Tanzania yapewa Sh. bilioni 344 za barabara

Herbalist Dr MziziMkavu

JF-Expert Member
Joined
Feb 3, 2009
Posts
42,872
Reaction score
34,363

Waziri wa Fedha, Dk. William Mgimwa (kushoto), akikabadilishana hati na Mkurugenzi wa Benki ya Dunia kwa Tanzania, Uganda na Burundi, Phillipe Dongier, kwenye hafla ya kusaini mkataba wa mkopo wa dola milioni 210 za Marekani jijini Dar es Salaam jana.


Serikali imepokea msaada wa kiasi cha dola za Marekani milioni 210 (sawa na Sh. bilioni 344.6) kutoka Benki ya Dunia (WB), zitakazotumika katika ujenzi na ukarabati wa barabara hapa nchini.

Uwekaji wa sahihi katika msaada huo uliwakilishwa na Waziri wa Fedha, Dk. William Mgimwa kwa na Mkurugenzi Mkazi wa WB, Philippe Dongier.

Dk. Mgimwa alisema fedha hizo zitatumika katika ukarabati wa barabara ya Mafinga-Igawa yenye urefu wa kilometa 140 na uboreshwaji wa barabara ya Songwe-Kasumulu kwa kujenga kituo cha kutoa huduma za pamoja katika eneo hilo.

Alisema fedha hizo pia zitasaidia kugharimia ubunifu wa miradi mbalimbali ya barabara hapa nchini na pia kusaidia kupunguza gharama za kijamii zikiwamo athari zitokananzo na barabara.

Matumizi mengine ni pamoja na kupunguza msongamano wa magari barabarani kwa kujenga barabara nyingi zaidi.

Aliongeza kuwa kiasi kingine kitatumika katika kuimarisha taasisi au vyombo vinavyosimamia usafirishaji hapa nchini.

Kwa upande wake, Mkurugenzi Mkazi wa WB nchi za Tanzania, Uganda na Burundi, Philippe Dongier, alisema mbali na fedha hizo kutumika katika miundombinu pia zitasaidia upatikanaji wa ajira kwa wananchi.

Alisema malengo ya WB ni kuhakikisha Tanzania inakuwa na miundombinu bora ili wananchi wake waweze kusafiri na kusafirisha bidhaa kwa urahisi.




CHANZO: NIPASHE

 
Barabara zitajengwa lakini si zenye ubora ili wajanja wajichotee chao mapema. Hawa viongozi hawajali wananchi wao.
 
Nchi haina vipaumbele hii hebu anagalia Mgimwa alivyotaja mambo mengi hapo hiyo hela itaisha bila hata kujua imefanya ninikwani wasiamue kutumia katika mradi mkubwa mmoja ambao utakuwa na impact kubwa? kwani wasitumie katika bara bara moja but ambayo kweli efficiency itakuwepo? kwanin wasipeleke hela yote katika reli ya kati ili watu wamikoa yote inayotegemea reli hiyo waoneze uzalishaji kupitia reli hiyo.Bado tuna safari ndefu sana
 

mkuu ukiona mtu ana mipango mingi fuatilia efficiency yao tu.
Hizo ni porojo ili donor aone kuwa anatoa pesa kwa watu makini kumbe hamna lolote. Na ujinga wa hawa ma donor wala huwa hawatakagi kujua ripoti ya hela walizotoa zimetumikaje. Na wakijifanya wanakaba sana sana wanapoozwa na sera za uwekezaji.
So you can see the viscious circle of finishing Tz resources. Bring money-many projects-less implementation-then reports full of shortfalls-requests more money-more politics- and on and on.
 
Yaani tutasubiri sana hadi kuja kumpata mtu sahihi wa kuongoza nchi yetu
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…