Tanzania yapata mkopo wa nyongeza Dola Mil 153 kutoka shirika la fedha duniani (IMF)

Fortilo

JF-Expert Member
Joined
Apr 10, 2012
Posts
5,807
Reaction score
17,416
Kwa Mujibu wa handle ya Twitter ya Tanzania Business Insight, Tanzania itapokea mkopo wa dharura na haraka wa $153M kwa ajili ya ku support budget yetu.

Katika marejeo ya Shirika hilo la fedha duniani, inaonekana Tanzania inafanya vizur licha ya changamoto kubwa za uchumi duniani .

Sasa swali?

Hivi kwel USD 153M ni hela ya kukopa IMF? Tunaweza pata ufafanuzi?

Pia, Soma=> Ufaransa yaipa Tanzania mkopo wa Tsh. Bilioni 361.7 kuzalisha umeme wa jua



Your browser is not able to display this video.
 
Nikimtazama tu Samia anavyomsikiliza Mwigulu kwa makini kwenye hiyo picha, ndio naona chanzo kwanini tumeshapotea kama taifa.
 
Mkopo wa dharura wa haraka kwa ajili ya kusapoti budget yetu kivipi wakati mwaka wa fesha serikalini unaelekea kwisha?
Budget mpya si ndio inapikwa mkuu?
 
Mkopo wa dharura wa haraka kwa ajili ya kusapoti budget yetu kivipi wakati mwaka wa fesha serikalini unaelekea kwisha?
Bajeti zetu huwa zipo vitabuni tu
 
Hongera serikali ya awamu ya 6.
 
Na zenyewe zitapigwa tu na wachache
halafu kama kawa sisi
wanyonge tutazilipia kwenye tozo point.
 
Budget mpya si ndio inapikwa mkuu?
Unapika vipi ikiwa chakula cha mwanzo kimeshindwa kulika sasa kimegeuka kiporo, hicho kipya unachopika nacho si kitageuka kiporo vile vile?

Hatujielewi wala hatujui kitu gani tunafanya.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…