Tanzania yapaa viwago vya FIFA kwa nafasi 9, kutoka nafasi ya 146 hadi 137 kati ya mataifa 211

kirerenya

JF-Expert Member
Joined
Aug 27, 2013
Posts
1,696
Reaction score
2,253

Tanzania imepaa kwa nafasi 9 hadi nafasi ya 137 kutoka nafasi ya 146 kati ya mataifa 211 katika viwango vya ubora wa soka duniani vilivyotolewa na FIFA siku za hivi karibuni.

Hivi karibuni, timu ya Taifa Stars kutoka Tanzania imekuwa ikicheza katika kiwango kizuri ambapo iliwashinda DR Congo katika mchezo wa kirafiki kwa mujibu wa ratiba za FIFA.

Katika viwango hivyo vipya vya mwezi Aprili, Germany imeendelea kushika usukani wa dunia huku Brazil ikiwa nafasi ya pili na Ubelgiji imefanikiwa kupanda nafasi mbili juu na kufikia nafasi ya tatu.

Katika 'top ten' mataifa yanayofuata ni Ureno, Argentina,Uswiss, Ufaransa, Hispania, Chile na Poland inakamata nafasi ya 10.

Barani Afrika Tunisia inaongoza ikiwa nafasi ya 14 ikifuatiwa na Senegal katika nafasi ya 28, Congo DR nafasi ya 38, Morocco nafasi ya 42, Nigeria nafasi ya 47, Cameroon nafasi ya 51, huku Burkina Faso akiangukia nafasi ya 53.

Kwa ukanda wa Afrika Mashariki na Kati, Uganda imepanda juu nafasi nne mpaka kufikia 74, ikifuatiwa na Kenya ikiwa imeporomoka kwa nafasi 8 hadi kufikia 113, Rwanda nayo ikiporomoka kwa nafasi 11 hadi kufikia 123, Tanzania ikiwa imepanda nafasi 9 hadi kufikia 137, Ethiopia ikiporomoka kwa nafasi 8 mpaka kufikia 145 huku Burundi ikidondoka kwa nafasi 3 na kufikia 145.

Wengine ni Djibouti ambayo iko nafasi ya 198 huku Eritrea na Somalia zikiwa mkiani kabisa katika nafasi ya 206

EATV
 
Yaani mechi ya kirafiki tunapanda nafasi tisa !haya ingawa uzee unanijia vibaya
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…