Tanzania yapaa nafasi ya 6 kati ya nchi 54 za Afrika kuwa na mtandao bora wa barabara

Tanzania yapaa nafasi ya 6 kati ya nchi 54 za Afrika kuwa na mtandao bora wa barabara

MTANZANIA620

Member
Joined
Jun 20, 2023
Posts
65
Reaction score
81
Tanzania imepaa mpaka nafasi ya 6 toka nafasi ya 16 mwaka 2022 kati ya nchi 54 za Afrika kuwa na mtandao bora wa barabara kwa mujibu wa Takwimu za mtandao wa Statista.

Hii ni kwa sababu ya kazi nzuri ya utekelezaji wa miradi ya barabara na madaraja yenye lengo la kuboresha huduma za usafiri na usafirishaji inayofanywa na serikali ya Awamu ya sita chini ya Mheshimiwa Rais Dkt

Kwa uchache tu tuone baadhi ya kazi ambazo Rais Samia Suluhu Hassan amefanikisha:-

Utekelezaji wa miradi 77 ya ujenzi wa barabara na madaraja inayoendelea kupitia TANROADS yenye thamani ya Shilingi Trilioni 4.6.

Ukamilishaji kwa asilimia 100 miradi 25 ya ujenzi wa barabara yenye urefu wa kilometa 1,198 iliyogharimu Shilingi Trilioni 1.68

Ujenzi wa Daraja la J.P Magufuli (Kigogo Busisi) ambalo linagharimu Shilingi Bilioni 717 limefikia zaidi ya asilimia 94.

Huu ni utekelezaji wa vitendo wa Ilani ya Uchaguzi ya CCM 2020 - 2025.

#SamiaKazini #HatunaMbadala2025
#TunaendaNaSamia
#TukiahidiTunatekeleza
#KaziIendelee
 
Attachments

  • 20241030_091918.jpg
    20241030_091918.jpg
    536.5 KB · Views: 8
  • 20241030_091611.jpg
    20241030_091611.jpg
    177.3 KB · Views: 7
  • 20241030_091907.jpg
    20241030_091907.jpg
    763.4 KB · Views: 7
  • 20241030_091705.jpg
    20241030_091705.jpg
    377.6 KB · Views: 8
  • 20241030_091508.jpg
    20241030_091508.jpg
    522.8 KB · Views: 6
  • 20241030_091430.jpg
    20241030_091430.jpg
    146.4 KB · Views: 7
  • 20241030_091417.jpg
    20241030_091417.jpg
    128.8 KB · Views: 6
  • 20241030_091410.jpg
    20241030_091410.jpg
    393.1 KB · Views: 7
  • 20241030_091308.jpg
    20241030_091308.jpg
    778.3 KB · Views: 6
  • 20241030_091224.jpg
    20241030_091224.jpg
    671 KB · Views: 7
Jana kulikua na uzi unasema TanRoad hoi bin taaban naona TanRoad wamejibu kibabe!
 
Ingawa Tanzania imefanya maendeleo makubwa katika kuboresha miundombinu ya barabara katika miaka ya hivi karibuni.
Hakuna ripoti rasmi kutoka kwa Statista au shirika lingine la kimataifa linaloonyesha Tanzania imepanda hadi nafasi ya 6 kati ya nchi 54 za Afrika.
Taarifa hii ina ukakasi sana Mkuu!
 
Taarifa za Machawa hizo na PAKA wa Lumumba.
 
Taarifa za Machawa hizo na PAKA wa Lumumba.
Wanafeli pakubwa sana!
Hawa wanatakiwa wakule ban! Unaanzaje kunukuu chanzo cha uongo!? Eti Statista? Yaani ujinga wa kiwango cha 5G
 
Miradi inayooneshwa yote ilijengwa miaka minne nyuma.chawa wanavituko sana kumtetea bibi Yao ambaye ameharibu uchumi wetu
 
Hii mentality ya kipiuzi! Rais si Mungu kwamba kila chenye mafanikio nchi hii ni yeye kafanya🚮🚮
 
Moderator naomba kuuliza hivi kufanya reference na quotation ya chanzo cha uongo ni kosa au sio kosa!? Je hawa Statista hawawezi kushughulikia watu kama hawa?
 
Tanzania imepaa mpaka nafasi ya 6 toka nafasi ya 16 mwaka 2022 kati ya nchi 54 za Afrika kuwa na mtandao bora wa barabara kwa mujibu wa Takwimu za mtandao wa Statista.

Hii ni kwa sababu ya kazi nzuri ya utekelezaji wa miradi ya barabara na madaraja yenye lengo la kuboresha huduma za usafiri na usafirishaji inayofanywa na serikali ya Awamu ya sita chini ya Mheshimiwa Rais Dkt

Kwa uchache tu tuone baadhi ya kazi ambazo Rais Samia Suluhu Hassan amefanikisha:-

Utekelezaji wa miradi 77 ya ujenzi wa barabara na madaraja inayoendelea kupitia TANROADS yenye thamani ya Shilingi Trilioni 4.6.

Ukamilishaji kwa asilimia 100 miradi 25 ya ujenzi wa barabara yenye urefu wa kilometa 1,198 iliyogharimu Shilingi Trilioni 1.68

Ujenzi wa Daraja la J.P Magufuli (Kigogo Busisi) ambalo linagharimu Shilingi Bilioni 717 limefikia zaidi ya asilimia 94.

Huu ni utekelezaji wa vitendo wa Ilani ya Uchaguzi ya CCM 2020 - 2025.

#SamiaKazini #HatunaMbadala2025
#TunaendaNaSamia
#TukiahidiTunatekeleza
#KaziIendelee
Umekosa cha kuposti sio lazima upost ungeenda hata kwenye ule Uzi wa kimasihara wa tunda ungepata hata mbinu ya kula kimasihara
 
Huyo BIBI hajajenga hata km 100 za rami tangu ashike madaraka
 
Back
Top Bottom