELE ANAZOPIGA ZOTE DHIDI YA CHADEMA ANAJUA SIYO MSAFI NA 2015 MAJI YA SHENGO LAZIMA AFANYE KAZI USIKU NA MCHANA KULINDA MASLAHI YAKE NA MAFISADI WENZAKE. NOTE THIS
 
Last edited by a moderator:
Hata wakati wa Miaka 23 ya utawala uliotukuka na kuifanya Tanzania nchi ya Ujamaa na kujitegemea bado Tanzania ilishindwa kuzishinda kiuchumi Uganda na Kenya chini ya Iddi Amin Dadaa na Jomo Kenyata.

Mkuu twende taratibu kidod; miaka hiyo 23 unayoiita ya utawala uliotukuka haikutusaidia kupiga hatua kwa sababu aliyeongoza nchi alikuwa na akili za kikomunisti. Hakuna nchi yoyote ya kikomunisti au kijamaa iliyowahi kupiga hatua kiuchumi duniani ikiwa chini ya mfumo huo. Ujamaa na uchumi ni vitu viwili tofauti. Nyerere alipotangaza propaganda zake za ujamaa na kujitegemea alitarajia watu wajitegemee vipi wakati hakuruhusu elimu ya maana ipatikane?
Wakati nchi kama Singapore na Korea ya Kusini zinajenga misingi ya maendeleo miaka ya sitini yeye alikuwa anahangaika kukomboa nchi zingine wakati kwake hakuna kitu. Huo ndiyo mwanzo wa maafa ya kiuchumi kwa Tanzania.
 
MWENYEKITI wa Chama cha Wananchi (CUF),Profesa Ibrahim Lipumba, amesema theruthi tatu ya wakazi wa jiji la Dar es Salaam wanakabiliwa na umasikini wa kutisha kutokana wakazi wake kuishi kwa sh 640 kwa siku.
Lipumba alisema chimbuko la umasikini huo ulichangiwa na ongezeko la watu huku wengi wao wakikabiliwa na ukosefu wa ajira za kueleweka.
Alisema jiji hilo lenye idadi ya wakazi wapatao milioni 4.5, kati ya hao ni milioni 1.3 wenye ajira, wengine ajira zao ni zile za kubahatisha.
 
Sasa kama hata rais mwenyewe hajui kwanini nchi yake ni masikini mnategemea nini?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…