Tanzania yaruhusu maziwa na sigara kutoka Kenya, nayo Kenya yaruhusu ngano na gesi kutoka Tanzania

Tanzania yaruhusu maziwa na sigara kutoka Kenya, nayo Kenya yaruhusu ngano na gesi kutoka Tanzania

MK254

JF-Expert Member
Joined
May 11, 2013
Posts
32,408
Reaction score
50,809
Uhusiano wa kibiashara baina ya nchi hizi mbili ulikua umeanza kudorora, lakini rais Magufuli na rais Uhuru wameongea na kurekebisha. Waziri wa mambo ya kigeni wa Tanzania bwana Mahiga amekuja Nairobi na wakaingia kwenye makubaliano mapya.

Pia wamekubaliana kubuni jopo kazi ambayo itakua na majukukumu ya kuweka sawa mkwaruzano ambao umekua ukitokea mara kwa mara baina yetu.

-------------------------------------------------------------

Kenya has lifted restrictions on wheat flour and cooking gas imports from Tanzania, which has in turn allowed milk and cigarettes from Kenya.

The countries’ Foreign Affairs ministers said in Nairobi on Sunday that the move followed discussions between presidents Uhuru Kenyatta (Kenya) and John Pombe Magufuli.

“The Republic of Kenya and the United Republic of Tanzania will lift any other restrictions that affect products and services exchanged between the two countries,” they said in a statement read by Tanzania Foreign Affairs minister Augustine Mahiga, who is also in charge of the East African Community Affairs docket.

TRAVEL
Kenyans will however still have to apply for visas when travelling to Tanzania for business, though Mr Mahiga said they were looking into the issue.

“If there are still some bottlenecks, we are pledging to address them to allow our citizens to travel easily,” he said.

The two countries would continue to man border posts jointly while the production of an East African Community (EAC) passport would help ease movement across the states, he said.
COMMITTEE
The two countries also agreed to set up a joint technical committee chaired by the Foreign Affairs ministers and comprising the EAC Affairs, Trade, Finance, Interior, Energy, Agriculture, Transport and Tourism ministries and any other relevant government agency.

Kenya banned the importation of cooking gas from Tanzania in April, with the Energy ministry at the time saying the move was meant to curb the proliferation of illegal filling plants.

LPG GAS
Petroleum Principal Secretary Andrew Kamau said at the time that Mombasa would be the only point of import for Liquid Petroleum Gas.

Tanzanian LPG companies export to Kenya about 40,000 tonnes of cooking gas annually.

TARIFF

Gas from Tanzania is cheaper because their costs of offloading at the ports in Tanga and Dar es Salaam are lesser than those in Mombasa.

Kenya had said it would only allow wheat flour and other products milled from grain produced in Tanzania or whose full Common External Tariff rate has been applied.
Tanzania signs new business deal with Kenya
 
Kenya wamejichokea sana Tz tungeimarisha export sector wakenya wangekua customers wetu ,fikiria tuna ng'ombe M 17 (second after Ethiopia) je kuna haja ya ku import maziwa?

Sent using Jamii Forums mobile app
Halafu sisi tuna export gesi , hivi hii gesi yetu hadi sasa ni nani anayefahamu hasa faida yake kwa watanzania?

Gesi hii imetosheleza mahitaji ya tanzania? Tuliambiwa shida ya umeme itaisha lakini bado shida ipo.

Na ku-import maziwa sijaelewa kabisa yaani kwa sababu inaonekana hatuna upungufu wa maziwa. Tulihitaji kitu ambacho kwetu ni adimu sasa maziwa ya nini? Tunaupungufu wa maziwa?

Any way mi naona hayo makubaliano hayata leta tija yoyote.

In short Tz tuna comparative and competitive advantages ya vitu vingi kushinda hao jirani zetu

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Halafu sisi tuna export gesi , hivi hii gesi yetu hadi sasa ni nani anayefahamu hasa faida yake kwa watanzania?

Gesi hii imetosheleza mahitaji ya tanzania? Tuliambiwa shida ya umeme itaisha lakini bado shida ipo.

Na ku-import maziwa sijaelewa kabisa yaani kwa sababu inaonekana hatuna upungufu wa maziwa. Tulihitaji kitu ambacho kwetu ni adimu sasa maziwa ya nini? Tunaupungufu wa maziwa?

Any way mi naona hayo makubaliano hayata leta tija yoyote.

Sent using Jamii Forums mobile app
Ndugu Industry ya Gas inahitaji uwekezaji wa mabilioni ya pesa
Bado serikali yako ipo kwenye Hatua za awali za ujenzi wa Kiwanda cha kuchakata gesi kule Lindi kitakachogharimu zaidi ya Trillion 60 za Kitanzania. Hapo ndio tutaona faida ya gesi, na huenda ikaenda hadi 2030
Hata hivyo, Hadi sasa zaidi ya asilimia 50 ya Umeme wa grid ya Taifa unazalishwa kwa nishati inayotokana na gesi asilia ndio maana ule mgao wa Umeme uliotusumbua miaka mitano iliyopita haupo tena.
Ujenzi wa mitambo zaidi ya Kufua Umeme kutoka kwenye gesi asilia unaendelea Pale Kinyerezi ambao utaongezea megawati 450 kwenye grid ya Taifa.
Hapo kwenye Maziwa nakubaliana na wewe.
Tuna maziwa ya kumwaga huko vijijini, Mimi binafsi nipo mjini na hayo maziwa yao ya pakiti huwa situmii, natumia maziwa fresh yaliyokamuliwa moja kwa moja.
Serikali iruhusu imports za vitu walau vyenye tija.
 
He hee, MK254 vipi ile mashine ya kukagua gesi fake inoliopuka toka Tz and other bs. Unyang'au tu ndio mnaweza, na tutawanyoosha, ndio kwaanza kunakucha pande hii. Mtabana na kuja na mashine za kila aina, ila mtaachia tu. Nyinyi hamuwezi isumbua Tz hata kidogo, we have all the advantages.
 
Izi nchi ua zina mambo ya ajabu sana wanaoneana wivu, wakati ata kweny robo ya uchumi wa dunia hawamo, Maskini ni maskini tu,... Na atabaki maskini,
 
Kenya wamejichokea sana Tz tungeimarisha export sector wakenya wangekua customers wetu ,fikiria tuna ng'ombe M 17 (second after Ethiopia) je kuna haja ya ku import maziwa?

Sent using Jamii Forums mobile app
Hata Waethiopia wanakunywa maziwa ya Kenya. Tuna ngombe wakuswaga kwenye mashamba ya watu na si wa biashara
 
Ukiwa na ng'ombe kama uko strategically unaweza ku plan wa beef au hao maziwa
Unakua na hiyo potential

Sent from my SM-J110H using JamiiForums mobile app
Longido kujenga Kiwanda kikubwa cha nyama nchini
16:39 0
Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Longido, Jumaa Mhina alisema jana kuwa kiwanda cha nyama kitakachojengwa na Kampuni ya Eliya Foods Overseas Ltd, kitakuwa na uwezo wa kuchinja ng’ombe 250, mbuzi 250 na kondoo 250 kwa siku.

Mkurugenzi huyo aliyasema hayo jana wakati wa ziara ya Naibu Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais (Tamisemi), Suleiman Jafo wilayani Longido Mkoa wa Arusha.

Alisema wilaya hiyo ina ng’ombe 216,000, mbuzi 399,000 na kondoo, 301,000.

Mkuu wa Wilaya ya Longido Daniel Chongolo, alimwambia naibu waziri huyo kuwa lile tatizo la wafugaji kukosa soko la uhakika la mifugo yao sasa limepatiwa ufumbuzi baada ya kuanza ujenzi wa soko la kimataifa wilayani humo.

Alisema mradi huo unaojengwa eneo la Namanga, utawasaidia wafugaji kuuza mifugo yao badala ya kuipeleka nchini Kenya.

Chongolo alisema ujenzi huo ni sehemu ya mradi wa kuboresha miundombinu ya masoko, ongezeko la thamani na huduma za fedha vijijini (MIVARF) uliopo chini ya ofisi ya Waziri
 
Ukiwa na ng'ombe kama uko strategically unaweza ku plan wa beef au hao maziwa
Unakua na hiyo potential

Sent from my SM-J110H using JamiiForums mobile app
Jenista: Mifuko ya jamii kuzalisha ajira 300,000
Kuchapa

0 Comments

WAZIRI wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu, Sera, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na wenye Ulemavu, Jenista Mhagama amesema kuwa Mifuko ya Hifadhi ya Jamii nchini inatarajia kuwekeza na kujenga viwanda zaidi ya 25 katika maeneo mbalimbali hivyo kuzalisha ajira zaidi ya 300,000 kwa Watanzania wakiwemo vijana.

Mhagama alisema hayo juzi wakati alipotembelea kiwanda cha kusindika nyama cha Nguru Hills Ranch kilichoko wilayani Mvomero, mkoa wa Morogoro. Alisema uwekezaji katika viwanda utaongeza kiwango cha asilimia ya Watanzania watakaojiunga na mifuko ya hifadhi za jamii na kufanikisha kupunguza kiwango cha ukosefu wa ajira ambacho kwa sasa kimeshuka kutoka asilimia13 hadi kufikia asilimia 10.3.

Waziri Mhagama aliambatana na Naibu wake, Anthony Mavunde na kupokewa kiwandani hapo na Uongozi wa Serikali ya Mkoa wa Morogoro ukiongozwa na mkuu wa mkoa huo, Dk Kebwe Stephen ambaye alifuatana na mkuu wa wilaya ya Mvomero, Mohamed Utaly na watendaji wengine wa serikali ya wilaya na mkoa wakiwemo viongozi wa Kijiji cha Wami Sokoine. Hata hivyo, alisema ziara hiyo ililenga kufuatilia maelekezo aliyoyatoa Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa alipofanya ziara mkoani Morogoro, Agosti 3, mwaka 2016 na kukitembelea kiwanda hicho ambapo moja ya changamoto iliyojitokeza ni ukosefu wa fedha za ukamilishaji kabla ya kuanza uzalishaji wake.

Alisema kutokana na mazungumzo yaliyofanyika mapema mwaka huu, Mfuko wa Pensheni wa LAPF umefikia uamuzi kutoa fedha za kuwekeza kwenye kiwanda hicho ili kumalizika kazi zilizobaki na kukiwezesha kufanya kazi za uchinjaii wa ng’ombe na mbuzi ikiwa na kutoa ajira kwa wananchi miezi sita ijayo mwaka huu. Waziri Mhagama alisema kuwa, Mfuko wa LAPF utawekeza fedha katika kiwanda hicho kulingana na utaratibu wa kisheria utakaosimamiwa na Mamlaka ya Usimamizi na Udhibiti wa Sekta ya Hifadhi ya Jamii (SSRA) ili kuona fedha za wanachama zinaingizwa kwenye uwekezaji ulio salama na wenye kuleta faida kwa mfuko na serikali.

Hata hivyo, waziri huyo alisema kuwepo kwa kiwanda cha kuchakata nyama wilayani Mvomero mkoani Morogoro kitamaliza mgogoro wa muda mrefu kati ya wakulima na wafugaji kwa kuwa wafugaji watapata fursa ya kuuza mifugo yao kiwandani hapo na wakulima kuzalisha nyasi za malisho. Kwa upande wake Mkurugenzi na Mshauri wa Kiwanda cha Nguru Hills Ranch, Dunstan Mrutu alisema kiwanda hicho chenye uwezo wa kuchinja ng’ombe 300, mbuzi na kondoo 1,500 kwa siku kutokana na uwezeshaji wa fedha kutoka LAPF kitatarajiwa kufunguliwa ndani ya miezi sita ijayo mwaka huu.

Mkurugenzi huyo alisema takriban asilimia 80 ya nyama itakayochinjwa kiwandani hapo itafungashwa na kuuzwa nje ya nchi, hasa Uarabuni kwa sababu nyama ya mbuzi ya Tanzania imebainika kuwa na mvuto maalumu katika nchi hizo. Alisema nia yao ni kuitikia mwito wa Rais John Magufuli wa kutaka viwanda vizalishe viatu nchini kuanzia vya majeshi na wananchi wote ambapo wamepanga kuanzia mwakani wataanza kuuza bidhaa hizo.
 
Pia GEPF ikishirikiana na ranchi ya taifa NARCO pamoja na bank ya uwekezaji ya taifa TIB wanajenga kiwanda kikubwa cha nyama mkoa wa Pwani.
 
Halafu sisi tuna export gesi , hivi hii gesi yetu hadi sasa ni nani anayefahamu hasa faida yake kwa watanzania?

Gesi hii imetosheleza mahitaji ya tanzania? Tuliambiwa shida ya umeme itaisha lakini bado shida ipo.

Na ku-import maziwa sijaelewa kabisa yaani kwa sababu inaonekana hatuna upungufu wa maziwa. Tulihitaji kitu ambacho kwetu ni adimu sasa maziwa ya nini? Tunaupungufu wa maziwa?

Any way mi naona hayo makubaliano hayata leta tija yoyote.

Sent using Jamii Forums mobile app
Gas tunayotumia kupika haizalishwi Tanzania inakuwa imported toka nje. Ndiyo hiyo hiyo inayopakiwa kwenye mitungi ikauzwa kenya.
Sisi bado gas tunayozalisha haijawa processed kwa matumizi ya nyumbani.
 
Gas tunayotumia kupika haizalishwi Tanzania inakuwa imported toka nje. Ndiyo hiyo hiyo inayopakiwa kwenye mitungi ikauzwa kenya.
Sisi bado gas tunayozalisha haijawa processed kwa matumizi ya nyumbani.

Kama Tanzania tunafaidikaje kuipelela hiyo gesi Kenya hadi kuleta ugomvi wa kusutana na gesi yenyewe hatuzalishi?
 
Back
Top Bottom