kwani bado ipo? I'm sorry !
Imenigonga wiki 2 zilizopita. Hii ya awamu hii usiombee hata kupishana nayo.
Siku ya kwanza kujisikia vibaya viungo vyote vilikuwa vinauma. Na kikohozi kigumu kibaya,kikavu. Nikaanza kutumia dawa ya maji ya kikohozi.
Nimezoea mazoezi,nikajua nikikamua zaidi ya saa 1;30 huwa vitakaa sawa. Nimezoea mazoezi asubuhi,siku hiyo nikaenda jioni nikakamua sana saa 1;45. Ikawa kosa la kwanza,kesho yake mchana nikajisikia baridi kali sana. Nikafikiri nina maralia. Nikavuta metercafllin nikazigonga 3,ikawa kosa la pili. Usiku nilikuwa vibaya sana. Kesho mwili wote ulikuwa unauma,yaani ukigusa ngozi inakuwa kama sio yako. Ngozi ya juu ya mgongo inauma hatari,haitaki ulale.
Hapo kwenye kikohozi ndio panauma,panakera hatari,panakuwa kama pamejaa wadudu. Siku ya 3 nilishindwa hata kuendesha gari kurudi home kutoka job. Kula ndio kabisa unaona chakula chochote hakiko sawa. Sijawahi kwenda hosp lakini siku ya 5 nilijipeleka mwenyewe hosp. Pima zaidi ya magonjwa 8 hawaoni kitu. Pima yote kavu. Wakaniambia tu itakuwa mafua na kikohozi ndio vinavyokusumbua. Lakini mafua nilikuwa sina,ila kikohozi. (Lakini naona madoctor wenyewe walishajua nasumbuliwa na nini)
Siku 9 nzima niko vibaya sana. Najikaza tu kwenda kazini. Inaachia kidogo kidogo. Vifo ni vingi tu vipo hasa huku mikoani. Si unajua wengi waligoma kuchanjwa. Kwa kweli mimi si muumini wa kichanjwa ila nawaaasa wenye miili mdebwedo kama sehemu zako za kazi unakutana na watu wengi bora ukachanjwa. Hii ngoma si ya kuichezea inakutoa chap.