#COVID19 Tanzania yarekodi visa vipya 116 kati ya Machi 5 hadi Aprili 6, 2022. Maambukizi yafikia 33,842

#COVID19 Tanzania yarekodi visa vipya 116 kati ya Machi 5 hadi Aprili 6, 2022. Maambukizi yafikia 33,842

beth

JF-Expert Member
Joined
Aug 19, 2012
Posts
3,880
Reaction score
6,368
Serikali imesema kuanzia Machi 5, 2022 - Aprili 3, 2022 Visa vipya 116 vya Corona vilithibitishwa kati ya watu 25,890 waliopimwa. Jumla ya Visa vya Ugonjwa huo tangu kuripotiwa kwake Machi 2020 hadi Aprili 3, 2022 ni 33,842 huku vifo vikiwa 803.

Katika taarifa yake, Wizara ya Afya imesema kati ya Machi 05, 2022 hadi Aprili 03, 2022, wagonjwa wapya 22 walilazwa. Aidha, imeelezwa Dar es Salaam imeendelea kuwa na idadi kubwa ya watu wenye maambukizi.

Tangu kuzinduliwa Kampeni ya Chanjo mpaka kufikia Aprili 03, 2022, watu 3,318,374 walikuwa wamepata dozi kamili.

TAARIFA YA WIZARA:

7F4F3882-350E-4D5C-B269-AD200E74C3E4.jpeg

59CD1471-6573-4ABC-92EA-D1E242160332.jpeg
 
Tutapataje fedha nyingine?.

Ni sisi tu ndiyo tulibaki, Museven alijipigia mpaka akazika majeneza feki, sisi tulikuwa na matangawizi + majani ya mwarobaini 🤭!.

Kule muhimbili nako kulikuwa na chuma/chumba cha kujifukiza ahahahaaa...
 
upumbavu na upuuzi wa viongozi wachumia tumbo,swiku zote walikuwa wapi wanataka hela za misaada
 
Hii ni homa kama homa zingine za matumbo ,typhord maleria nk kwa sasa so pamoja na ugonjwa huu lazima maisha yaendelee
 
kwani bado ipo? I'm sorry !
Imenigonga wiki 2 zilizopita. Hii ya awamu hii usiombee hata kupishana nayo.

Siku ya kwanza kujisikia vibaya viungo vyote vilikuwa vinauma. Na kikohozi kigumu kibaya,kikavu. Nikaanza kutumia dawa ya maji ya kikohozi.
Nimezoea mazoezi,nikajua nikikamua zaidi ya saa 1;30 huwa vitakaa sawa. Nimezoea mazoezi asubuhi,siku hiyo nikaenda jioni nikakamua sana saa 1;45. Ikawa kosa la kwanza,kesho yake mchana nikajisikia baridi kali sana. Nikafikiri nina maralia. Nikavuta metercafllin nikazigonga 3,ikawa kosa la pili. Usiku nilikuwa vibaya sana. Kesho mwili wote ulikuwa unauma,yaani ukigusa ngozi inakuwa kama sio yako. Ngozi ya juu ya mgongo inauma hatari,haitaki ulale.

Hapo kwenye kikohozi ndio panauma,panakera hatari,panakuwa kama pamejaa wadudu. Siku ya 3 nilishindwa hata kuendesha gari kurudi home kutoka job. Kula ndio kabisa unaona chakula chochote hakiko sawa. Sijawahi kwenda hosp lakini siku ya 5 nilijipeleka mwenyewe hosp. Pima zaidi ya magonjwa 8 hawaoni kitu. Pima yote kavu. Wakaniambia tu itakuwa mafua na kikohozi ndio vinavyokusumbua. Lakini mafua nilikuwa sina,ila kikohozi. (Lakini naona madoctor wenyewe walishajua nasumbuliwa na nini)

Siku 9 nzima niko vibaya sana. Najikaza tu kwenda kazini. Inaachia kidogo kidogo. Vifo ni vingi tu vipo hasa huku mikoani. Si unajua wengi waligoma kuchanjwa. Kwa kweli mimi si muumini wa kichanjwa ila nawaaasa wenye miili mdebwedo kama sehemu zako za kazi unakutana na watu wengi bora ukachanjwa. Hii ngoma si ya kuichezea inakutoa chap.
 
kwani bado ipo? I'm sorry !
Bado iko kibao tu, imemuondoa mama yetu mzazi 4th January 2022 imemuondoa mdogo wangu j3 ya wiki iliyopita maziko yalikuwa alhamis ya wiki hiyo hiyo, mzigo bado upo tuendelee kuchukua tahadhari
 
Bado iko kibao tu, imemuondoa mama yetu mzazi 4th January 2022 imemuondoa mdogo wangu j3 ya wiki iliyopita maziko yalikuwa alhamis ya wiki hiyo hiyo, mzigo bado upo tuendelee kuchukua tahadhari
Pole Sana mkuu
 
Imenigonga wiki 2 zilizopita. Hii ya awamu hii usiombee hata kupishana nayo.

Siku ya kwanza kujisikia vibaya viungo vyote vilikuwa vinauma. Na kikohozi kigumu kibaya,kikavu. Nikaanza kutumia dawa ya maji ya kikohozi.
Nimezoea mazoezi,nikajua nikikamua zaidi ya saa 1;30 huwa vitakaa sawa...
Mkuu umetumia dawa gani sasa??
 
Mkuu umetumia dawa gani sasa??
Sana dawa ya maji ya kikohozi ile inaitwa ngoja nipate picha yake nakutumia. Hiyo nilitumia chupa ya kwanza yote,kavu bado kikohozi kipo tu. Doctor kanishauri nigonge chupa cha pili. Ndio kikapotea. Lakini hizo hali zingine kama ngozi kuuma na viungo na kichwa hakuna dawa waliyonipa. Vimeishia vyenyewe. Sitaki hata kukumbuka ile homa
 
Balaa sana nitumie mkuu naona kuna kihali kinaninyemelea hapa

Back
Top Bottom