Tanzania yapata Sh trilioni 1 kufadhili programu za kilimo

Unamaanisha hizo hela zinatolewa kama charity au?
Hapana, kwenye BBT, kuna kitu kinaitwa "block farming", kwenye hii kuna wafadhili ambao wana mitaji mikubwa kilimo, haww analima mfano eka 1,000, basi atazungukwa na vijana wa BBT ambao watalima kwa mtaji wa huyo mwekezaji, mazao ambayo huyu mkulima mkubwa atayamunuwa yote kwenye mashamba ya BBT na watapigiana hesabu mwisho wa siku wanaponunuwamazao. Hapo kuna win win situation.

Mfano mwingine, kuna mfadhili kakubali kuja kuwekeza zana za kisasa za kilimo kila yalipo mashamba ya BBT.

Wengine mbolea.

Wengine mazao.

Anatowa mtaji wake mumlimie parachichi au mumfugie mbuzi aina fulani.

Mfano mzuri ni wanaofadhili ligi ya Tanzania, anasema yeye atatowa gharama zote lakini mvae jezi zenye nembo yake.
 
Approach ya Bashe na Saa100 ni Wizi tupu. Hakuna Kilimo cha hivyo.
Approach yao haidili na tatizo la Kilimo. Ila ina dili na fursa kwa wao kupiga pesa tu.
 
Hatimae chaka la kupiga hela limepatikana 🎶🎶🎶🎶
 
Ila Faiza hujaniambia ukweli bibi yangu
 
Hela zote zinakwenda kwa wakulima wa mijini...hata shamba hawalijuwi
[emoji1]

Ova
 
Niko nasoma kitabu hapa cha 'how to avoid a scam'
 
Weka vzr ndugu yangu ni mkopo au ni misaada?
 
Hapo 50% ndo zitaenda sehem husika ,mafisadi akina mwigulu wanazisubiri kama fisi
 
Kwani kile kilimo cha Bashe kimeishia wapi?

Hizo pesa wanazopewa na WB huwa wanazichezea tu, hawana maana hao wapendwa wako.
Hufuatilii kilimo Cha Bashe,unafuatilia nyuzi zinazoisema vibaya tu serikali
 
Hivi 'ufadhili' ni tofauti na mkopo?

Maana imeandikwa as if ni zawadi imetolewa. Ifikie mahali kabla serikali haijafanya maamuzi ya kutilia saini haya mambo yapelekwe kwanza bungeni na hata wananchi tushirikishwe.
Kama hujui ifadhili ni nini,una ujuzi gani wa kuishauri serikali kuhusu mambo mazito ya nchi!?
 
Alisisitiza kuwa nchi za Afrika zinapaswa kusaidiana katika masuala ya kutafuta rasilimali, uzalishaji na masoko ili kuwaondoa wananchi katika umaskini.
Ni Tanzania itakuwa na Shirika la misaada kwa ajili ya nchi nyingine?
Yaani tuwe na Tanzania Aid kama ulivyo USAID.

Ni lini tutaacha kukopa na kuomba misaada Tena yenye Mashariti na kuanza kutoa mikopo kwa wengine na Hata misaada pia?

Unadhani jambo hili kuacha kukopa na kuomba misaada na kuanza sisi kukopesha na kutoa misaada endelevu ni jambo jema kwa kizazi cha Sasa na vijavyo vya nchi hii ya Tanzania?

Natanguliza Shukrani kwa majibu yenye kuimarisha Tanzania ijitegemee.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…