Miss Zomboko
JF-Expert Member
- May 18, 2014
- 4,599
- 9,532
Waziri wa Afya Dkt.Dorothy Gwajima, amepokea Chanjo za Moderna chini ya Mpango wa COVAX hii ikiwa ni Awamu ya Kwanza kwa aina hii ya Chanjo kuingia nchini kiasi cha dozi 376,320 ambazo zitatumika kuchanja wananchi 188,160.
"Tumepokea chanjo aina ya Moderna kupitia mpango wa COVAX jumla ya dozi 376,320 ambazo zitatumika kuchanja wanachi 188,160, nichukue fursa hii kuishukuru mpango wa COVAX na hii ikiwa ni awamu ya kwanza kwa aina hii ya chanjo kuingia nchini kupitia mpango wa COVAX"
"Mapokezi ya chanjo hizi za leo yanafanya jumla ya chanjo tulizopokea nchini tangu tuanze kutoa chanjo dhidi ya UVIKO 19 hadi sasa kuwa dozi 6,408,950 zikijumuisha (Sinopharm, Janssen na Pfizer), ambazo zinatosha kuchanja jumla ya watanzania 3,204,475"
"Serikali itaendelea kutoa Chanjo dhidi ya UVIKO-19 katika vituo mbalimbali vya Afya hapa nchini kwa mujibu wa miongozo iliyopo, hivyo niwaombe wanaohusika na zoezi hilo kuwajibika kwa kasi kubwa ili kuwawezesha watanzania wengi kupata chanjo mapema iwezekanavyo, Wizara ilitoa Mwongozo wa Chanjo unaofafanua vyema taratibu za utoaji wa chanjo hizi wenye lengo la kufikia uchanjaji wa asilimia 60 ya watanzania"
MillardAyoUPDATES